SI KWELI Mbowe na Mnyika Waisifia TAMISEMI. Lissu atakiwa kuwapisha CHADEMA huku Fedha za Chama zikielekezwa uchaguzi kanda ya Kaskazini kisa chama hakina hela

SI KWELI Mbowe na Mnyika Waisifia TAMISEMI. Lissu atakiwa kuwapisha CHADEMA huku Fedha za Chama zikielekezwa uchaguzi kanda ya Kaskazini kisa chama hakina hela

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mbowe na Mnyika Waisifia TAMISEMI. Lissu atakiwa kuwapisha CHADEMA huku Fedha za Chama zikielekezwa uchaguzi kanda ya Kaskazini kisa chama hakina hela.

si kweliJF.jpg
 
Tunachokijua
Freeman Aikaeli Mbowe mwanachama na mwenyekiti wa cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Alikuwa mmoja wa waasisi wa CHADEMA mwaka 1992. Mbowe anafahamika kuwa mpangaji mahiri wa mikakati, na hivyo kumfanya kuwa mmoja wa viongozi wa juu kabisa wa siasa nchini.

Mnamo mwaka 2005 Mbowe aliwania urais wa Tanzania kupitia chama chake cha CHADEMA ambapo hakufanikiwa kushinda kiti hicho.

Novemba 19, 2024 Freeman Mbowe alifanya Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo kabla ya yeye kuzungumza alitangulia Mkurugenzi wa Ikifaki na Mawasiliano CHADEMA, John Mrema ambaye alimkaribisha Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika kuzungumza kuweka utangulizi kabla ya Freeman Mbowe kuzungumza.

Je, Mbowe na Mnyika wameipongeza TAMISEMI?

Mara baada ya Mkutano huo kumeibuka Posta zinazoonekana kama za Jambo Tv, Moja ikiwa imebeba ujumbe unaodai kuwa Mnyika ameipongeza TAMISEMI kwa kurudisha wagombea wengi wa CHADEMA walioenguliwa (Tazama hapa)

Na nyingine Ikiwa na ujumbe kuwa Mbowaipongeza TAMISEMI kwa maadalizi mazuri kuelekea uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa. (Tazama hapa)

Uhalisia Upoje?

Jamiicheck imefatilia Mkutano wa Freeman Mbowe na Waandishi wa Habari uliofanyika Makao Makuu ya CHADEMA, 19 Novemba 2024 na kubaini kuwa Posta hizo Si za kweli kwani John Mnyika na Freeman Mbowe hawajaipongeza TAMISEMI kwa kitu chochote kile.

Aidha, Mbowe na Lissu wamezungumzia kuhusu kulalamikia mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotegemewa kufanyika Novemba 27 2024 ambapo Mbowe na Mnyika wameeleza kuwa Wagombea wa CHADEMA wameenguliwa na kubakizwa .... tu kitu ambacho Mbowe amedai ni ubakwaji wa Demokrasia.

Vilevile, Jambo Tv hawajaposti taarifa kama hizo kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii hivyo kuthibitisha kuwa posta hizo zimetengenezwa na kuwekwa nembo ya Jambo Tv ili kupotosha.

1732025076052-jpeg.3156212

1732024917302-jpeg.3156203
Je, Mbowe ameuliza kuhusu pesa alizochangiwa Lissu kununua gari?

JamiiCheck imebaini kuwa Katika mkutano wa Mbowe na waandishi wa habari wa Novemba 19 2024, Mbowe hakuuliza kuhusu Pesa zilizochangwa na Wananchi kumnunulia Gari Lissu baada ya wadau kutaka lile alilopata nalo shambulio la risasi liwekwe makumbusho (tazama hapa)

Aidha taarifa hiyo haikutolewa na JamiiForums wala Mwanahalisi digital.

1732024762238-jpeg.3156190

Je Mbowe alitoa kauli ya kumfukuza unachama Tundu Lissu?

Katika mkutano wake na waandishi wa habari Mbowe si kweli kwamba alisema CHADEMA haitasita kumfukuza uanachama wala kumtuhumu Lissu kuivunja CHADEMA, aidha taarifa hiyo haikutolewa na JamiiForums wala Mwanahalisi digital.

