Pre GE2025 'Mbowe Must go inalenga kuyumbisha CHADEMA, kuweni Macho wamachama

Pre GE2025 'Mbowe Must go inalenga kuyumbisha CHADEMA, kuweni Macho wamachama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwanini asiondoke anayeuza urithi wa Watanganyika kwa waarabu? Mbowe ana madhara gani kwa taifa hili? Na kwanini wanaccm ndiyo wanataka Mbowe aondoke?
 
Kujua tofauti tu ya M7 na Mbowe umeshindwa, lakini unakaza fuvu kuwa Mbowe must go. Wanaowalipa ndiyo wajinga kuliko hata nyie. Wawe hata wanawapa elimu kidogo
Kwahyo mnataka aendelee?
 
Tuseme ukweli. Waliofanya hadi CDM iwahangaishe CCM ni wakina Slaa, Lissu, Zitto, Mdee, Msigwa, Heche(Bado yupo) na wengine wengi waliotoka. Hawa walimzidi mbali sana mwenyekiti kwa impact dhidi ya CCM. Walikuwa wazuri kujenga hoja kuliko mwenyekiti. Bado CDM ndiyo chama kikuu cha upinzani lakini hakina tena nguvu iliyokuwa nayo kipindi cha majembe hayo. Ukichunguza utaona CCM wanafaidika sana na uwepo wa Mbowe kama mwenyekiti, wameishamsoma, wanammudu.
Nguvu ya Chadema iliathirika sana kipindi cha Magufuli Mbowe alijitahidi sana hadi kufungwa,kufilisiwa nk aliyekifikisha chama hapo kilipo ni Mbowe kwa uongozi wake wa ujasiri. hao unao wasema hawajawahi kuongoza chama. Chadema ni Taasisi na chama kikubwa. kazi ya Mbowe imeonekana, wote hao unaowataja amewa recruit Mbowe ie Heche,Halima, Mnyika etc.Wewe wacha kutumika na akina Msigwa kukisambaratisha chama. Kitavuka tu, Kamanda tuvushe tena
 
Kukubali kuingia kwenye uchaguzi bila katiba mpya,kumeiondolea heshima chadema kama chama cha siasa na kuwa wachumia tumbo!!!

Ni wa kuwapuuza hao!!
Bora nusu shari kuliko Shari kamili. Utambue vyama vya upinzanzi sio chadema tu, vipo na Act, chauma so chadema wakigomea haimaanishi uchaguzi hautakuwepo. Cha maana wataambiwa kutokushiriki pia ni uhuru wa chama na ni demokrasia. Kutoa ccm madarakani mpaka wananchi wachoke haswa na sio Kwa njia ya sanduku
 
Umechagua kutumia mfano mbaya huu, wa Dr Slaa kujengea hoja ambayo ni hoja nzito. 'Credibility' ya William Slaa ilivurugika alipo kubali kukivuruga chama chake mwenyewe na kwenda kuungana na mahasimu wa chama hicho.

Ninacho kubaliana nawe bila pingamizi ni kusikiliza hizo sauti toka nje ya CHADEMA, hasa toka huko ndani ya CCM. Inawezekana hizi sauti zinapazwa sasa baada ya kuona 'project' (mradi wao) walio kuwa wameuanzisha kwa kumtumia Mbowe unaelekea kuvurugika baada ya Mbowe kutambua hadaa alizo kuwa akifanyiwa na 'Chura Kiziwi'.
Sasa matumaini yao yanageuka na kutaka kumvuruga Mbowe na chama chake.

Lakini pia tunapo walaumu CCM na mbinu zao za kutaka kuwavuruga CHADEMA, tusisahau pia kwamba kuna sauti zisizohusiana na CCM zinazomshauri Mbowe aweke maslahi ya nchi zaidi. Kama kuendelea kwake kuongoza chama kunafifisha kwa njia yoyote ile chama kufanya juhudi za kuwaondoa CCM madarakani, sauti hizo nazo zisipuuzwe.
Kusema ukweli Mbowe hafifishi mimi ninaamini CCM Dola ndilo tatizo kubwa pamoja na elimu ya uraia kwa watanzania kuchukua hatua bado sana, mifumo na undumilakuwili wa wana siasa wetu. UKAWA iliumizwa na deep state pamoja na kushinda uchaguzi, Dr Slaa na Lissu ,Vivyo hivyo kwa Zanzibar Maalim Seif. walifanya nini.Hii siyo kirahisi hivyo,sasa hivi pesa zimemwagwa kiuvuruga chadema komaeni msikubali. Mbowe tena!
 
