Mbowe: Kukosa pesa za MCC Inachafua jina la nchi ktk medani za kimataifa

Mbowe: Kukosa pesa za MCC Inachafua jina la nchi ktk medani za kimataifa

Misaada enyewe ilikua inaishia kwenye semina na posho,damn.....hatuna shida nayo
 
Nitakua proud zaidi kama tutaweza hata kuraise 50% ya MCC money wenyewe na kutekeleza walichotaka kusupport
 
Nyakati Za Magufuli Sio Za Kulialia Hivi. Cyber Crime Tumetunga Wenyewe Kwa Kuona Inatufaa Na Mambo. Hatuwezi Kulazimishwa Kufanya Tusiyotaka Kama Taifa Kisa MCC
 
Mawazo haya ya Mbowe yazingatiwe katika falsafa ya hapa kazi tu.

Kila issue itakuwa analysed kwa merit yake. Naweza kuwa sikufurahia ukaribisho wa Lowassa CDM lakini hilo halifanyi kutupa mawazo positive (kwa mtazamo wangu bila shaka ) ya Mbowe.
 
Siasa za matukio ndio zinafikia ukingoni. Magufuli atawafanya hawa wapinzani wakose dili.
 
Hizo fedha za MCC ndizo zilizofanya ndugu zenu waishio vijijini kupata umeme. Kama Magufuli ana dhamila ya dhati kusaidia Taifa hili hana budi kutatua mgogoro wa zanzibar haraka sana. Nashangaa kuona watu wanamshabikia Magufuli kama timu ya mpira. Sasa naanza kuamini tafiti zilizoonesha kuwa "BLACK PEOPLE ARE NOT AS SMART AS WHITE"

Zanzibar ni nchi , Magufuri aende kusuruhisha nchi za watu ? MCC wakae na pesa Zao , Magufuri atatafuta zake baada ya kuchimbua majipu yote
 
Mbowe anamtaka Rais yeye kama Nani!?
Anamtaja Rais yupi zaidi ya Lowassa
DJ fanya mengine hunajipya
 
mbowe anafurahia sisi tukiwa omba omba milele lakini yeye ana mapesa huko nje ya nchi. badala ya kushauri namna ya kuongeza pato la taifa ili kufidia hili gap anazidi kuunga mkono mabeberu wenzake.

Huwa najisemea Mbowe analindwa Na haya Manyumbu take
huyu MTU ni hovyo
 
Ilikuwa tupate pesa kiasi gani kutoka mcc??
Sasa ni dhahiri tumezikosa, je hakuna namna nyingine tunaweza kufanya tukapata pesa kama hiyo??
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KAULI YA MWENYEKITI FREEMAN MBOWE

KUHUSU

UAMUZI WA BODI YA MCC KUZUIA MSAADA WAKE KWA SERIKALI YA TANZANIA

Muda mfupi baada ya Bodi ya MCC kutoa taarifa inayoonesha Tanzania haitapata msaada kutoka shirika hilo kama ilivyotarajiwa kwa ajili ya mwaka 2016, Mwenyekiti wa Chama (T), Freema Mbowe ametoa kauli nzito juu ya suala hilo akisema kuwa kuchelewa kupatikana kwa fedha za MCC si tu kunachafua jina la nchi na hadhi yake katika medani za kimataifa, bali kutaathiri kwa kiasi kikubwa miradi yote iliyo chini ya ufadhili wa MCC.

MCC imeahirisha msada huo wa USD Mil. 472.8 ambazo ni takriban trilioni moja kwa fedha za Tanzania zilizolengwa kusaidia sekta ya nishati ya umeme hususan ule wa vijijini, katika kuunganisha wateja wapya, mabadiliko ya kimuundo ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) ili lifanye kazi na kutoa huduma kwa ufanisi katika sehemu za uzalishaji, usafirishaji na usambazaji.

