Mbowe, Lissu nidhamu inaporejea wafundeni wafuasi heshima

Mbowe, Lissu nidhamu inaporejea wafundeni wafuasi heshima

Muhimu tusichanganye kati ya ukosefu wa nidhamu na uhuru wa kutoa maoni, vinginevyo tunaweza kufurahia unatibu tatizo moja, kumbe tunaenda kutengeneza tatizo lingine la chama kuwa makondoo na chawa tupu, wawe watu wa kuwasifia viongozi tu hata pale watapoona mambo hayaendi vizuri.
 
Hakuna mlengwa ndugu mkaanga mbuyu. Mada iko wazi. Hoja hupingwa kwa hoja.

Habari ndiyo hiyo.
Hakuna hoja inayokuja toka hewani bila tukio. Endelea na maumivu ya kichwa, nyoka mumewafuga wenyewe
 
Muhimu tusichanganye kati ya ukosefu wa nidhamu na uhuru wa kutoa maoni, vinginevyo tunaweza kufurahia unatibu tatizo moja, kumbe tunaenda kutengeneza tatizo lingine la chama kuwa makondoo na chawa tupu, wawe watu wa kuwasifia viongozi tu hata pale watapoona mambo hayaendi vizuri.

1. Nidhamu na uhuru wa kutoa maoni ni muhimu sana na mawili hayo hayapaswi kuchanganywa.

2. Hata hivyo kwa niaba ya chama wasemaji ni viongozi na wenye dhamana hiyo.

3. Wakati kauli za viongozi ni kauli za chama si hivyo kwa wasiokuwa na dhamana ya kukisemea chama.

4. Kauli za wajumbe, wanachama bila ridhaa ya chama hizo ni maoni yaani ni kauli binafsi kama za yeyote katika chama.

5. Tofauti za wanachama na viongozi ziko bayana hapo kwenye kukisemea chama kuepuka mikanganyiko.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Hakuna hoja inayokuja toka hewani bila tukio. Endelea na maumivu ya kichwa, nyoka mumewafuga wenyewe

Kama kwenu kusema jambo ni mpaka mpigwe tukio kama hivi:

F-Ay3s_WUAAKYKi.jpeg


Kwetu hujipanga uzuri kwa ajili ya kesho na kabla ya hatari.

Habari ndiyo hiyo.
 
Mara nyingi tuliwaonya sana kuhusu utovu wa nidhamu wa Mdude_Nyagali dhidi ya matusi na dharau kwa Rais Samia. Tuliwaambia viongozi wa CHADEMA wakapuuza na kuona kuwa Mdude ana haki ya kusema anayo yasema.

Sasa Mdude anawageukia nyinyi wenyewe CHADEMA na kuanza kuwatafuna

Mdude kamtafuna CHADEMA wapi ndugu? Huyu si mdude:

F0v5tYZXgAEPFoz.jpg.jpg


Cc: WALOLA VUNZYA
 
Hongereni kwa kurejea kwa nidhamu chamani.

"Mbowe, Lissu chukueni hatua kurejesha nidhamu kwenye chama"

Kwamba hii ni kwa maelekezo yenu au ni kwa heshima au kuhofiwa kwa majina yenu? Hilo wala si la msingi tena:

"The end justifies the means."

Kuhusiana na "heshima," huu ni ushauri mwingine wa bure kwenu ukilenga kwenye kuwafunda wafuasi kuzingatia:

"Heshima ni kitu cha bure na kuwa hutokana na umri, hekima, mchango wa mtu katika jamii au kutokea katika mafanikio yake, yakiwamo u nguli."

Ni muhimu wafuasi wakaelekezwa na wakafahamu:

1. Tofauti zilizipo baina watu au baina ya viongozi na wanachama katika chama.

2. Mbowe au Lissu hawawezi kuwa sawa na mwanachama yeyote.

3. Kauli ya Mbowe au Lissu haiwezi kuwa sawa na kauli ya mwanachama au mfuasi yeyote (na eti kwa sababu tu ana mdomo).

4. Kauli ya Mbowe au Lissu ni kauli za chama, lakini si za kila mwanachama, mjumbe au mfuasi mwingine (na hasa inapokuwa bila ridhaa ya chama).

5. Kauli ya nguli mheshimika katika jamii haiwezi kubezwa kireja reja kwa niaba ya chama na hasa bila ridhaa ya chama.

6. Ni muhimu ikawa wazi kuwa wajumbe, wanachama au wafuasi wenye sharubu jamii ya kambale hawawezi kuvumiliwa.

Heshima ni nguzo kuu kuelekea kwenye nidhamu ya kudumu katika chama ambayo umuhimu wake hauwezi kupuuzwa.
🤨
 
Back
Top Bottom