Mbowe: Mama! Mama! Mama! Kwenye hili HAPANA

Ndugu,

Kwani movement hizi zinazotaka kuanzishwa ni kwa ajili ya nini haswa?? Kwa mfano hii movement wanayoifanya chadema na watu wao wa Twitter ni kwa ajili ya nini???
Tujadiliane

..mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ni haki ambayo imebainishwa ktk katiba na sheria zetu.

..sasa Mama Samia ametoa kauli kwamba anasimamisha utekelezaji wa haki ambayo wananchi wamepewa na katiba yao.

..mimi kwa mtizamo wangu Mama ameteleza kufanya hivyo kwasababu yeye amekula kiapo cha kuilinda Katiba.

..halafu Mama pia amesema wabunge ndio amewapa ruhusa kufanya mikutano ya hadhara. Sasa tukiangalia composition ya bunge letu watakaopata nafasi kufanya hiyo mikutano 99% ni CCM chama chake Mama.

..kwa hiyo hapo naona Mama ameteleza tena kwani huo utakuwa ni upendeleo. Katika kiapo chake Mama alitamka hatapendelea.

..Tukiingia kwenye sababu alizosema zimemlazimisha kufanya uamuzi huo nazo naziona hazina ushawishi na sitapenda kuzichambua ikaonekana kama namkomoa.

..Mama alikuwa anakwenda vizuri, tena hatua kwa hatua, lakini sijui ni kitu gani kimemtokea mpaka kufanya maamuzi haya.

..Labda ni swali ambalo hakuwa amejiandaa kulijibu. Labda alikuwa amejiandaa na majibu ya kero za wanahabari kwasababu ulikuwa mkutano maalum na wanahabari.
 
Mdude Nyagali ametoka RUMANDE kwa huruma ya mh. Rais Samia Suluhu Hassan..

Masheikh wa UAMSHO wanakula biriani mtaani kwa sababu ya huruma ya mh. Rais Samia Suluhu Hassan...
Acha upotoshaji Mdude na Mbowe et al., kilichowafanya wawe huru ni Mahakama kufanya kazi yake sio huruma ya Rais
 
She has declared: "Mimi na Magufuli ni kitu moja". So, there is no surprise at all. "ninapayuka tena: KATIBA MPYA!!!?"
Niki jenga imani kubwa sana kwa Mh Mama Samia lakini kwa kauli yake ya jana, ana nilazimisha kumuona kweli yeye na Magu ni kitu kimoja. Sikuwahi kufikiri ataweza kutoa maamuzi kinyume na katiba.

Hapo si sawa. Ana takiwa afuate katiba.
 
Wacha story za uchumi na kifikra,swali ni je mama Yuko tayari kuleta Katiba mpya ambako jaji mkuu anaweza kusema uchaguzi huu ni batili na urudiwe?Jaji Maraga wa Kenya unamjua...
Baada ya uchaguzi kurudiwa, mpinzani alishinda?
 

Hao chadema unaowaongelea mnakutana nao wapi?


Ni humu mitandaoni?
 
Unataka kuwa mhuni???

Basi Nenda Chadema..!

Kiila ukifanya upumbavu, utaambiwa wewe ni Mandela wa pili Africa,

Ukivuta bange ukabahatika kumtukana Raisi, basi hapo wewe ni shujaa kama Mandela

Mna kutakana wapi na chadema hao?


Ilikuwa vizuri kukagua facts zenu kwanza kujiridhisha.
 
..mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ni haki ambayo imebainishwa ktk katiba na sheria zetu.

..sasa Mama Samia ametoa kauli kwamba anasimamisha utekelezaji wa haki ambayo wananchi wamepewa na katiba yao....

Kwamba?

"..Mama alikuwa anakwenda vizuri, tena hatua kwa hatua, lakini sijui ni kitu gani kimemtokea mpaka kufanya maamuzi haya."

Huu ni ukweli kumhusu Mama na JPM.

1. Day 1, Samia = JPM. -- Samia
2. (a) Mapema, nipeni muda niinyoroshe nchi -- JPM.
(b) Jana, nipeni muda nisimamishe uchumi -- Samia.

Hata kabla ya jana sifa zote kajizolea mama (akizungukwa na wahafidhina) kutokana na haya:



Nini kimebadilika hapo kuleta mtafaruku wowote?

Kitu gani labda wewe umekiona mkuu?
 
Ooh Poor Mbowe, alipokuwa Mbunge wa Hai, hakufanya mikutano Hai, akakimbilia Kawe na tundulissu, au Usukumani kwa Mawazo. Haki ya kufanya mikutano jimboni kwako aliizeleu kwa vile Jimboni kwake eti akij8danganya kuwa wametosheka. Ukaja uchaguzi kaangushwa chini puu na katoto kadogo. Sasa hata Ubunge hana sasa atakuwa mgeni wa nani?
 
Mbowe kaanza na hizo 'yeyeyeeeeee yeyeyeeeeeee haya ingieniii' zake tena. Mama anataka nchi iwe 'calm and cool' ili kazi iendelee kukuza uchumi wa nchi na wa mtu mmoja mmoja na kuwezesha watu wengi zaidi wapate ajira. Hizo kelele za akina Mbowe za lengo la kuwaingiza ikulu hazina tija yo yote na ni fujo tu za kuvuruga nchi.
 
Leo machadema wanamkana mama Samia [emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23] kabla Jogoo hajawika
 
Unataka katiba mpya?.

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Kwani unagombea nafasi ipi mkuu

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Mbowe kwanini haachii uwenyekiti chadema? Aanze yeye
Nimetaka kipengele ambacho Mbowe alibadilisha ili atawele milele lkn naona jamaa amekula Kona.

Mbowe atakua anataka kutawala miaka sawa Kama ya Nyereee ndio aruhusu 'Vyama vingi',.hahah.
 
Kwa hiyo ni kweli kwamba wote hao walifikiwa na hayo kwa utashi wa rais dikteta aliyefariki na kama ni kuachiliwa pia ni kwa majaliwa ya rais wa sasa.!

Hivyo ni kweli kwamba Tanzania hamna sheria ila ni matakwa ya rais ndiyo yanatekelezwa. Rais ndiyo anaweka watu ndani na ikimpendezea anawaachilia. Nchi imekuwa ya hovyo na takataka kabisa.
 
Uwe na heshima na adabu kabla hujaliandika jina la rais

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…