Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo Februari 18, 2022 inatarajiwa kutoa uamuzi kama Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe pamoja na Washtakiwa wengine watatu wana Kesi ya Kujibu au Hapana.
Ile siku iliyosubiriwa ya kutolewa maamuzi kesi Mbowe na wenzake 3 kama wana kesi ya kujibu au hawana ni leo 18 Februari 2022 ambapo Jaji Tiganga anatarajiwa kutoa maamuzi hayo katika mahakama kuu ya Uhujumu Uchumi na Rushwa.
Kujua kesi ilipoishia fungua kiunganishi hiki:
Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe na Wenzake. Tumaini Swila amaliza ushahidi. Mawikili wa Serikali wafunga Ushahidi. Jaji kutoa uamuzi 18/02/2022
=========
UPDATES
1230hrs: Freeman Mbowe na wenzake, bado hawajafikishwa Mahakamani. Kesi itaanza kusikilizwa saa nane za Mchana.
1330hrs: Freeman Mbowe na Wenzake wamefikishwa mahakani.
=========
Jaji ameingia Mahakamani Saa 8 na Dakika 55.. Yupo Tayari..
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Jamhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ikupendeze naitwa Robert Kidando nipo pamoja na
- Wakili Pius Hilla
- Abdallah Chavula
- Jenitreza Kitali
- Nassoro Katuga
- Esther Martin
- Ignasi Mwinuka Mawakili Wa Serikali Waandamizi na
- Wakili Tulimanywa Majige Wakili wa Serikali
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja
- Iddi Msawanga
- Sisty Aloyce
- John Malya
- Edward Heche
- Jeremiah Mtobesya
- Nashon Nkungu
- Fredrick Kihwelo
- Dickson Matata
- Michael Mwangasa
- Seleman Matauka
- Alex Massaba
- Gaston Garubindi
- Khadija Aron
- Evaresta Kisanga
- Maria Mushi
- Paul Kisabo
Jaji anaita Washitakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya kutolewa Uamuzi Mdogo baada ya Upande Wa Mashitaka Kufunga Kesi Yetu tupo tayari Kupokea Uamuzi Mheshimiwa Jaji
Wakili Peter Kibatala: nasi pia Mheshimiwa Jaji tupo tayari Kwa ajili ya Kupokea Uamuzi Mdogo
Jaji anaandika Kidogo Mahakama ipo Kimyaaa
Jaji kama ambavyo Mawakili Wame zungumza Kwamba Shauri lipo Mahakamani Kwa ajili ya Uamuzi Mdogo.. Na Uamuzi huu Mdogo upo tayari, Nafanya Chini ya Kifungu cha 41 cha Sheria ya Uhujumu Uchumi, Sura ya 200, Ikitaka Kujibu Kama Washtakiwa Wana la Kujibu au Hapana
Jaji: Kupima Ushahidi, na angalia Kama Kuna chochote Cha Kuita Washtakiwa Waweze Kujitetea, Kama Mahakama ikiona Kwa Ushahidi Uliletewa Wana Kesi ya Kujibu, Watapata nafasi Ya Kujitetea, Na Mahakama ikiona Pia Kwa Ushahidi Uliletewa Hawana Vya Kujibu Basi Mahakama Itawaachia huru
Jaji: Kwa Mujibu Wa Sheria Kesi ya Mahakama Ya Rufani Phillip Vs Jamuhuri Kesi namba 217/2020, Mahakama Ilisema Kwamba Mahakama hii inakwenda Kutekeleza Jukumu hilo, Mahakama Kabla haijafika ni Vizuri iseme Washtakiwa ni akina nani na Wameshtakiwa Kwa Makosa Gani
Jaji: Washtakiwa Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe, Washtakiwa Wameshtakiwa Kwa Makosa Sita. Makosa ya Kula Njama Kutenda Vitendo vy Kigaidi Kwamba walivunja Kifungu Namba 4(3)i, 2(2), 9, na Kifungu cha 27 (c) la Sheria ya Uhujumu Uchumi
Shitaka la Pili Ni la Mshitakiwa wa Nne, anashitakiwa kwa Kosa la Kufadhili Ugaidi Kifungu cha 57, 62 Kosa Lingine ni Kushiriki Kikao cha Kula Njama Kutenda Vitendo Vya Kigaidi Hapa Wanadaiwa Kuvunja Sheria Kifungu cha 4(1) 3,5 na 57 ya Sheria ya Kuzuia Ugaidi
Na Kosa la Tano ni Mshtakiwa wa Kwanza Peke yake Kukuta na Vifaa ambavyo ni Vya Kutendea Ugaidi, Anadaiwa Kuvunja Sheria Kifungu cha 6(1), 3(1)
Jaji: Maelezo ya Mashtaka ni kwamba Washtakiwa Wote Wanne Wanadaiwa Siku ya Tarehe 1 May 2020 wakiwa katika Hotel ya HAI, na Maeneo Mbalimbali ya Arusha, Mwanza na Morogoro, Walikula Njama ya Kutaka Kuchoma Vituo Vya Mafuta
Vitendo ambavyo Walikuwa wanataka Kuleta Hofu Kwa Watanzania, Katika Kifungu hicho hicho Washtakiwa Wanadaiwa Kula Njama Kutaka Kumdhuru Lengai Ole Sabaya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Kwa Kutaka Kuleta Hofu na Taharuki Kwenye Nchi
Jaji: Mshtakiwa Namba Nne Katika vipindi Mbalimbali yeye Mwenyewe alitoa Fedha Mbalimbali Kwa Mshtakiwa Namba 1,2,na 3, Kama Sehemu Ya Kutaka Kufadhili Ugaidi, Vitendo ambavyo Vilikuwa Vilete Madhara Kwa Watanzania na Kuleta Hofu Kwa Watanzania,
Washitakiwa namba Moja, Mbili, tatu na Moja, Wanadaiwa Kushiriki Katika Vikao kwa nia ya Kutaka Kulipua Vituo Vya Mafuta Vitendo Vilivyo Lenga Kuleta Hofu Kwa Watanzania..
