Chama cha siasa kinategemea kura za wateja unlike companies ambazo zina leverage kwenye various business lines not necessarily the entire population. Kwahiyo umepotosha.
Nashangaa sana genge la mbowe lina vijana wajinga sana .
Vijana wasiojua katiba ya chama ,wasiojua katiba ya nchi ,wasiojua historia ya hivi vyama wala hawajui chochote nyuma ya mwaka 2015 .
Labda tuwakumbushe tu wapumbavu na Machawa wa Mbowe.
Mwaka 1995 uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi. Mbowe aligombea jimbo la Hai ambako ni nyumbani kwake .
Wakati huo nilikua nasoma sekondari huko huko nyumbani Moshi . Kuna watu wanafikiri kuwa nampiga vita Mbowe wakidhani Wachagga wote wanamuunga mkono kwa kila kitu .
Mwaka 1995 mbowe alishindwa na mgombea wa NCCR Mageuzi kwenye uchaguzi . Hapakuwa na tume na tume huru wala katiba mpya .
Kusema kuwa Eti Mbowe ndiye aliyejenga Chadema ni Ux3ng3 mkubwa sana. NCCR mageuzi ilishinda Mbowe kwenye jimbo la nyumbani anakotoka yeye na Edwin Mtei.
Ndani ya miaka minne Chadema ya Edwin Mtei na Mbowe ilishindwa kujijenga kwenye jimbo la nyumbani wanakotoka na alipogombea Mbowe .
Mbowe alikua kijana wa miaka 35 ' Kwenye uchaguzi huo alitumia fedha nyingi sana. Tuliamishwa kuwa alikua anafanya biashara ya madawa ya kulevya pale Bilcanas kwenye Casino yake maarufu iliyovunjwa na JPM baada ya mbowe kuasi na kushundwa kufanya kazi maalumu aliyokua amepewa ya kuwabaini wauza unga na wateja wa Casino.
Tuachane na hayo .
Jimbo la Hai ilichukuliwa na Mgombea wa NCCR mageuzi. Chama kilichomsimamisha Mrema ndani ya miezi michache tangu atoke CCM na kujiunga na NCCR Mageuzi. Wakati huo hapakuwa na Whasap wala Face book wala twitter wala Instagram wala simu za mikononi hazikua nyingi . Wakati huo TV ilikua moja tu huko mikoani yaani ITV na watu wachache walikua wanamiliki tv iliyokua inauzwa zaidi ya sh.laki 4 mpaka 5 kwa nchi 21 ambayo kwa sasa hivi ni zaidi ya sh.mil.5 za leo.
Hata hivyo Watanganyika walifuatilia Radio na tv chache na wakamfuata Mrema kumuunga mkono maana alikua mtu mwadilifu na aliyepinga rushwa ndani ya serikali ya CCM.
Kuwadharau wapiga kura eti hawajui kuwa Mbowe ni king'ang'anizi na anakifanya chama kupotezea mvuto ni kuwadharau wananchi na wasomi na wanaharakati waliotumika kwa miaka mingi kukijenga chama.
Wakati huo Mbowe anakataliwa na Wamachame kule nyumbani kwao Hai kwa tiketi ya Chadema ,kule moshi mjini kwa watu wa makabila mchanganyiko Philemon Ndesamburo alishinda ubunge kwa tiketi ya Chadema . Kule Karatu Willbrod Slaa akashinda Jimbo la Karatu kwa kwa tiketi ya Chadema .Wakati huo Dr.Slaa alikua anatokea CCM akaingia ndani ya Chadema ndani ya wiki mbili akaondoka na wanachama wa CCM na kushinda ubunge. Hapo Mbowe hakujenga chama nyumbani kwake lakini watu walikua wanafuatilia siasa kupitia kwenye magazeti na redio na tv chache sana.
Kaburu kule Kigoma akamgakagaza Mgombea wa CCM mahakamani . Kule Bunda Mzee Wasira kwa tiketi ya NCCR akamgalagaza Mgombea wa CCM.
NCCR ilpata kura nyingi sana kwa mgombea wa Urais ambaye alikua ni Mrema .
Mrema ndani ya NCCR alikubalika nchi nzima bila kujali vyama ,kabila wala dini yake.
Kilimanjaro jimbo lililopata Mbunge na madiwani wengi kutoka Chadema lilikua ni jimbo moja tu la Ndesamburo Moshi mjini .
Mbowe na Mtei walishindwa kujenga Chama chao jimboni kwao hivyo Mbowe akapigwa chini pamoja na kugawa fedha nyingi sana kwenye uchaguzi huo. Mashuleni tulikula sana mpunga kwa sababu ya kampeni za Mbowe .
Kula kwa Mbowe kura kwa NCCR.
Kwa hiyo Mbowe na genge lake la wala rushwa kudharau nguvu ya umma kwa kutumia fedha ni ni kukiua chama.
Miaka 30 huku pakiwa na vyombo vya habari vingi sana historia itajirudia kula kwa Mbowe kura kwa Lisu. Mbowe atatumia pesa nyingi sana kununua wajumbe kwa lengo la kulinda heshima yake binafsi kwa kudhani kuwa akishindwa ni fedheha ila hata amini kitakachotokea . Atapandwa na hasira na presha kubwa sana kwa hasara atakayoipata kutokana na hasara kubwa ya kupoteza pesa nyingi.
Wajumbe wakimfuata Mbowe na tamaa zake na kumchagua bila kusikiliza maoni ya wananchi wataua chama maana kampeni za ubunge ,udiwani na urais zitakua ngumu sana sana kuuza sera za Chadema ambazo hazitekelezwi kwa vitendo .Wetu wengi hasa mashabiki wa Chadema hawatapiga kura . Hii itapelekea ACT kushika nafsi ya pili na kuwa chama kikuu cha upinzani.