Mbowe, mkanye Lissu

Mbowe, mkanye Lissu

Mataga Jiwe harudi hata mfanyaje , lieni machozi ya damu , mbona mnahangaika Sana wakati Jiwe anaenda kuwa mtanzania wa kwanza kuwa malaika mkuu mbinguni , I wish I could be igp in jiwe's voice .
 
Ni nini alichoposti kilichokuvuruga kiasi hiki mkuu!

Hivi hadi sasa bado machungu hayajapungua tu na kukubali aliyofanya Mwenyezi Mungu?

Achana na Lissu, hatakusaidia lolote katika maumivu yako.
nimezungumzia mwenendo wake hakuna upuuzi wowote ulinishtua ni vile alinipotezeaga mda kumkampeni mtu mpuuzi
 
Ushauri mzuri!
Tamaduni zetu ni kuheshimu maiti na wafiwa.
Alipaswa kutoa pole na kukaa kimya.
Nilishangaa zaidi alipoendelea kung'ang'ana kwenye vyombo vya nje kuwa corona ndio imemuondoa Magu na kwamba alifariki trh 09.
Sikuona mantiki yake.
Ni kweli aliumizwa lakini inabidi asamehe ama akae kimya.
Bado hajatufahamu watz vizuri?
Tayari ameshaharibu reputation yake.
Siasa inahitaji akili kubwa sana hasa kwa Tanzania.
Yaani Roma mkatoliki kamzidi saikolojia Lissu?
What? Kuheshimu maiti ya mtu muuaji? Huo ni utamuduni wa kishenzi sana. Hebu vaa viatu vya Lissu wewe uone.
1. Unamiminiwa magazine nzima ya risasi ili ufe lakini Mungu mkubwa unapona japo kwa kujeruhiwa sana
2. Watu wanataka kukuombea wanakatazwa.
3. Unanyimwa fedha za matibabu ambazo ni haki yako
4. Unanyanganywa ubunge bila kufuata taratibu
5. Unagombea urais kura zako zinaporwa huku ukipewa kejeli
6. Unaviziwa kuuawa mara ya pili mpaka unakimbilia uhamishoni
Nasemaje, kwanza Lissu ana heshima sana. Ingekuwa mtu mwingine angefanya shehere kubwa tena airushe live!
Hebu tuache unafiki. Muuaji kafa mwacha Lissu apumue.
 
1. Unamiminiwa magazine nzima ya risasi ili ufe lakini Mungu mkubwa unapona japo kwa kujeruhiwa sana
Na kama hiyo haitoshi; mtu huyo huyo angalau angejitahidi kuonyesha kuwa yeye hahusiki na tendo hilo; akakupa pole, na akafanya yaliyo ndani ya uwezo wake kukupa stahiki yako ili upone vizuri,...; badala yake jamaa anakuongezea maumivu waziwazi hadi kukuvua ubunge?

Kuna roho ya ubinaadam gani hapo?
 
Sidhani kama JPM anausika na kupingwa Risasi lissu. Kama ni hivyo basi atuna askari au TISS wa kijinga hivyo. Au washafukuzwa kazi.

..ni nani aliyeagiza walinzi wa area D waondolewe siku aliyoshambuliwa Tundu Lissu?

..ni nani aliyeagiza uchunguzi wa shambulio dhidi ya Tundu Lissu usifanyike?

..ni nani aliyeagiza Tundu Lissu asipewe stahiki zake za matibabu kama mbunge?
 
..hata kama ni mropokaji, Jiwe hakutakiwa kumtumia magaidi wamshambulie kinyama namna ile.
Unalojibu siyo mada ya thread hii inayohusu Mbowe kumkanya Lissu aache uropokaji; ni speculations zako kuwa unadhani Jiwe alituma Magaidi wamwue Lissu.
 
..ni nani aliyeagiza walinzi wa area D waondolewe siku aliyoshambuliwa Tundu Lissu?

..ni nani aliyeagiza uchunguzi wa shambulio dhidi ya Tundu Lissu usifanyike?

..ni nani aliyeagiza Tundu Lissu asipewe stahiki zake za matibabu kama mbunge?
ni maswali yenye hisa tupu mpaka pale tutakapoletewa ushahidi. Kuna sababu nyingi sana kuwa maswali haya hayawezi kuwa na uzito wowote wa kuweza kukubalika kwenye mahakama yoyote independent.
 
Unalojibu siyo mada ya thread hii inayohusu Mbowe kumkanya Lissu aache uropokaji; ni speculations zako kuwa unadhani Jiwe alituma Magaidi wamwue Lissu.

..mama yake Abdullah Kassim Hanga alishangilia kifo cha Abeid Karume.

..sijui kwanini mnashangaa kusikia kwamba walioumizwa na utawala wa Jiwe hawasikitikii kifo chake.
 
JF iko miaka mingi na mambo ya hovyo huwa yanalaaniwa. Siyo Lissu siyo, Magufuli (RIP), siyo Kikwete, siyo Mbowe. JF haiko hapa kwa ajili ya wanasiasa tu! Ila hatutaki nchi kugeuzwa brothel na mtu asiyejitambua kama Lissu. Yaani ijulikabne eti huyo ndo mtu wa maana upinzani! Foooool!
Hataki kubadilika sasa, wewe utafanya nini?

Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app
 
..Mbowe anajua mateso aliyopitia Tundu Lissu.

..yeye ndiye aliyehangaika naye baada ya serikali na bunge kumsusia mgonjwa tena akiwa mahututi.

..wanaosema Mbowe amkanye Tundu Lissu ndio waliokuwa wakimuombea afe, na baadae wakawa wakimcheka kuwa ni mlemavu.
 
Ninachokiona hapa Mataga wengi wanajaribu kwa kila namna kuwatia moyo Watendaji wa Serikali ili waweze kumuenzi Jiwe kwa yale mabaya na ukatili dhidi ya Wapinzani. Hawatafanikiwa pia kwa hilo.
 
Ninachokiona hapa Mataga wengi wanajaribu kwa kila namna kuwatia moyo Watendaji wa Serikali ili waweze kumuenzi Jiwe kwa yale mabaya na ukatili dhidi ya Wapinzani. Hawatafanikiwa pia kwa hilo.
labda mataga lakini si Mimi. Mimi napigania haki katika mlengo wa reconciliation na sio revenge .
 
Back
Top Bottom