Uchaguzi 2020 Mbowe, nakuahidi kuwa CHADEMA hamtochukua nchi ila wewe utakosa Uenyekiti

Labda ndugu zangu niwape brief kidogo ninyi mnaosema nchi nzima kuanzia kwnye serikali za mitaa hadi taifa tuvae kijani. Kipindi hiki kifupi ambacho CCM imechukua serikali za mitaa tunataabika sana kupata huduma hata ya barua tu kinyume ilivyokuwa wakati mitaa ikiongozwa na CHADEMA. Ku fanya process ya kitu kidogo unaambiwa lipa posho za wajumbe mara muhuri na kadhalika. Pamoja na kufanya hivyo bado uwezekano wa kupata kitu kwa wakati unakuwa mdogo sana sana. Kuna rushwa ya hali ya juu ndani ya serikali za mitaa kuliko kipindi kingine chochote. unakwamishwa na mtendajii wa mtaa au wa kata kama huna hela mfukoni. Wacha CCM ichukue kila mahali corruption index itapanda na uchumi lazima utashuka. kuhalalisha rushwa kulianzia juu tulipoambiwa tuwape traffic hela ya ku brush kiatu. Sasa kitakachowazuai wengine kudai kifuta viatu ni nini? Nchi itarudi reverse ambayo haijawahi shuhudiwa ni suala la muda. Hakuna atakayesema acha na wote watakuwa wanaongea lugha moja
 
Mwaka huu hakuna cha kuchezea uchaguzi wala kuchakachua matokeo jiandae kisaikojia wauaji wakubwa Marekani inawaweka kwenye rada tu.
 
Mkuu uoni kumuandama sana Bw Mbowe huku wewe ukitokea CCM tawala chenye kila aina ya silaha lukuki ni kama unaogopa kivuli chake?
Hatusemi Mh.Mbowe ni malaika,lakini hiyo sekeseke aliopata toka mjomba Magu akalie kiti cha enzi si ndio mmezidi kumuongezea pointi?
Kabomolewa Bilcanas club yake,hadi leo haijajengwa chochote ili kumkomoa,kaharibiwa mazao shambani kwake kisa DC anatafuta URC,kakaa gerezani vipindi vingi tu kwa tuhuma ya uchochezi,kila siku yupo mahakamani hadi amegeuka sugu wa kesi za kisiasa. Mikutano yake mara nyingi imezuiwa hata press conference nazo wanamzuia.Kama haitoshi hata huko bungeni hoja zake zimetupwa kapuni na spika.
Nakushangaa sana wewe kuendekeza ubaguzi wa wazi kwa binadamu mwenzio kuliko hata kaburu wa Africa Kusini.Au unalipwa kujitoa ufahamu?Kumbuka kuna kesho na kuna Mungu.
Siasa sio vita ni nguvu ya hoja.
 
Kwanini tunamuandama shetan wakat Mungu ndie mwenye kila kitu?
 
Ushauri huo kampe meko na bashiru,membe tu kawatoa puru mpka mmemfukuza ili asimpinge.ccm inaendesha na mtu mmoja hakuna kupingwa au kukosolewa
 
Hivi Mbowe akikosa Uenyekiti ATAKUFA????? Au itakuwa mwisho wa Dunia. Kwanini wapinzani wa CDM hawataki Mbowe awe Mwenyekiti?? Anaejua plz aniambie/ anielimishe
 
Tume Huru ndiyo dawa yenu..uhuni uhuni hatutaki safari hii.
Hizo ni porojo tuu, tume haipigi kura wanapiga watu. Nakufahamisha hata tungepiga kura kwa kujipanga nyuma ya mgombea mtalalamika ila ukweli ni kuwa, sisi wapiga kura kwasasa hatuwaelewi.
 
Hii elimu yetu inatuangusha sana.

Huyu anaweza kuwa ni mtu mwenye digrii kabisa aliyeipata katika vyuo vyetu vikuu nchini.

Na sio ajabu yupo huko ndani ya CCM, ndio makada wategemewa watakaoisimamia hii nchi yetu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…