GE2025 Mbowe na Mpina: Mfano wa Wanasiasa wasio na Mioyo ya Shukrani

GE2025 Mbowe na Mpina: Mfano wa Wanasiasa wasio na Mioyo ya Shukrani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mzee

Platinum Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
13,620
Reaction score
5,868
Habari za leo Watanzania

Tukiwa tunaelekea ktk Uchaguzi mkuu, zimefika zile nyakati za Wanasiasa kuhama Chama hiki kwenda kile kwa Maslahi ya Kisiasa.

Naomba kuwagusia hawa Wanasiasa wawili kama mfano wa namna Wanasiasa wasivyo na Mioyo yenye Shukrani.

1.Freeman Aikael mbowe ameingia ndani ya Chama tangu kinaanzishwa mwaka 1992, kwa zaidi ya Miaka 30 amekuwa ndani ya nyadhifa mbali mbali. Na zaidi ya Miaka 20 amekuwa Mwenyekiti wa Chadema.

Kupitia Chadema ameweza kuwa Mbunge na Kiongozi mkuu wa kambi ya Upinzani Bungeni KUB. Haya yote ni mafanikio makubwa ya kisiasa.

Kupitia Chadema amekuwa mgombea Uraisi. Chama kimempa mafanikio. Sio kwamba amekisaidia Chama pekee. Chama nacho kilimpa nafasi.

Mwaka huu amepumzishwa kuwa Mwenyekiti, akaachiwa Mjumbe wa kudumu wa Halmashauri kuu anaamua kususa na kuanza kukipasua Chadema. Je alitaka kuwa Mwwnyekiti mpaka siku anaingia kaburini???

Hii ni roho mbaya, roho isiyo na Shukrani, roho isiyo tosheka.

2. Luhaga Mpina amekuwa ndani ya CCM kwa zaidi ya Miaka 20 na amekuwa Mbunge Kisesa kwa Miaka 20 kupitia CCM.

Aliingia Bungeni akiwa na miaka 31, sasa ana miaka 51.

Kupitia CCM amekuwa Mbunge na Waziri, hizi ni nafasi za Juu sana kisiasa. Mwaka huu CCM wanamkata ktk kugombea Ubunge ambao amekaa kwa miaka 20 anakasirika na kuhama CCM.

Je! alitaka akae Kisesa kwa miaka Mingapi?. Je anadhani Kisesa haina mwanaCCM mwingine wa kuliongoza?

Mpina hajaondoka CCM kwasababu anaichukia CCM, hajaondoka CCM sababu ya Wizi na madudu ya CCM. Ameondoka CCM kwakua maslahi yake yanaanza kuondolewa.


Hii ni ishara kuwa Mpina ni aina ya Viongozi ambao wana Roho mbaya sana, hawatosheki, hawana Shukrani.

Kuna haja ya kuwakataa.
 
Hii ni ishara kuwa Mpina ni aina ya Viongozi ambao wana Roho mbaya sana, hawatosheki, hawana Shukrani.
Kama ni suala la kuwa na shukrani, basi tungeanza na Sa100 ambaye hajawahi hata kuota kuwa makamu wa Rais, amepata hadi Uraisi na bado hataki kuondoka. Siasa za Tanzania haziko hivyo, siasa sio shukrani.
 
Kama ni suala la kuwa na shukrani, basi tungeanza na Sa100 ambaye hajawahi hata kuota kuwa makamu wa Rais, amepata hadi Uraisi na bado hataki kuondoka. Siasa za Tanzania haziko hivyo, siasa sio shukrani.
Ulitaka agombee mamako? Unaandika vt ht havihusiani.
 
Mpina hajatendewa haki na Mwenyekiti wa ccm taifa mama sa100, wananchi bado wanampenda kwangu mimi Mpina yuko sahihi kuhama chama, alichokosea ni kwenda kugombania nafasi ya urais, angerudi jimboni kwake angeshinda saa 3 asubuhi, ila kwenye urais pia anaweza akaleta changamoto kwa samia kwa upande wa kanda ya ziwa
Mbowe yeye ni mbinafsi anayeangalia maslahi yake binafsi, hana shukrani wala hajali wengine inapokuja kwenye hela,
 
Back
Top Bottom