Ukiangalia tabia ya Mbowe kwenye uongozi ni mtu mvumilivu, ana subra, hekima, busara, na hupenda kutumia diplomasia. Ni mjenga hoja zenye mashiko. Wakati Lissu ni mkali, mharakati, havumilii sana, na anayo subra ndogo.
Hapendi kutumia diplomasia, yeye ni koleo kwa koleo, lakini ni mjenga hoja nzito na zenye mashiko pia. Ukiwa na watu wenye tabia na mitizamo na mchanganyiko tofauti kama huu, unatengeneza "checks and balances" ili mradi wote wakatambua na kukiri umuhimu wa karama ya mwenzake, chama kitasonga mbele.
Si rahisi kujenga chama kwa viongozi wenye tabia, mwelekeo, na mitizamo unaofanana. Kila mmoja atafaa mahala fulani, kipindi fulani, na kwa mazingira fulani kufanikisha malengo ya chama, ili mradi sera, mifumo, na taratibu za chama zinaheshimika. Nyie wengine mnasemaje?