Mbowe, maridhiano yako bila kuwasamehe wale wabunge 19 yatakuwa hayana maana

Mbowe, maridhiano yako bila kuwasamehe wale wabunge 19 yatakuwa hayana maana

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
3,891
Reaction score
8,448
Freeman Mbowe huwa anahubiri mambo ya kusema kweli na maridhiano wakati yeye si mkweli na hatabiriki misimamo yake kwani anauwezo wa kubadili gia angani haraka sana ili mradi kuwe na pesa mbele yake.

Alifanya hivyo wakati anauza chama kwa Lowasa na amefanya hivyo tena wakati anaanza kupokea ruzuku ya chama aliyoikataa kwamba inatokana na uchaguzi haramu wa 2020.

Mbowe anasimama mbele ya Rais na kuwakataa wabunge 19 huku akijua bila hao wabunge hawezi kupokea hiyo ruzuku ya milioni 900 kwa mwezi.

Haya maridhiano ili yawe na maana lazima yawe ya kufaidisha watu wote na siyo kufaidisha Mbowe na genge lake tu.
 
Wewe unaweza kumsamehe mtu aliyekukosea na akakataa kukiri kosa na kukuomba msamaha? Msamaha kwa COVID-19 upo wazi.

Waombe msamaha na waachie nafasi za ubunge wa viti maalumu walizozipata kwa njia ya udanganyifu. Huwezi kuiba halafu usamehewe kabla hujarudisha ulichokiiba na kuomba msamaha!
 
Ama kweli kama taifa tumepotea. Ni aibu kwamba kuna watu hata hawajui ruzuku ya vyama vya siasa inatokana na nini.

Hoja yako ya COVID-19 kama ingesemwa na kiongozi wa CCM ingetosha kuwa uthibitisho kwamba hao wabunge wamewekwa na CCM. N8 hoja mfu, ya hovyo, isiyokuwa na mashiko, inayoashiria uvivu wa kufikiri.
 
Na bado, mwaka huu na yote inayokuja mtalia sana, wewe na wenzako mnaoshirikiana.

Kwani maridhiano ya Serikali na CHADEMA yanalenga mifumo au yanahusu watu?

Kwamba ili kuwe na maridhiano inabidi CHADEMA iishinikize serikali ianze kushitaki wale wote waliokuwepo kwenye serikali iliyopita?

Pia CCM iwarudishe CHADEMA wale wote waliounga jitihada kwa kuhamia CCM?

Serikali iishinikize CHADEMA iwasamehe siyo tu COVID19 bali imrudishe dr. Slaa na kumkabidhi ukatibu mkuu wake.

Hivi huwa mnayasoma haya mnayoyaandika au kujisikiliza mnayoyaongea?
 
Wewe unaweza kumsamehe mtu aliyekukosea na akakataa kukiri kosa na kukuomba msamaha? Msamaha kwa COVID-19 upo wazi, waombe msamaha na waachie nafasi za ubunge wa viti maalumu walizozipata kwa njia ya udanganyifu. Huwezi kuiba halafu usamehewe kabla hujarudisha ulichokiiba na kuomba msamaha!
Je hiyo taarifa ya chama (CHADEMA) kupokea ruzuku ni ya kweli ?
Kama ni kweli wanaipokea kwa vigezo gani.
 
It seems hujui mambo mengi ndugu. Ruzuku wanayopokea Chadema inatokana na wingi wa kura alizopata Lissu kwenye uchaguzi uliopita, nje ya wabunge.

Kwa msingi huo, hata vyama vilivyopata kura nyingi kama ACT na NCCR kwenye uchaguzi uliopita wanapata ruzuku hiyo hata kama hawana wabunge. ACT yenyewe ina wabunge toka visiwani. Jielimishe kidogo.
 
Je hiyo taarifa ya chama (CHADEMA) kupokea ruzuku ni ya kweli ?
Kama ni kweli wanaipokea kwa vigezo gani.
Taifa lina hasara sana. Kama mpaka leo hujui ruzuku inakokotolewaje then kua shida mahali
 
Wewe unaweza kumsamehe mtu aliyekukosea na akakataa kukiri kosa na kukuomba msamaha? Msamaha kwa COVID-19 upo wazi, waombe msamaha na waachie nafasi za ubunge wa viti maalumu walizozipata kwa njia ya udanganyifu. Huwezi kuiba halafu usamehewe kabla hujarudisha ulichokiiba na kuomba msamaha!
Lema madhambi yake aliyosamehewa na mama Tena juu ya gari wala sio mahakamani unayajua,na mbona iliwezekana na yupo tu mtaani anatukana watu tena anaotegemea wampigie kura uchaguzi ujao?
 
ruzuku ni haki yao kikatiba, kuikubali na kuikataa ilikuwa hiari yao
Hatujakataa uchaguzi haramu haujaisha mana tangu 2020 hatujafanya uchaguzi tena ila tunaye raisi anayemalizia huo uchaguzi haramu wanaousema CHADEMA. Je, kipi kimewafanya kupokea hela inayotokana na uchaguzi haramu?
 
Wewe unaweza kumsamehe mtu aliyekukosea na akakataa kukiri kosa na kukuomba msamaha? Msamaha kwa COVID-19 upo wazi, waombe msamaha na waachie nafasi za ubunge wa viti maalumu walizozipata kwa njia ya udanganyifu. Huwezi kuiba halafu usamehewe kabla hujarudisha ulichokiiba na kuomba msamaha!
Mbona amewasamehe ccm?
 
Pale ni maslahi,na wanasiasa wengi wa Tz penye maslahi lazima wapambane cos asilimia elf kumi ya wanasiasa Tz ni kupambania maisha yao na si wananchi....... wanawake wanazitaka zile nafasi 🤣
 
Wewe unaweza kumsamehe mtu aliyekukosea na akakataa kukiri kosa na kukuomba msamaha? Msamaha kwa COVID-19 upo wazi, waombe msamaha na waachie nafasi za ubunge wa viti maalumu walizozipata kwa njia ya udanganyifu. Huwezi kuiba halafu usamehewe kabla hujarudisha ulichokiiba na kuomba msamaha!
Kwa Chadema kukubali ruzuku zinazotokana na uchaguzi haramu kuna hata mwana ccm aliyekiri tu kuwa kweli ule uchaguzi ulikuwa haramu? Hao hao ccm ndio waliyoshirikiana na hao covid 19 na hadi sasa bado Samia anawakinga hao covid 19.
 
Ama kweli kama taifa tumepotea. Ni aibu kwamba kuna watu hata hawajui ruzuku ya vyama vya siasa inatokana na nini.

Hoja yako ya COVID-19 kama ingesemwa na kiongozi wa CCM ingetosha kuwa uthibitisho kwamba hao wabunge wamewekwa na CCM. N8 hoja mfu, ya hovyo, isiyokuwa na mashiko, inayoashiria uvivu wa kufikiri.
Imagine jamaa hajui hata ruzuku inalipwa kwa utaratibu upi halafu anakuja na thread ya propaganda. Halafu utakuta ni Graduate huyo ..... No wonder Waziri anataka kuwapeleka VETA ....!!
 
Back
Top Bottom