Mbowe ndiye anayewafanya Wajinga na siyo Spika Tulia au CCM!

Mbowe ndiye anayewafanya Wajinga na siyo Spika Tulia au CCM!

Wanasiasa (kasoro Nyerere na Magufuli) wapo pale kwa masilahi yao binafsi, siyo ya wananchi.
Aliyewapeleka hao matapeli 19 bungeni Ni Nani kama siyo Maguguli? Aliwapeleka kwa maslahi ya nani?
 
Sijui ni kitu gani kinawafanya muone Mbowe jinsi mnavyomuona kwamba ni Malaika, sasa mnaamini kabisa ule Mkutano Mlimani ulikuwa real ? Kwa nini hamuulizi maswali ?

Iweje waliofukuzwa Ubunge warudi Bungeni wakati Mbowe yuko karibu sana na Raisi Samia na hata anakwenda kumtembelea muda wowote Ikulu akiamua?

Kama ni kweli Mbowe au sijui ni baraza la chadema alinuia kuwafukuza akina Halima Mdee kwa nini warudi Bungeni bila consequences zozote ?

Aidha Mbowe amewaloga na mnashindwa kuona lolote baya analowafanyia ?

View attachment 2222595
ni kawaida kwa ccm kukumbatia mafisadi na wezi kinachoendelea bungeni ni wizi wa kodi zetu.
 
Mnataka Mheshimiwa Rais aingilie Mhimili mwingine, and you still call yourselves democratic!
Usisahau upo ulio jichimbia chini zaidi. Kifupi mhimili ni mmoja tu, mingine ni ghost.
 
Ajabu sana, Spika anasema wakina Mdee wameenda mahakamani kudai uanachama wao waliofukuzwa Chadema.

Sasa kama Spika anakiri wakina Mdee hawana chama wanachokiwakilisha bungeni, kule bungeni wapo wanafanya nini?

Hapa ni wazi kuna mchezo unaochezwa kati ya CCM na hizi taasisi zake, nasisitiza Mbowe ajitafakari na chama chake kuhusu umuhimu wa vile vikao vya maridhiano wanavyofanya ikulu.

Binafsi sioni umuhimu wa kukutana na watu wanaoendelea kuvunja sheria mbele ya macho yenu, hizi ni dharau.
Mbowe ana enda kupewa taarifa ya nini kina endelea. Chadema kwa ujumla wake imemaliza ngwe yake kwa swala la hawa wabunge, japo viongozi wa juu inaonekana wanafahamu fika nini kinaendelea.
 
Kinacholeta ugumu hapo ni kua wakiwatoa covid 19, bunge litabaki halina upinzani litakua bunge la chama kimoja, tutakosa misaada ya wahisani, hapo ndo mtaona kua uchaguzi wa 2020 jiwe lilifanya mambo ya kijinga bila kujifikilia,

cha msingi hapo chadema wakubali kama wanawatoa covid 19 basi walete majina mengine ili walau bungeni kuwemo na vyama viwili
Wakipeleka orodha mpya tayari wameutambua uchaguzi wa 2020. Wabunge wakitoka misaada itakatwa. Suruhisho: peleka case mahakamani, ipigwe kalenda mpaka 2025.
 
Mbowe na wenzie wasijidanganye kuwa watapewa katiba na tume mpya kwa njia za amani. Hili halijawezekana tangu 1992 mfumo wa chama kimoja ulipoanza. Halitawezekana hadi mwisho. CCM wanajua wanavyo "shinda" chaguzi. Hawawezi kukubali mfumo wa haki. Inabidi walazimishwe. Mbowe bado hajalijua hilo. Atasubiri sana hadi atastaafu siasa.
Mbowe anajua sana, na yupo kwa hilo. CCM ni chama dola, kinajua michezo yote.
 
Mbowe alifuata nini Ikulu tena peke yake na yakiwa yamebaki masaa machache kikao kilichowafukuza kina Mdee kufanyika?!

Ni kweli Mbowe hana maslahi ya uwepo wa kina Mdee huko Bungeni?!
Nina uhakika Mbowe ni Master mind wa haya maigizo yanayo endelea,,Muda utaongea. Anajua kila kitu, lakini anataka kuwafanya misukule wanachama wake.
 
