Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Sidhani kama kuna mtu ambaye anaweza kusimama na kwa dhamira akazikataa jitihada za Mbowe katika kuijenga CHADEMA na katika kupigania haki na demokrasia nchini Tanzania.
Ni katika jitihada hizo, Mbowe aliwekwa mahabusu za polisi mara kadhaa, alifilisiwa kwa nguvu, alitumia muda wake, rasilimali zake, akili yake na kila jitihada kuhakikisha nchi inapiga hatua katika uhuru, haki na demokrasia, na zaidi kuifanya CHADEMA kuongoza katika jitihada hizi. Kama binadamu, Mbowe katika kuyatenda hayo, yawezekana alifanya makosa ya hapa na pale. Hiyo ni kawaida.
Lakini pamoja naye, wapo Watanzania wengi walioungana naye, nao walipambana na kupoteza mengi, wengine mpaka uhai wao (Mungu wa huruma awarehemu). Miongoni mwa walioumizwa sana katika mapambano haya ni Tundu Lisu, na wengi tuwajuao.
Mbowe na Lisu na hawa wengine wote walioumizwa kwa namna mbalimbali kwaajili ya kuipigania Tanzania na CHADEMA, walistahili kuheshimiwa na kukumbukwa daima katika historia yetu.
Kuna mahali Mbowe na Lisu, wanataka kukosea. Na makosa wanayoyafanya yanaweza kuwafanya wapoteze heshima kubwa ambayo wanastahili. Kwa yanayoendelea sasa, tumefikia hata watu wasio na mchango wowote wa maana katika nchi hii, watu kama Ntobi na Steve, wanawadhihaki na kuwakejeli miamba hii mikubwa ya siasa za upinzani.
Kabla muda haujaenda, Mbowe na Lisu, wafedhehesheni wapuuzi hawa. Haraka mnaweza kufanya yafuatayo:
1. Kwa uwazi kabisa, onesheni kuwa hakuna uhasama baina yenu maana mnachokioigania ni kimoja ingawa mnaweza kutofautiana katika mawazo na mbinu namna ya kutekeleza.
2. Mbowe muda uliokitumikia Chama ni mrefu sana, tangaza kujiondoa na kuwaunga mkono wote waliogombea kuchukua nafasi yako, na kutamka wazi kuwa utampa ushirikiano wa kutosha yeyote atakayechaguliwa.
3. Lisu jitahidi kuzuia kauli zinazoweza kutafsiriwa kama ni personal attack dhidi ya mwenyekiti wako, japo una haki ya kutofautiana naye kimbinu endapo utachaguliwa. Ni vema na ni sahihi kabisa kuweka bayana juu ya mambo utakayoyafanya tofauti na mtangulizi wako, endapo utachaguliwa.
4. Lisu endelea kuzipuuza kauli za kejeli dhidi yako kutoka kwa watu ambao hawana mchango wowote wa maana katika harakati hizi za kuitafuta haki na demokrasia.
5. Katibu Mkuu Mnyika, wakati wagombea wako wa nafasi ya umwenyekiti wakijizuia kupambana na watu binafsi, jukumu la kutunza nidhamu na maadili lipo mikononi mwako. Toa maelekezo kwa mamlaka zinazohusika kuchukua hatua dhidi ya wote wanaoonekana kutoa kauli zinazokiuka maadili ya chama, lakini kwa kufuata taratibu na katiba ya chama, bila ya kumwonea au kumpendelea mtu.
Mbowe usiipe nafasi CCM kukutumia wewe katika kuleta mfarakano ndani ya chama. Mbinu inayotumika sasa ya kuonesha kuwa wewe ni kipenzi cha CCM na Serikali ya CCM, ni silaha mbaya sana dhidi yako.