Fedha hizo pia zilikusudiwa kusaidia kuanza kwa mpango mkubwa wa kuboresha sekta ya umeme nchini.2014-2024.

Mbowe amemtaka Rais John Magufuli kuchukua hatua za haraka za kiuongozi kumaliza mtanziko wa kisiasa Zanzibar kwa mshindi wa nafasi ya urais kutangazwa kutokana na uchaguzi uliofanyika mwezi Oktoba, mwaka huu.

Aidha amesema kuwa Sheria ya makosa ya mtandao (Cyber Crime Act 2015) ambayo ni mojawapo ya sababu zilizotumiwa na MCC kuahirisha msaada huo kwa Tanzania hadi itakapokuwa imefanyiwa kazi, ni sheria mbaya sana inayokinzana na kukua kwa technologia ya habari na mawasiliano na kuzuia upashanaji wa habari miongoni mwa jamii ambayo ililenga kuweka makosa ya kijinai ili kudhibiti wapinzani wa CCM katika uchaguzi mkuu na kukipatia mazingira ya ushindi chama hicho.

"Sasa imethibitika kuwa Bodi ya MCC iliyokaa tarehe 16 Dec 2015 imeahirisha rasmi kuidhinisha msaada wa Millenium Challenge uliokuwa umekusudiwa kwa Tanzania kwa mwaka wa fedha 2016. Sababu kuu mbili zilizosababisha uamuzi huo ni:

1. Mkwamo wa Uchaguzi wa Rais na Wawakilishi Zanzibar na
2.Matumizi mabaya ya she ria ya makosa ya mtandao hususan kuhusiana na uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa 2015."

"Ubabe wa baadhi ya viongozi wa CCM ni janga la Taifa. Kuchelewa kupatikana kwa fedha za MCC si tu kunachafua jina la nchi na hadhi yake katika medani za kimataifa, bali kutaathiri kwa kiasi kikubwa miradi yote iliyo chini ya ufadhili wa MCC," amesema Mwenyekiti Mbowe na kuongeza;

"Sheria ya makosa ya mtandao (Cyber Crime Act 2015) ni sheria mbaya sana inayokinzana na kukua kwa technologia ya habari na mawasiliano. Aidha, kwa makusudi kabisa inafifisha uhuru wa kupashana habari na ni dhahiri ilitungwa kwa nia mbaya ya kuthibiti kijinai uchaguzi mkuu."

"Tuliipinga sheria hii Bungeni na ikapitishwa usiku wa manane kwa ubabe wa wabunge wa CCM na hata tulipomtaka rais Kikwete asiisaini aliisaini kibabe akijua anaandaa mazingira gani ya "kihalifu", " amesema Mwenyekiti Mbowe.

Ameongeza kusema kuwa sheria hiyo ilitumika kuvamia vituo vya CHADEMA vilivyokuwa vikitumika kukusanya matokeo ya kura za rais na wabunge na hadi leo vijana zaidi ya 161, wakiwemo wanafunzi, wana kesi za "kubumba" mahakamani.

Mwenyekiti Mbowe amesema kuwa Sheria hiyo hiyo ilitumika kuficha dhana ovu iliyotumika kuhalalisha kuvamia Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kilichokuwa kikiratibu watazamaji wa uchaguzi wa ndani kwa kibali cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

"Vile vile Sheria hii imetumika kuwakamata na kuwaweka ndani na hata kuwanyima dhamana vijana wetu ambao walituunga mkono katika uchaguzi mkuu."

"Namtaka rais Magufuli achukue hatua za kiuongozi na kiutawala kwa kufanya yafuatayo:"

"Kwanza aumalize mgogoro wa kisiasa Zanzibar kwa kuhakikisha kuwa mshindi halali anatangazwa.

"Pili achukue hatua ya kuifanyia marekebisho makubwa Sheria ya makosa ya mtandao katika bunge lijalo. Aidha wale wote waliobambikiwa kesi amuamuru DPP kuzifuta kesi hizo mara moja," amesema.

