Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Jana Mwenyekiti Mpya wa CHADEMA Tundu Lissu, alikwenda kwa mara ya kwanza makao Makuu ya CHADEMA kama Mwenyekiti wa chama hicho.
Lakini tangu ashinde nafasi hiyo mambo mengi yamesemwa dhidi yake na pande mbili zilizokuwa kinyume chake.
Upande wa kwanza ni watu wa CCM. Na ingekuwa ajabu kama CCM wasingesema mabaya dhidi ya Lissu kama ambavyo wangesema mabaya dhidi ya Freeman Aikaeli Mbowe kama naye ndiye angeshinda.
CCM hawaitaki CHADEMA inayoongozwa na Lissu wala Mbowe. Ushahidi unaonesha CCM haikuwahi kuwa na wema Kwa CHADEMA enzi Mbowe akiwa Mwenyekiti na Wala haitakuwa na wema sasa hivi Lissu alivyo Mwenyekiti.
Lakini upande mwingine ni waliokuwa wafuasi wa Mbowe kwenye Kampeni za uchaguzi uliomweka Lissu madarakani. Hawa pia inaeleweka ni kwa nini kwa Sasa hawana furaha na ushindi wa Lissu.
Lakini wafuasi wa Mbowe hawatakiwi kumshambulia Lissu Kwa maneno ya uzushi kama wafanyavyo watu wa CCM.
Kwa mfano kusema kuwa Lissu alikuwa anamtukana Mbowe kwa ivo Mbowe asifanye kazi na Lissu. Haya maneno yanatakiwa yasemwe na CCM na siyo na wanachadema.
Kweli mtu anawezaje kusema Lissu kashinda kutokana na kumtukana Mbowe? Yaani mwachadema unawezaje kusema kuwa ushindi wa Lissu ulitokana na kumtukana Mbowe. Alimtukanaje?
Kwa nini mtu anajifanya ni mwanachadema lakini anashikilia kuwa "Mbowe hawezi kumsamehe Lissu". Yaani tunawezaje kuona maridhiano na CCM ni jambo linalowezekana lakini hatuoni kama Mbowe na Lissu wanaweza kufanya kazi kwa pamoja?
Kwa hakika Mbowe na Lissu ni wamoja.