Emanuel Jumanne John
Member
- Sep 28, 2014
- 78
- 113
Sasa imethibitika kuwa Bodi ya MCC iliyokaa tarehe 16 Dec 2015 imehairisha rasmi kuidhinisha msaada wa Millenium Challenge uliokuwa umekusudiwa kwa Tanzania kwa mwaka wa fedha 2016.
Sababu kuu mbili zilizosababisha uamuzi huo ni:
1. Mkwamo wa Uchaguzi wa Rais na Wawakilishi Zanzibar na
2. Matumizi mabaya ya sheria ya makosa ya mtandao hususan kuhusiana na uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa 2015.
Kauli yangu juu ya jambo hili ni hii;
1. Ubabe wa baadhi ya viongozi wa CCM ni janga la Taifa. Kuchelewa kupatikana kwa fedha za MCC si tu kunachafua jina la nchi na hadhi yake katika medani za kimataifa, bali kutaathiri kwa kiasi kikubwa miradi yote iliyo chini ya ufadhili wa MCC.
2. Sheria ya makosa ya mtandao (Cyber Crime Act 2015) ni sheria mbaya sana inayokinzana na kukua kwa technologia ya habari na mawasiliano. Aidha, kwa makisudi kabisa inafifisha uhuru wa kupashana habari na ni dhahiri ilitungwa kwa nia mbaya ya kuthibiti kijinai uchaguzi mkuu.
Tuliipinga sheria hii Bungeni na ikapitishwa usiku wa manane kwa ubabe wa wabunge wa CCM na hata tulipomtaka rais Kikwete asiisaini aliisaini kibabe akijua anaandaa mazingira gani ya "kihalifu".
Sheria hii ilitumika kuvamia vituo vyetu vya kukusanya matokeo ya kura za rais na wabunge na mpaka Leo vijana wetu zaidi ya 161 wana kesi za "kubumba" mahakamani.
Aidha Sheria hii ilitumika kuficha dhana ovu kuvamia kituo cha Sheria na haki za binadamu (LHRC) waliokuwa wakikusanya matokeo ya kura za Rais .
Vile vile Sheria hii imetumika kuwakamata na kuwaweka ndani na hata kuwanyima dhamana vijana wetu ambao walituunga mkono katika uchaguzi mkuu.
Namtaka rais Magufuli achukue hatua za kiuongozi na kiutawala kwa kufanya yafuatayo:
1. Aumalize mgogoro wa kisiasa Zanzibar kwa kuhakikisha kuwa mshindi halali anatangazwa .
2. Achukue hatua ya kuifanyia marekebisho makubwa Sheria ya makosa ya mtandao katika bunge lijalo. Aidha wale wote waliobambikiwa kesi amuamuru DPP kuzifuta kesi hizo Mara moja.
Hatua hizo zitalinusuru taifa na hasara ya kupoteza mabilioni hayo ya MCC na zaidi kuepusha kuporomoka zaidi kwa biashara ya Utalii nchini Zanzibar.