Mbowe, mkanye Lissu

Mbowe, mkanye Lissu

Baba jayaron

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2015
Posts
4,324
Reaction score
5,933
Popote ulipo mwenyekiti wa chama.

Tunakufikishia salamu hizi sisi Watanzania tusio na chama na wanachama wa CHADEMA.

Mwambie Tundu Lissu akae kimya wakati huu, aache tabia za kuropoka ropoka na kujibishana asiye jibishane naye.

Mwambie kwenye msiba tamaduni zetu ni kuungana na kua wamoja huo utofauti anaoulazimisha utazidi kumuumbua na kukiumbua chama chenu.

Mwambie hata kama ana uchungu na kisasi kwa yale aliyofanyiwa mwambie kwa nafasi yake hastahili kufanya anayoyafanya labda kama hana mpango wakugombea.

Mwambie anaharibu image ya chama, kama anajua hatarudi wala kugombea mwambie anawaponza wenzake. Mbona wewe (Mbowe) hupost post au anadhani huna bando au smartphone?

Mwambie au mumkanye adharani au mumfute uanachama. Tundu Lissu behave like gentleman.
 
"Tamaduni zenu?"

My foot.. Hizo tamaduni zenu za kijinga na za kishirikina, ni mbaya, ni chafu. Kaeni nazo menyewe. Zinapaswa kuvunjwa haraka.

Mimi nasema hivi;

Tundu Lissu endelea kusema kila lililo muhimu kwa Tanzania na ulimwengu kusikia.
 
Watu kama Lissu wanaishi Tanzania ambayo ipo zaidi mitandaoni haswa JF na Twitter, Tanzania flani ya kufikirika. Kuna ukweli wanauona ila wamegoma kuukubali.

Watanzania ni wapole wapo kimya ila wanajua ukweli na uongo, ukiwapa nafasi watoe maamuzi yao utawaona.

Mara nyingi watanzania wanazungumza kwenye maboksi ya kura na matukio kama haya tulioona wakimlilia Magufuli.
 
Back
Top Bottom