Mbowe na wapambe wake tuambieni kiasi gani mbowe alitumia kumsaidia Tundu Lissu tumlipe

Mbowe na wapambe wake tuambieni kiasi gani mbowe alitumia kumsaidia Tundu Lissu tumlipe

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2014
Posts
4,664
Reaction score
9,929
Eeeh tusichoshane kwa mijadala isiyo na afya ooh Lisu hana adabu katumia sana pesa ya Mbowe haya sasa nguvu ya umma tunamtaka Lissu nyie timu mbowe leteni gharama alizotumia boss wenu tumrudishie
 
Sio kila kitu unaweza ukabadisha na gharama za fedha. Mbowe alishikilia dripu ya damu kutoka Dodoma hadi Nairobi, haya changisha umlipe!
Ukute yeye ndio alikuwa sababu ya hiyo damu kutoka.
Kwa speed tunayokwenda nayo, soon mbivu na mbichi zitajulikana.
 
Kuna anayekusaidia ili aje aumiliki utu wako, msaada wake hauji kwa kukutakia heri bali ainunue nafsi yako...

Yupo tayari kukufanya ushindwe kujitegemea, hatoridhia kuona ukisimama na ukitembea labda ukichechemea.

Msaada usipotoka moyoni aliyeutoa hudai malipo, anaweza kukudhalilisha kwa namna yeyote popote ulipo.

Usipo wiwa kutoa usitoe tafadhali, kuliko ukatoa ukaondoa hata ule uafadhali.

Hauwezi kuwa msaada.

@X Ray
 
Mtu anakupa mswaki kisha anakung'oa jino....
 
Hayo madai ya mhusika mwenyewe na wafuasi wake kuwa katumia fedha zake binafsi nyingi kukijenga chama na viongozi wengine ndani ya chama ni ishara ya umiliki wa chama na kutokuwa tayari kuona maamuzi ndani ya chama yasiyo m-favour.
 
Eeeh tusichoshane kwa mijadala isiyo na afya ooh Lisu hana adabu katumia sana pesa ya Mbowe haya sasa nguvu ya umma tunamtaka Lissu nyie timu mbowe leteni gharama alizotumia boss wenu tumrudishie
Unaweza kulipa muda, hisia na akili zilizotumika kumtengeza na kumbrand mtu?
 
Sio kila kitu unaweza ukabadisha na gharama za fedha. Mbowe alishikilia dripu ya damu kutoka Dodoma hadi Nairobi, haya changisha umlipe!
Kwamba ile stand ya drip ilikosekana?
 
Eeeh tusichoshane kwa mijadala isiyo na afya ooh Lisu hana adabu katumia sana pesa ya Mbowe haya sasa nguvu ya umma tunamtaka Lissu nyie timu mbowe leteni gharama alizotumia boss wenu tumrudishie
Mchangieni kwanza hela alizoomba kununulia gari, halafu ndo uje na upupu wako hapa.
 
Back
Top Bottom