Mbowe muige Raila Odinga shirikiana na Rais Magufuli kuijenga Tanzania yetu!

Mbowe muige Raila Odinga shirikiana na Rais Magufuli kuijenga Tanzania yetu!

Bwashee hebu nikuulize - hicho unachokisema kinawezekana vipi endapo Rais Magufuli hataki kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani? Kwa upande wa Kenya hili liliwezekana kwa kuwa yeye hakuwa na kinyaa cha kukutana na wapinzani.
Rais Magufuli ameshakutana na viongozi wengi tu wa Upinzani pale Ikulu kwa mfano maalimu Seif, Prof Lipumba na mzee Lowassa akiwa bado Chadema.

Ndomana najiuliza huyu Mbowe anafeli wapi bwashee?!
 
Hivi tumewahi kusikia Odinga na wapinzani Kenya wana kesi mahakamani kwa kumuongea vibaya Kenyatta? wenzetu wanaheshimiana zaidi yetu na wanaongea mambo makubwa kuliko hata sisi. Tanzania ya sasa ukisema serikali ya kibepari au ubepari mcharwa unaweza kabisa kufuliwa kesi? Mikutano ya wakati wa kikwete imefanywa haramu wakati sheria inaruhusu eti leo hii upinzani ndiyo ulalamikiwe.

Wengi hapa mseme ukweli tu kwamba hamtaki kuwe na chama cha upinzani au chenye mawazo tofauti huu ndiyo ukweli. Ukiwa na vyama ambavyo vinakubaliana na kila kitu ina maana huna mfumo wa vyama vingi tena. Ni bora nia iwe wazi badala ya kununua wabunge, madiwani na kuwatisha wafanyakazi wa serikali wasifuate sheria kwenye kuwaruhusu wapinzani kufanya mikutano na hata kufanya kampeni zao
 
Mbowe kwa sababu ana wabunge, madiwani na mameya angeweza kutoa ushirikiano wa kisera na kisayansi zaidi!

Unaongelea kitu ambacho hakipo mbona mawazo ya kisera yanatolewa kila siku? je wanasikilizwa basi!
 
Je Mbowe aliongea nini kwenye sherere za uhuru Mwanza je kasikilizwa? Magufuli kafanya nini mpaka sasa?
Mbowe anataka uchaguzi wa serikali za mitaa urudiwe wakati wagombea wao walishiriki!
 
ni uhayawani kuilinganisha Tanzania na Kenya
ni upuuzi kumlinganisha Mbowe na Raila Oginga Odinga (Baba)
ila ni dhambi kubwa pengine umesha kufuru na kuwa kafiri kabisaa kumlinganisha Uhuru na Magufuli
Huwezi kumlinganisha Uhuru na vitu vya ajabu ajabu
 
Hivi upinzani ukiisha ndo sote watanzania tutapata unafuu wa maisha? Akina Cheyo , Shibuda na Mrema nao ni wapinzani? Hebu kuwa na aibu kidogo nyie vijana. Tangia nizaliwe jimbo langu halijawahi kutwaliwa na upinzani bali ni CCM miaka yote lakini hali ni ngumu sana..watu hawana maji, hamna umeme, huduma duni na chache za afya, elimu tangu madarasa aliyojenga Nyerere, barabara tunasikia kwingine sijui kuna tarura sijui nini lakini kwetu hamna...sasa sijui hao wapinzani wanashirikiana na serikali kujenga nini cha ziada..wanasiasa wote ni koooja no CCM, no CHADEMA wote lao moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawezi kushirikiana na dikteta......... Hata huko ndani ya ccm watu wanaangalia show ya kibabe ya mtu mmoja tu........
MKUU ACHA KUFANANISHA KENYA NA VITU VYA HOVYO
 
Mkuu, nadhani hapa Mh Rais Magufuri ndiye anapaswa kumuiga Mh Rais Kenyatta.
Ni ushauri tu kwa mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Upinzani Bungeni mh Mbowe kwamba afanye siasa za kushirikiana na serikali ili tuijenge nchi yetu.

Pale Kenya Kiongozi wa Upinzani mh Raila Odinga yuko mstari wa mbele akishirikiana kwa karibu na Rais Uhuru Kenyata katika kuwaletea wananchi wao maendeleo.

Ni vema Mbowe akaiga jambo hili jema kwa jirani zetu na siyo kupinga pinga tu kila jambo kama Zitto Kabwe wa ACT wazalendo.

Niishie hapo.

Maendeleo hayana vyama!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni rahisi sana kushirikiana na Uhuru Kenyata kuliko kushirikiana na Raila Odinga!JPM ni mtu anayeamini katika chama kimoja,kwake upinzani ni uhaini ndio maana wapinzani katika awamu yake wanapitishwa kwenye tanuru la moto haijawahi kutokea nchi hii!
 
Mbowe ana tatizo moja kubwa, ni kupenda ukuu hivyo hawezi kujishusha na kukubaliana na uhalisia
Ni Mbowe huyo huyo ambaye alimuomba rais kufanya maridhiano ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu 2020!Au hukusikia hotuba yake?
 
Back
Top Bottom