Jaji: Kosa la Tano ni Mshtakiwa Namba Mbili , Eneo la Rau Madukani Mshitakiwa alikurwa anamiliki Bastola aina ya Luger A5340 ambayo Silaha hiyo ililenga Kutumika katika Vitendo Vya Kigaidi,
Jaji: Kosa la Tano ni Mshtakiwa Namba Mbili , Eneo la Rau Madukani Mshitakiwa alikurwa anamiliki Bastola aina ya Luger A5340 ambayo Silaha hiyo ililenga Kutumika katika Vitendo Vya Kigaidi,
Jaji: Kosa la Sita Mshtakiwa Namba Moja ndiye anayeshakiwa Peke yake, Ambapo Mshtakiwa Namba Moja alikutwa anamiliki pair Nne za Suruali za JWTZ, pair Nne za Suruali za JKT, pair Moja la Shati la JWTZ, pair Moja ya Shati la JKT
Jaji: Kosa la Sita Mshitakiwa Namba Moja ndiye anayeshakiwa Peke yake, Ambapo Mshitakiwa Namba Moja alikutwa anamiliki pair Nne za Suruali za JWTZ, pair Nne za Suruali za JKT, pair Moja la Shati la JWTZ, pair Moja ya Shati la JKT
Jacket, Kofia Tano za JWTZ, overoli la JWTZ, Ponjol Ya JWTZ, ballet Mbili za Kofia za JWTZ, Beji Mbili za HASSAN HD, Renki Mbili Vyeo Vya Coplo Mali ya JWTZ, Kidaftari Cha 5Srar ambacho alikutwa nacho, Mikanda Minne ya JWTZ, pair Moja ya Soksi , pair Moja ya Rasketi ya JWTZ
Kakutwa na Wing Moja ambayo ni Beji ya Ku attend Mafunzo ya Parashuti, Kisu cha AK 47 CHA JWTZ, Vitu Vyote Vililenga Kutumika katika Matendo Ya Ugaidi.
Jaji: Washtakiwa Wote Waliposimamishwa Mbele ya Mahakama Walikana Makosa, Mbele ya Kaka Yangu Jaji Siyani (Jaji Kiongozi Walikana Mashtaka yao, Walikubali Tu Maelezo Yao ya Particulars). Walikubali Kuwa Waliwahi Kufanya Kazi Katika Kambi ya Ngerengere.
Jaji: Mshtakiwa Namba Nne (Freeman Aikael Mbowe) alikiri kuwa ni Mwenyekiti Wa Chadema na Kwamba alikamatwa Mwanza Nyamagana,
Jaji: Upande wa Mashtaka Waliongozwa na Mawakili Robert Kidando, Pius Hilla, Abdallah Chavula, Jenitreza Kitali, Nassoro Katuga, Ignasi Mwinuka, na Wakili wa Serikali Tulimanywa Majige.
Jaji: Kwa Upande Wa Utetezi walikuwa Mawakili 19.. Jeremiah Mtobesya na Nashon Nkungu wakimwakilisha Mshtakiwa wa 1, John Mallya Mshtakiwa Wa 2, Fredrick Kihwelo na Dickson Matata wakimwakilisha Mshitakiwa Wa 3, Peter Kibatala na Mawakili Wengine Wakimwakilisha Mshtakiwa Wa 4
Jaji: Mashahidi walikuja Walikuwa ni ACP KINGAI Kaaya Hafidh Mahita Madembwe Gladys Fimbari Luteni Denis Urio Swila Goodluck
Walileta Vielelezo, Silaha tab Bastola aina ya Luger A5340, Risasi Hai, Maganda Mawili Ya Risasi, Barua Kutoka Tigo, Mhamala Wa Fedha Kutoka TIGO, KYC, Barua Kutoka Kwa Marajisi, Certificate ya Handing Over ya Bastola, Seizure Certificate ya Kukamata Uniform za Mshitakiwa Wa kwanza, Barua ya Kamishina Wa Forensic Beaural, KYC ya 0784779944, KYC ya 0782 237913, Financial Transactions Riport ya 0787 555200, Financial reports Ya 0784779944, Taarifa Ya Uchunguzi kutoka Extraction Report, Simu Moja ya Techno labeled A, labeled B, labeled C, Lebeled D na Simu labeled H, Certificate of handing over ya Pistol, Certificate Ya Inspector Swila N Luteni Denis Urio.