Pre GE2025 Mbowe: Lissu kusema hajui nilichozungumza na Rais ni Umbea

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Wakiwa kwenye vikao wanatabasamu na kucheza pamoja, wakitoka hapo ni spana kwa kwenda mbele! Ni huzuni! :PepeHands: :KEKLaugh:

1737099571504.png

"Taarifa kwamba sikusema nilichozungumza na Rais ni umbea, na unapoona kiongozi mwandamizi kama kweli amesema..mimi sijasikikia ila kama kweli amesema inanishangaza kwasababu nimezungumza na Rais, tumezungumza na vyombo vya habari, nimeleta taarifa kamati kuu, kamati kuu imepeleka taarifa baraza kuu, baraza kuu lina wajumbe 500 kutoka mikoa na wilaya zote, wamekubaliana tuingie kwenye maridhiano, akisema hajui kilichozungumzwa wala hakuwa na taarifa ni umbea.

"Hiyo ni moja, mbili mimi nikiwa gerezani Rais alikwenda Brussels (Nchini Ubelgji) Makao Makuu ya Umoja wa Ulaya na akiwa huko alikutana na Makamu wangu, Mhe. Lissu wakazungumza na Lissu akamtaka Rais azungumze na CHADEMA, amuondoe Mwenyekiti gerezani na kadhalika, sasa yeye kuzungumza na Rais ilikuwa haki lakini Mwenyekiti wake kuzungumza na Rais imekuwa ni nongwa, hii siyo vizuri"

Pia soma: Uchaguzi 2025 - Lissu apinga tuzo aliyopewa Samia na kusema kuwa huo haukuwa uamuzi wa Chama bali maamuzi binafsi ya Mwenyekiti, ataka ahojiwe

"Mimi ni Mwenyekiti wa chama yaani nikitaka kuzungumza na Rais wa taifa ni lazima niite mkutano mkuu, wajumbe wote kutoka kila jimbo nizungumze kuomba kibali cha Rais? Hapana, na katiba ya chama imenipa mimi mamlaka ya kuwa kiunganishi kati ya chama na serikali, ni majukumu ya Mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya chama, na mimi ndiye msemaji mkuu wa chama, hatuwezi kuwa na wasemaji wa chama kumi, lazima kiongozi mkuu ashike bendera na ndiye anakuwa msemaji mkuu wa chama"- Mbowe.

Mbowe ameyasema hayo akizungumza leo Ijumaa Januari 17, 2025 katika kipindi cha Morning Trumpet kinachorushwa na chaneli ya runinga ya UTV.
 
Mbowe kawa Khadija Koppa sasa malkia wa mipasho. Aibu mimi naona,kutoka Mwamba hadi kuwa Malkia wa mipasho.
zimebaki siku nne, kila siku anafanya press, mara kwake, mara studio, mara wapi kule. Ndani ya siku nne hizi anaweza kufanya hata press tatu kwa siku mmoja kumponda mpinzani wake huyo. Anarudiarudia yaleyale, apumzike tu
 
Kama Chair ameanza kutoa maneno kama ya kwenye khanga, basi hapo kilicho baki ni kutoana roho tu.
Kila kitabu na zama zake...☹️
 
Wajumbe sio watu! Tusubiri tarehe 21
Sanduku la Kura litaamua!

Ikitokea Lissu akashindwa kwa Hali kabisa. Nitaamini wajumbe ni wanafki
Sasa wajumbe unafki wao ni upi? Unadhani hawa wapiga domo hapa kuna mpiga kura? Wenye shughuri yao wapo kimya.

Hivi kwa akili yako unaona Mbowe hana akili aingie kwenye uchaguzi bila research?

Uchaguzi ulianza mikoani na majimboni, tarehe 21 ni hitimisho tu huwezi kubadili mitandao ya watu waliotengeneza mpango kazi wao kitambo.
 
Lissu kumbukumbu zimekuwa ni tatizo kwa siku za hivi karibuni.
 
Wakuu,

Wakiwa kwenye vikao wanatabasamu na kucheza pamoja, wakitoka hapo ni spana kwa kwenda mbele! Ni huzuni! :PepeHands: :KEKLaugh:

"Taarifa kwamba sikusema nilichozungumza na Rais ni umbea, na unapoona kiongozi mwandamizi kama kweli amesema..mimi sijasikikia ila kama kweli amesema inanishangaza kwasababu nimezungumza na Rais, tumezungumza na vyombo vya habari, nimeleta taarifa kamati kuu, kamati kuu imepeleka taarifa baraza kuu, baraza kuu lina wajumbe 500 kutoka mikoa na wilaya zote, wamekubaliana tuingie kwenye maridhiano, akisema hajui kilichozungumzwa wala hakuwa na taarifa ni umbea.

"Hiyo ni moja, mbili mimi nikiwa gerezani Rais alikwenda Brussels (Nchini Ubelgji) Makao Makuu ya Umoja wa Ulaya na akiwa huko alikutana na Makamu wangu, Mhe. Lissu wakazungumza na Lissu akamtaka Rais azungumze na CHADEMA, amuondoe Mwenyekiti gerezani na kadhalika, sasa yeye kuzungumza na Rais ilikuwa haki lakini Mwenyekiti wake kuzungumza na Rais imekuwa ni nongwa, hii siyo vizuri"

Pia soma: Uchaguzi 2025 - Lissu apinga tuzo aliyopewa Samia na kusema kuwa huo haukuwa uamuzi wa Chama bali maamuzi binafsi ya Mwenyekiti, ataka ahojiwe

"Mimi ni Mwenyekiti wa chama yaani nikitaka kuzungumza na Rais wa taifa ni lazima niite mkutano mkuu, wajumbe wote kutoka kila jimbo nizungumze kuomba kibali cha Rais? Hapana, na katiba ya chama imenipa mimi mamlaka ya kuwa kiunganishi kati ya chama na serikali, ni majukumu ya Mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya chama, na mimi ndiye msemaji mkuu wa chama, hatuwezi kuwa na wasemaji wa chama kumi, lazima kiongozi mkuu ashike bendera na ndiye anakuwa msemaji mkuu wa chama"- Mbowe.

Mbowe ameyasema hayo akizungumza leo Ijumaa Januari 17, 2025 katika kipindi cha Morning Trumpet kinachorushwa na chaneli ya runinga ya UTV.
Mchagga kachefukwa
 
Mbowe na Lissu wanapigana sana spana hadi kuitana wambea. Ni huzini jamani
 
Back
Top Bottom