Mbowe muige Raila Odinga shirikiana na Rais Magufuli kuijenga Tanzania yetu!

Mbowe muige Raila Odinga shirikiana na Rais Magufuli kuijenga Tanzania yetu!

Mbona Mrema, Cheyo, Shibuda na Prof Lipumba wanashirikiana na serikali ya Rais Magufuli, yeye Mbowe anafeli wapi?!
Uko serious?Kushirikiana ni kama vile kamari kuu ya TLP kumpitisha JPM kuwa mgombea wa Urais?Au ni kama Lipumba kuiteketeza CUF?Au ni kama Cheyo kuwa domo zege kwa matendo maovu ya watawala?
Tatizo la mpasuko kisiasa linaanzia kwa JPM mwenyewe!
 
Ni ushauri tu kwa mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Upinzani Bungeni mh Mbowe kwamba afanye siasa za kushirikiana na serikali ili tuijenge nchi yetu.

Pale Kenya Kiongozi wa Upinzani mh Raila Odinga yuko mstari wa mbele akishirikiana kwa karibu na Rais Uhuru Kenyata katika kuwaletea wananchi wao maendeleo.

Ni vema Mbowe akaiga jambo hili jema kwa jirani zetu na siyo kupinga pinga tu kila jambo kama Zitto Kabwe wa ACT wazalendo.

Niishie hapo.

Maendeleo hayana vyama!
Mbowe anamkubali sana JPM mpaka kichwa kinamuuma, angetangaza hadharani kuwa hili Burudoza kazi yake haifanani na hata wao walivyokuwa wanawaza.
Lakini nakumbuka mwaka 2016 alizungumza wazi kuwa agenda yao nayo imo kwenye utekelezaji na kwamba hawana la kusema. For that extent Mbowe hana shida ila shida yake ipo kwenye output ya siasa ya Chama chake, kwani Hii 2020 sidhani kama Kutakuwa na upinzani mkubwa labda kutoka ndani ya CCM wenyewe.
 
Back
Top Bottom