Tetesi: Mbowe kujiuzulu mwezi Novemba

Tetesi: Mbowe kujiuzulu mwezi Novemba

Status
Not open for further replies.
Kuna taarifa zinazoenea kwenye mitandao ya kijamii zisemazo Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe anatarajia kujiuzulu Mwezi wa Novembe na kuainisha sababu Lukuki zisizo na ukweli wowote. Nipropaganda za watu wasiokitakia chama mema.

Habari hizo nizakuzipuza hazina ukweli wowote ni upotoshaji wa kiwango kikubwa.

Nimatumaini yetu mamlaka husika mtachukuwa hatua stahiki kwa mtu aliyeanzisha habari hizo za kupotosha.

CHADEMA
 
Kitendo bila kuchelewa.
Sio yule jamaa kaitwa bukoba weeeeee mpaka watu sauti zimewakauka.
 
Asante kwa taarifa tusubiri mamlaka kama zipo na zinafanya kazi zitatupa majibu juu ya stahiki iliyochukuliwa.
 
Hao watukua wale wa Lumumba bk7 ndio wanaeneza hizo habari.
Maana nimeona uzi unaosema kua Kinana atajiuzuru November humu JF.
 
Angekuwa amezushiwa wa ccm basi aliyetuma uzi huu angesakwa kwa uchochezi.
 
Kwani wewe ni msemaji wa Mbowe? Hata wakati ule iliposemekana Lowasa anajiunga na CHADEMA mlikanusha. Asa yupo wapi?
 
Hii taarifa imekanushwa na wenyewe CHADEMA (they responded very quick). Kama mnaweza nanyi (CCM/Magamba) kanusheni ile iliyoandikwa na Mwanahalisi kuhusu Kinana kuachia ngazi ifikapo Novemba.
 
Wakati fulani nilipopata habari hizi, nilijua ni muendelezo wa siasa zetu zisizo na afya njema.

Ila nilipata kusikia pia kuwa hivi sasa Meya wa Kinondoni, rafiki yangu Jacob pamoja na mameya wengine wa Jiji mama la Dar es salaam wamekuwa watu wa karibu na familia ya Mhe Lowassa.

Nyumbani kwa Mhe Lowassa ni ofisi ya pili ya Meya huyo wa Kinondoni, mwanzoni sikuwa naamini sana maana maneno maneno ni mengi, ila thread hii inanipa picha nyingine ambayo inakaribia kuondoa ule walakini niliyokuwa nayo hapo kabla.

Lisamwalo lipo, tusubiri hiyo Novemba.
 
WanaJamvi,

Habari iliyoandikwa na MwanaHalisi leo "JPM na Kinana Hapatoshi' ndio iliyopelekea watu wa hapo Lumumba kujaribu kuipoteza kwa kuzusha habari hii ya uongo

Ni mbinu ya kitoto sana.İmeandikwa Kinana anapanga kujiuzulu
 
WanaJamvi,

Habari iliyoandikwa na MwanaHalisi leo "JPM na Kinana Hapatoshi' ndio iliyopelekea watu wa hapo Lumumba kujaribu kuipoteza kwa kuzusha habari hii ya uongo

Ni mbinu ya kitoto sana.İmeandikwa Kinana anapanga kujiuzulu
Ben,
Umepewa nafasi ya usemaji wa Chama..?

lakini kwanini msitafute hoja za msingi, kuelezea kinagaubaga mgawanyo wa mamlaka ndani ya Chama kwa sasa, maana msiendelee kuficha maradhi, kifo KIPO...kitawaumbua.

Binafsi bila kuegemea kwenye taarifa za mleta thread nimesikia kuwa Meya wa Kinondoni in particular amekuwa mtiifu kwa Mzee wa Monduli kuliko Mwenyekiti wake...mnaweza kutolea ufafanuzi wa kutosha na mkaeleweka, kuliko kukimbilia kusema kuwa maneno haya ama taarifa hii ni sababu ya Mwanahalisi kuandika.....majibu rahisi kiasi hiki katika maswali magumu ndio yanawapekela mrama siku zote.

Mimi nimeanza kusikia haya kabla hata ya habari ya Mwanahalisi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom