Mbowe: Kilichofanyika kwa kina Mdee ni Uhuni. Rais wasitishie mishahara

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema kilichofanyika kwa wabunge 19 waliopelekwa bungeni bila idhini ya chama ilikuwa ni uhuni, na ni kuvunja Katiba.

Amesema wabunge hao walikuwa ni viongozi wao, hata hivyo mchakato wa kuwapeleka bungeni haukuwa mchakato wenye baraka za chama. Wale walikuwa sehemu yetu, lakini waliowasaidia kuingia bungeni ni wenzako (Rais Samia).

Baadhi ya vyombo vya habari vilipotosha kusema kuwa CHADEMA iliridhia kuwapeleka wabunge wale bungeni. Wale wabunge hawakilishi mtu wanawakilisha familia zao, bunge na spika wameamua kuwalinda.

Wewe Rais ndio unayeidhinisha mishahara yao, liangalie hili uepushe matumizi mabaya ya kodi za wananchi kwa wabunge wale wasiomuwakilisha mtu.

Mbowe ameyasema hayo akiongea na wanawake wa CHADEMA katika Siku ya Wanawake Duniani, ambayo Mgeni Rasmi alikuwa Rais Samia.
 
Hahaha, walioshindwa kuvumilia ile vita 2015-2020 wana mengi ambayo wanatamani yapite haraka yaishe.
 
Mbowe anajua chadema ni majuha, anayazungusha tu
Unaonekana unajua san ukwel juu ya vovido 19! Kwann usitupe evidence juu ya nan aliwaweka na kuwapa ubunge? Tuwekee mkuu huo ukwel
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…