saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 624
- 1,456
MBOWE NA ZITTO KWANINI WAMEAMUA KUZIACHA HOJA ZA WANANCHI MIKUTANO YA HADHARA
Nimefuatilia mikutano ya hadhara ya Chadema na ACT Wazalendo sijawasikia Mbowe wala Zitto wakizungumzia au wakipaza sauti zao juu ya mambo makubwa yanayolalamikiwa na wananchi.
Mfano suala ulinzi wa rasilimali za Taifa, utoroshaji wa Madini na mambo ya Makinikia, suala la kushamiri kwa Ujangili wa wanyama pori, kushamiri kwa Uvuvi Haramu mpaka ndege zilizokuaa zinatua Mwanza na kupeleka samaki Ulaya haziji tena kwa kukosa samaki.
suala la ubadhirifu wa mali za umma na ufisadi, kushuka nidhamu kazini kwa watumishi wa umma, sintofahamu wanazokumbana nazo machinga, mama ntilie, wachimbaji wadogo wa Madini, Wavuvi, mauaji ya wakulima na wafugaji, Mifugo kupigwa risasi.
utoaji hafifu wa huduma za afya na malalamiko ya wananchi kukosa dawa baadhi ya hospitalini.
Umeme kukatika hovyo watu kupoteza ajira zinazotegemea umeme, mikataba yenye mashaka inayopigiwa kelele ya SGR Tabora Kigoma, gharama za ukarabati wa Kivuko cha MV Magogoni Bilioni 7.5.
Tanzania kuagiza mchele kutoka nje ikiwa tunayo Ardhi ya kutosha ya kulima mpunga, mgogoro wa ruzuku ya mbolea, usimamizi duni wa miradi ya madarasa na vituo vya afya maeneo mbalimbali nchini ambayo imetumia fedha nyingi za umma na maeneo mbalimbali.
Lakini jambo la kusikitisha maeneo yote ambayo Wananchi ndio wanalalamikia sana wao Mbowe na Zitto wameyaacha kabisa kuyazungumzia wala kutoa ushauri kwa Serikali.
Badala yake mikutano yao imebeba maudhui makubwa ya kuwaeleza watanzania juu ya ubaya wa Serikali ya awamu ya tano.
Nini kimesababisha Mbowe na Zitto wameyaacha mambo yanayolalamikiwa na wananchi kwa sasa na kujikita kutuelezea ubaya wa Serikali ya Magufuli ambayo wote tulikuwepo tangu anaapishwa Novemba 2015 hadi anafariki dunia Machi 17, 2021.