Katiba yao inasemaje? Kama inamruhusu basi aendelee, na wewe acha kuumia kwa yasiyokuhusu
NEndeni mahakamani mukaombe mpewe hati za Mali zote za chama unaweza kuta zinamajina ya Mbowe, madikiteta huwa yanatamaa za mali
 
Kusema ukweli Mbowe hafifishi mimi ninaamini CCM Dola ndilo tatizo kubwa pamoja na elimu ya uraia kwa watanzania kuchukua hatua bado sana, mifumo na undumilakuwili wa wana siasa wetu. UKAWA iliumizwa na deep state pamoja na kushinda uchaguzi, Dr Slaa na Lissu ,Vivyo hivyo kwa Zanzibar Maalim Seif. walifanya nini.Hii siyo kirahisi hivyo,sasa hivi pesa zimemwagwa kiuvuruga chadema komaeni msikubali. Mbowe tena!
Tunatafuta visababu chungu nzima vya kuhalalisha CCM kubaki madarakani. Binafsi sikubaliani na hizo sababu.

Hiyo 'deep state', au 'elimu ya uraia', ni visababu tu visivyo na maana yoyote. Nchi hii ipo tayari sana kupokea mabadiliko ya kiutawala toka kwa CCM wakati wowote.
 
Mmeishiwa hoja,mkishindwa msilalamike mmeonewa kama 2020!!
Kwanini lawama za katiba mpya unazitupa chadema? Kwani chadema ni wakala ama jukwaa la kupigania katiba mpya? Wewe kama ni mwalimu kweli, basi wanafunzi wako wanapoeza muda tu.
 
Tuseme ukweli. Waliofanya hadi CDM iwahangaishe CCM ni wakina Slaa, Lissu, Zitto, Mdee, Msigwa, Heche(Bado yupo) na wengine wengi waliotoka. Hawa walimzidi mbali sana mwenyekiti kwa impact dhidi ya CCM. Walikuwa wazuri kujenga hoja kuliko mwenyekiti. Bado CDM ndiyo chama kikuu cha upinzani lakini hakina tena nguvu iliyokuwa nayo kipindi cha majembe hayo. Ukichunguza utaona CCM wanafaidika sana na uwepo wa Mbowe kama mwenyekiti, wameishamsoma, wanammudu.
Wewe huijui siasa,timu nzuri ya Samia ndiyo inayomsaidia samia siyo yeye kama yeye ndiyo inavyokuwa,uwepo wa hao unawataja i.e Heche, Lissu, Halima, Easther Bulaya ndiyo timu yenyewe kwenye ubora wake ulitegemea nini?
 
Mbowe alishasema haondoki ng'o! Labda wanachama wake wakimkataa. Anasisitiza kuwa hakuna faida ya kuwa mwenyekiti wa CHADEMA 😁😁😁

View attachment 3047374
Bora Msigwa angebaki CHADEMA na kupiga kelele za kumuondoa Mbowe angesikilizwa. Lakini sasa yuko CCM na kupiga kelele za ubaya wa mbowe na kumtaka angatuke, hafanikiwi chochote kwa muujibu wa Mbowe mwenyewe.
Ahhh, Msigwa kapotea!
 
Hawa ni wanasiasa. Bila shaka wanajuana. Usidanganyike!
 
Wala wanachadema hawana habari na hizi cheap propaganda zenu. Kama zina majina ya mbowe wewe unawashwa wapi ili hali hauko chadema?
 
Mbowe alishasema haondoki ng'o! Labda wanachama wake wakimkataa. Anasisitiza kuwa hakuna faida ya kuwa mwenyekiti wa CHADEMA 😁😁😁

View attachment 3047374
Ni kweli

Na kila msimu wa chaguzi zikifika tu, vita ya kumtaka Freeman Mbowe kuachia uenyekiti huanza kwa kasi

Kama katiba ya CHADEMA inamruhusu, mimi nasema Freeman Mbowe na safu yake ya uongozi (makamu wake Tundu Lissu) waendelee mbele mpaka kieleweke.!!
 
Back
Top Bottom