Tetesi: Mbowe kujiuzulu mwezi Novemba

Status
Not open for further replies.

security guard

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2011
Posts
799
Reaction score
603
Taarifa za kuaminika kutoka katika vyanzo nyeti katika chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimedai kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Mhe Freeman Aikael Mbowe yuko mbioni kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti wa chama hicho kutokana na kile kinachodaiwa kuchoshwa kunyooshewa vidole na kutuhumiwa kukiuza Chama hicho kwa Lowassa.

Tangu Ndugu Lowassa alipoamua kujiunga na Chama hicho mwishoni mwa mwezi October mwaka 2015, tuhuma za moja kwa moja zilielekezwa kwa Mhe Mbowe kutoka kwa washirika wake wa karibu akiwemo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Dr Wilbroad Slaa kuwa amepokea hongo ya takribani bilioni 20 ili kumpoitishia mgombea huyo aiyekatwa CCM kwa tuhuma za ufisadi.

Mwenyekiti Mbowe, amefikia hatua hiyo baada ya katibu Mkuu wa sasa na viongozi wote walioteuliwa na kuchaguliwa ndani ya chama hicho kuelekeza utii wao kwa Lowassa na kuacha kumtii Mhe Mbowe, imethibitika ndani ya chama hicho kuwa center of power imehama kutoka kwa Mwenyekiti na kuhamia kwa Mhe Lowassa ambapo Wabunge, Madiwani na Mameya wote wanasikiliza kauli na maelekezo ya Mhe Lowassa.
 
Ingekuwa mimi ndio wewe au hata wengine, nisingetuma thread ambayo sina uhakika nayo!
 

Boresha Tittle yako andika "Chadema Kufa mwezi Novemba" maana akijiuzuru huyo tu hakuna Chadema tena
 
Dah..Halafu afanye nini na ile Club imefungwa?😎
 
Kweli hoja kwa hoja propaganda kwa propaganda
 
Hata akijiuzuru, ataendelea kukumbukwa kama mtu kigeugeu aliyewakatisha tamaa wapenda mabadiriko ya ukweli,
Na kukubali kuua msingi wa chama kwa sababu ya tamaa yake ya kuabudu pesa!
 
Unauza gari lakini bado unataka kulitumia kwa shughuli zako. La msing mkabidhi mnunuzi wa gari card akabadili jina TRA
 
Maelezo yako yana mapungufu! Upande mmoja Mbowe amechoka kunyooshewa vidole kutokana na kumleta Lowassa! Katika hali ya kawaida, kama tatizo ni Lowassa basi tusingetarajia Lowassa huyo huyo awe na influence ndani ya chama kwavile hatakiwi!

Kwa upande mwingine, unadai center of power ipo kwa EL kiasi kwamba Wabunge, Madiwani na Mameya utii wao ni kwa EL. Hao watu ni muhimu sana kwa chama!! Suala la utii wao kuwa kwa EL inaonekana wanamkubali EL!!

Sasa Mbowe ana sababu gani ya kutaka kususa kutokana na kauli za watu wa nje kuhusu kumleta EL ikiwa watu wa ndani wenyewe hawana tatizo na EL hadi kufikia kumtii?
 
Hata akijiuzuru, ataendelea kukumbukwa kama mtu kigeugeu aliyewakatisha tamaa wapenda mabadiriko ya ukweli,
Na kukubali kuua msingi wa chama kwa sababu ya tamaa yake ya kuabudu pesa!

mjasiriamali wa kisiasa

Sweet Mangi
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…