Mwenyekiti Mbowe amesisitiza kuwa Rais Magufuli hana budi kuchukua hatua hizo za haraka ili kulinusuru taifa na hasara ya kupoteza mabilioni hayo ya MCC na zaidi kuepusha kuporomoka zaidi kwa biashara ya utalii nchini Zanzibar.

Amesema katika taifa ambalo sekta ya umeme inakabiliwa na matatizo makubwa katika uzalishaji, usambazaji na usafirishaji huku wananchi wa kipato cha chini wakibebeshwa mzigo mkubwa wa kumudu nishati hiyo na wengine wakilazimika kutumia nishati mbadala kama mkaa unaotokana na miti hivyo kusababisha uharibifu wa mazingira, serikali inayojua wajibu wake yenye viongozi wanaothamini uwajibikaji, haikupaswa kushindwa kuchukua hatua stahiki kutimiza vigezo vya msaada huo ambao umeshaisaidia Tanzania katika miradi mingine kadhaa.

Imetolewa leo Ijumaa, Desemba 18, 2015 na;

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
 
Mi nadhani Mbowe angepaswa kuliongelea suala la ZnZ bila kuhusisha fedha za MCC Kwani km taifa tunapaswa kujenga uchumi wetu nasi kusubiri wadhamin watupatie hii ni aibu kwa upinzani kuzungumzia mkopo km faida kwa taifa bila kuja na mikakati ya nn kifanyike ili taifa lisonge mbele bila kutegemea misaada
 
Ukiona mtu anashabikia wazungu muogope kama ukoma. Misaada unaiua uchumi.

Naona unamtukana mkwere hapo, maana yeye ndie alisema huko kwa wazungu mahela ni mengi sana, ni suala la kujenga hoja tu, unapata.
 
Mwambieni Mbowe hatutaki misaada, na yale mapesa ameficha nje ayarudishe haraka.

sawa misada hatutaki lkn vp kuhusu sisi ndugu zenu wa Zanzibar hamtaki tutoke hapa tulipokwama ?
 
Siasa za matukio ndio zinafikia ukingoni. Magufuli atawafanya hawa wapinzani wakose dili.

Wewe ndio huna dili anayepelekwa kama bendera fuata upepo bila kutafakari kinachoendelea! Ndugu yangu ndio kazi ya serikali ya Mhe Magufuli imeanza na kisiasa miaka mitano ni muda mrefu sana anything can happen!
 
Kwa mawazo yangu nafikiri MCC inatakiwa itatue mgogoro wa IT wa ule mfumo wa komputa uliokuwa ukiingilia mtandao wa NEC na ZEC.Mgogoro wa uchaguzi unahusika hasa na ule mfumo wa kijangili uliokuwa ukiingilia matokeo ya NEC na ZEC na kuzalisha matokeo ya kugushi. Bila shaka MCC wanalijua hilo vizuri.

NEC waliwahi mapema na kuwadaka wahusika na wako mahakamani. ZEC wakachelewa ndio maana imependekezwa Uchaguzi urudiwe ili matokeo yakusanywe na Mtandao usioingiliwa. MCC kuingilia na kusema hawatoi hela kuna tatizo kwenye chaguzi mmmmmmmm!!!! Mhusika hasa wa hilo tatizo ni nani? Sio MCC wenyewe kweli? Sio wao waliofadhili?

Isije kuwa wanatengeneza tatizo halafu wanataka mtu mwingine atatue. Si watatue wenyewe?

Toa ushahidi wa kituo kimoja tu Zanzibar ambacho IT iliingilia mchakato wa kura Zanzibar, weka hapa. Au unafurahisha barza? Ukishindwa basi angalau lete kifungu cha katiba kilichomfanya jecha kufuta uchaguzi. Usiwe unaongea tu kama huna kaa kimya
 
Back
Top Bottom