Pre GE2025 'Mbowe Must go inalenga kuyumbisha CHADEMA, kuweni Macho wamachama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwanini asiondoke anayeuza urithi wa Watanganyika kwa waarabu? Mbowe ana madhara gani kwa taifa hili? Na kwanini wanaccm ndiyo wanataka Mbowe aondoke?
 
Kujua tofauti tu ya M7 na Mbowe umeshindwa, lakini unakaza fuvu kuwa Mbowe must go. Wanaowalipa ndiyo wajinga kuliko hata nyie. Wawe hata wanawapa elimu kidogo
Kwahyo mnataka aendelee?
 
Nguvu ya Chadema iliathirika sana kipindi cha Magufuli Mbowe alijitahidi sana hadi kufungwa,kufilisiwa nk aliyekifikisha chama hapo kilipo ni Mbowe kwa uongozi wake wa ujasiri. hao unao wasema hawajawahi kuongoza chama. Chadema ni Taasisi na chama kikubwa. kazi ya Mbowe imeonekana, wote hao unaowataja amewa recruit Mbowe ie Heche,Halima, Mnyika etc.Wewe wacha kutumika na akina Msigwa kukisambaratisha chama. Kitavuka tu, Kamanda tuvushe tena
 
Kukubali kuingia kwenye uchaguzi bila katiba mpya,kumeiondolea heshima chadema kama chama cha siasa na kuwa wachumia tumbo!!!

Ni wa kuwapuuza hao!!
Bora nusu shari kuliko Shari kamili. Utambue vyama vya upinzanzi sio chadema tu, vipo na Act, chauma so chadema wakigomea haimaanishi uchaguzi hautakuwepo. Cha maana wataambiwa kutokushiriki pia ni uhuru wa chama na ni demokrasia. Kutoa ccm madarakani mpaka wananchi wachoke haswa na sio Kwa njia ya sanduku
 
Kusema ukweli Mbowe hafifishi mimi ninaamini CCM Dola ndilo tatizo kubwa pamoja na elimu ya uraia kwa watanzania kuchukua hatua bado sana, mifumo na undumilakuwili wa wana siasa wetu. UKAWA iliumizwa na deep state pamoja na kushinda uchaguzi, Dr Slaa na Lissu ,Vivyo hivyo kwa Zanzibar Maalim Seif. walifanya nini.Hii siyo kirahisi hivyo,sasa hivi pesa zimemwagwa kiuvuruga chadema komaeni msikubali. Mbowe tena!
 
Katiba yao inasemaje? Kama inamruhusu basi aendelee, na wewe acha kuumia kwa yasiyokuhusu
NEndeni mahakamani mukaombe mpewe hati za Mali zote za chama unaweza kuta zinamajina ya Mbowe, madikiteta huwa yanatamaa za mali
 
Tunatafuta visababu chungu nzima vya kuhalalisha CCM kubaki madarakani. Binafsi sikubaliani na hizo sababu.

Hiyo 'deep state', au 'elimu ya uraia', ni visababu tu visivyo na maana yoyote. Nchi hii ipo tayari sana kupokea mabadiliko ya kiutawala toka kwa CCM wakati wowote.
 
Mmeishiwa hoja,mkishindwa msilalamike mmeonewa kama 2020!!
Kwanini lawama za katiba mpya unazitupa chadema? Kwani chadema ni wakala ama jukwaa la kupigania katiba mpya? Wewe kama ni mwalimu kweli, basi wanafunzi wako wanapoeza muda tu.
 
Wewe huijui siasa,timu nzuri ya Samia ndiyo inayomsaidia samia siyo yeye kama yeye ndiyo inavyokuwa,uwepo wa hao unawataja i.e Heche, Lissu, Halima, Easther Bulaya ndiyo timu yenyewe kwenye ubora wake ulitegemea nini?
 
Mbowe alishasema haondoki ng'o! Labda wanachama wake wakimkataa. Anasisitiza kuwa hakuna faida ya kuwa mwenyekiti wa CHADEMA 😁😁😁

View attachment 3047374
Bora Msigwa angebaki CHADEMA na kupiga kelele za kumuondoa Mbowe angesikilizwa. Lakini sasa yuko CCM na kupiga kelele za ubaya wa mbowe na kumtaka angatuke, hafanikiwi chochote kwa muujibu wa Mbowe mwenyewe.
Ahhh, Msigwa kapotea!
 
Bora Msigwa angebaki CHADEMA na kupiga kelele za kumuondoa Mbowe angesikilizwa. Lakini sasa yuko CCM na kupiga kelele za ubaya wa mbowe na kumtaka angatuke, hafanikiwi chochote kwa muujibu wa Mbowe mwenyewe.
Ahhh, Msigwa kapotea!
Hawa ni wanasiasa. Bila shaka wanajuana. Usidanganyike!
 
Wala wanachadema hawana habari na hizi cheap propaganda zenu. Kama zina majina ya mbowe wewe unawashwa wapi ili hali hauko chadema?
 
Mbowe alishasema haondoki ng'o! Labda wanachama wake wakimkataa. Anasisitiza kuwa hakuna faida ya kuwa mwenyekiti wa CHADEMA 😁😁😁

View attachment 3047374
Ni kweli

Na kila msimu wa chaguzi zikifika tu, vita ya kumtaka Freeman Mbowe kuachia uenyekiti huanza kwa kasi

Kama katiba ya CHADEMA inamruhusu, mimi nasema Freeman Mbowe na safu yake ya uongozi (makamu wake Tundu Lissu) waendelee mbele mpaka kieleweke.!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…