Tetesi: Mbowe kuondoka na covid-19 kumi kwenda nao CHAUMMA

Ni haki yake,ila ndiyo anazikoleza kwa wino mweusi zile tuhuma za agano la nusu mkate na pia kuwa hela za Abdul zilizopenyezwa Chadema sasa zinaelekezwa CHAUMMA kuifanya kazi ile ile ya kuidhoofisha Chadema.
 
Heshima yake itashuka kama Mrema ni bora angebaki alivyo. Kila mtu anajua Chauma ni fake !!
Mkuu, kati ya heshima na mafekeche, wee unachagua nini?

Maana ghafla tu paap! Mzee Hashim Rungwe anakipaisha chama chake angani jimbo kwa jimbo kwa helikopta.
 
Ni haki yake,ila ndiyo anazikoleza kwa wino mweusi zile tuhuma za agano la nusu mkate na pia kuwa hela za Abdul zilizopenyezwa Chadema sasa zinaelekezwa CHAUMMA kuifanya kazi ile ile ya kuidhoofisha Chadema.
Kuhusu utajiri wa ghafla wa CHAUMMA, tumeambiwa ni wale wahisani wa zamani wa Sidiemu wamehamia huko pamoja na kundi bobevu na lenye mikakati la G55.
 
Hayo ya' Chopa', ni ya kawaida sana!
Yasiyo kuwa ya kawaida ni:

"...kugombea urais", ili iweje? Hawezi kushinda nafasi hiyo; labda iwe ni yale yale ya siasa za Kenya, ya "nusu mkate"; siasa ambazo tayari zilikuwa zinaandaliwa CHADEMA, kabla ya kufurumushwa.
"... pamoja na WABUNGE 10 wa KUNDI LA COVID-19...". Hili pia siyo tukio la kushangaza; lilitegemewa kuwa hivyo.

ILA hili "...akiwemo Halima mdee!" Nitaomba niwiwe radhi na wasomaji, kwa maana hili nimelirudia rudia mara nyingi sana humu JF. Sijui kwa nini huyu Halima Mdee hadi leo hii, akili yangu imekataa kabisa kuwa sehemu ya watu wannaoweza kuyumbishwa kwa kiasi hiki. Siamini! Pesa?, Pesa? Bado siamini
 
G55 ni kikundi cha majungu wizi uzinzi umbea na mambo yote ya hovyo huko chauma ubwabwa patanuka majungu hadi wampindue Babu ubwabwa Rungwe wajimilikishe chama
 
Rungwe ataporwa chama mda si mrefu kwani cha umbea kigaila na mnafiki salum mwalimu ni kumpindua Rungwe
 
Halima Mdee na Esther Bulaya ndiyo nawaona wana msimamo japo waliyumbishwa sana kwenye sakata la covid 19,ngoja tuwapime katika hili kama wakimfuata Mbowe basi hatutakuwa na shaka tena na ushiriki wa Mbowe kuwapeleka Bungeni kimtindo akishirikiana na ma lieutenant wake Kigaila na Salum Mwalimu.
 
HAKIKA.
 
Kwa hiyo Mbowe na chauma yao ni wapinzani wa ccm na wa upinzani!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…