Chapisho linalodaiwa kuwa la Mwanahalisi digital lina mapungufu kadhaa yanayodhihirisha kuwa si chapisho rasmi la Mwanahalisi ni pamoja kutokuwepo kwa mstari mwekundu unaozunguka poster nzima, kadhalika kutofautiana kwa sehemu ya nyuma ya rangi nyekundu panapoandikwa kichwa cha habari.

Chapisho linalodaiwa kutolewa na JamiiForums limebainika kuwa na mapungufu kadhaa ukilinganisha na machapisho rasmi ambayo hutolewa na JamiiForums katika kurasa zake za mitandao ya kijamii, sehemu ya mapungufu hayo ni kutofautiana kwa rangi, ambapo rangi iliyotumika haitumiwi na JamiiForums katika maudhui ya kisiasa, pia kutofautiana kwa mwandiko (fonts) wa maandishi yaliyotumika kuandika kichwa cha habari (title), si ule unaotumiwa na JamiiForums, uwepo wa alama ya taarifa zaidi upande wa juu kushoto ambayo humiwa kwenye machapisho yenye kurasa zaidi ya moja (slides)

Aidha nukuu inayodaiwa kutolewa na Mbowe juu kutaka kumuondoa Makamu mwenyekiti Tundu Lissu na kusambaa kupitia Chapisho linaloonekana kuwa la Kasuku news. Kadhalika taarifa hiyo isiyo ya kweli juu ya madai ya Mbowe kutaka kumfukuza uanachama Lissu imesambazwa pia kupitia ukurasa wa Korosho media.

Madai kuhusu CHADEMA kukosa fedha za uchaguzi na zilizopo kupelekwa kanda ya kaskazini

Kumekuwapo na taarifa zinazosambaa pia zikieleza kuwa Mbowe amesema Chama hakina fedha za uchaguzi na zilizopo zimeelekezwa kwenye uchaguzi kanda ya Kaskazini kusaidia uchaguzi wa Chama.

Akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari Mbowe alieleza kuwa Vyama vya upinzani havina fedha wala vitendea kazi na badala yake wanajitolea na hakusema kuwa Chama hakina fedha za uchaguzi na zilizopo zitaenda kutumika kwenye uchaguzi kanda ya kaskazini

“Chama Cha Mapinduzi hakioni aibu kupambana na vyama vya upinzani ambavyo havina fedha, havina vitendea kazi, havina magari, watu wanajitolea’’ alisema Mbowe.

Pia taarifa hiyo inayosambazwa ikiwa na grafiki ya Jambo Tv haipo kwenye kurasa rasmi za mitandao ya Jambo Tv.

Madai kuhusu Mnyika kuwasifia TAMISEMI kwa kuwarudisha wagombea wa CHADEMA

Kumekuwapo na taarifa inayodai kuwa Katibu mkuu wa CHADEMA, John Mnyika kwenye mkutano uliofanyika leo tarehe 19/11/2024 ameipongoza Wizara ya TAMISEMI kwa kuwarudisha asilimia kubwa ya wagombea wa CHADEMA walioenguliwa mwanzoni.

Akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari Mnyika hakutoa pongezi kwa wizara hiyo kuhusu suala la kurudisha wagombea na badala yake aliongelea kuhusu kutokukubaliana na maneno ya Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa kuwa CHADEMA ilikubaliana na mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

‘’Sisi CHADEMA hatujakubaliana na TAMISEMI katika hatua yoyote juu ya huu utaratibu mbovu wa usimamizi wa uchaguzi kwanza uchaguzi kusimamiwa na waziri wa TAMISEMI, pili uchaguzi kusimamiwa na kanuni mbovu na mbaya, kutolewa kwa ratiba mbaya ya uchaguzi na hatimaye usimamizi wa uchaguzi kwa ujumla wake kusimamiwa na watu wasio huru waliofanya engua engua ya wagombea katika maeneo mbalimbali ya uchaguzi’’ Miongoni mwa maneno aliyozungumza Mnyika katika mkutano na waandishi wa habari.

Lakini pia taarifa hiyo iliyokuwa inaonekana na grafiki ya Jambo tv haijatolewa na Jambo Tv na pia wao wenyewe wamekanusha kutoa taarifa hiyo.
Ila CCM kwa uongo khaaa

Lucas Mwashambwa ndio kazi yenu uvccm kuzalisha propaganda za uongo kiasi hiki, mmejaza taifa uongo uongo tu ovyo kabisa nyie
 
Back
Top Bottom