Hayo ya' Chopa', ni ya kawaida sana!
Yasiyo kuwa ya kawaida ni:
"...kugombea urais", ili iweje? Hawezi kushinda nafasi hiyo; labda iwe ni yale yale ya siasa za Kenya, ya "nusu mkate"; siasa ambazo tayari zilikuwa zinaandaliwa CHADEMA, kabla ya kufurumushwa.
"... pamoja na WABUNGE 10 wa KUNDI LA COVID-19...". Hili pia siyo tukio la kushangaza; lilitegemewa kuwa hivyo.
ILA hili "...akiwemo Halima mdee!" Nitaomba niwiwe radhi na wasomaji, kwa maana hili nimelirudia rudia mara nyingi sana humu JF. Sijui kwa nini huyu Halima Mdee hadi leo hii, akili yangu imekataa kabisa kuwa sehemu ya watu wannaoweza kuyumbishwa kwa kiasi hiki. Siamini! Pesa?, Pesa? Bado siamini