Kama chadema wameisha peleka barua rasmi bungeni juu ya maamuzi yao ya kuwafukuza wale wabunge 19 uanachama...basi ni SPIKA ndie anawafanya Watanzania WAJINGA sio Mbowe....nguvu ya Mbowe na Chadema kuwazuia wale wabunge wasitinge Bungeni iliishia pale Mlimani City kwenye baraza kuu...na ilichobaki ni Kiongozi wa bunge kutimiza wajibu wake pindi tu akipokea taarifa rasmi ya uamuzi ule...lakini kama taarifa ya kufukuzwa uanachama haijamfikia basi wale bado ni wabunge na niwajibu wa Spika kulinda Ubunge wao...
😀kwani si Mbowe ndiye alituaminisha kuwa LOWASA fisadi.. sasa kwanini aliibuka naye kikaoni kuwa ndiye mgombea urais wa CHADEMA? Huu ni mfano rahisi, amkeni enyi wanachama wa CHADEMA
 
Tuthibitishie
Hela ya nchi ilitumikaje kuwalipa along the way wakati CDM iliwafukuza uanachama right away kipindi hicho hicho?
Magu alikuwa anajifanya kuchukua ufisadi huku akiruhusu kodi ya wananchi kutumiwa vibaya na hao wabunge batili.
 
Sijui ni kitu gani kinawafanya muone Mbowe jinsi mnavyomuona kwamba ni Malaika, sasa mnaamini kabisa ule Mkutano Mlimani ulikuwa real ? Kwa nini hamuulizi maswali ?

Iweje waliofukuzwa Ubunge warudi Bungeni wakati Mbowe yuko karibu sana na Raisi Samia na hata anakwenda kumtembelea muda wowote Ikulu akiamua?

Kama ni kweli Mbowe au sijui ni baraza la chadema alinuia kuwafukuza akina Halima Mdee kwa nini warudi Bungeni bila consequences zozote ?

Aidha Mbowe amewaloga na mnashindwa kuona lolote baya analowafanyia ?

View attachment 2222595
wew unaamini kwamba bunge linaendeshwa kwa weledi au unaandika tu kwasababu upo kwenye viunga vya lumumba hapo ukijichokoa na kunusa mwenyewe?
jibu maswali haya
sofia simba alipofukuzwa ubunge na lile dubwasha sasa marehemu nini kilifuatia hapo bungeni?
wabunge kina riziki ngwali na wenzake walipofukuzwa ubunge nini kilifuatia hapo bungeni?
mtu akiwana rufaa kama yule mpuuzi SABAYA anapaswa kuwa wapi?
wanaposema hawajasikilizwa ni kweli hawakusikilizwa pale mlimani city?
acha kutufanya wajinga kama wewe mwehu mkubwa wewe?
unatuwekea picha ya lowasa ili kiwe nn wakati lowasa na mtoto wake wapo ccm tena walipokelewa kwa shangwe kubwa
 
😀kwani si Mbowe ndiye alituaminisha kuwa LOWASA fisadi.. sasa kwanini aliibuka naye kikaoni kuwa ndiye mgombea urais wa CHADEMA? Huu ni mfano rahisi, amkeni enyi wanachama wa CHADEMA
umesahau kwamba lowasa alipelekwa lumumba na rostam azizi na akapokelewa kwa vifijo na nderemo na lile chizi lililokufa kibudu? kama unaamini kwamba lilikuwa linachukia ufisadi wa lowasa kwann halikumkamata?
 
covid 19 wanahitajika kwa sababu mbili..ule msaada wa european union WA EUROS ZA KUTOSHA BUNGENI unaohitaji idadi fulani ya wapinzani kwenye kamati zabunge wakati huo kuna watu waliiiba kupitiliza
Pili inadhaniwa kwamba hii situation italeta mgawanyiko chadema kumbe IMEWAGEUZA WATU WENYE"HESHIMA ZAO" KUWA VITUKO
 
Naona mnaogopa kutaka kujua ni nani aliyapeleka majina 19 ndani ya CDM.
 
😀kwani si Mbowe ndiye alituaminisha kuwa LOWASA fisadi.. sasa kwanini aliibuka naye kikaoni kuwa ndiye mgombea urais wa CHADEMA? Huu ni mfano rahisi, amkeni enyi wanachama wa CHADEMA
CCm wamekuaminisha mangapi na yanakuwa si kweli? umeamka au bado waisujudia CCM! na mwisho uelewe sio kila anaye support issue inayohusiana na chadema basi ni mwanachama wa Chadema! wengine sisi ni concerned citizens!
 
Hapa sio suala la kuingilia mhimili mwingine. ni kuangalia sheria zilizopo zinasema nini kuhusu wakina Mdee na wenzake mpaka muda huu.

Katiba inatamka wazi, kifungu cha 67 (1) (b) wabunge lazima wawe wanatokana na chama cha siasa ili wahalalishe uwepo wao bungeni, tofauti na wale wanaoteuliwa na Rais.

Wale kina Mdee wamefukuzwa uanachama, maana yake kule bungeni mpaka muda huu hawatokani na chama chochote, hawa wanavunja sheria kwa uwepo wao bungeni.

Spika Tulia ni mwanasheria, ina maana haoni huu uvunjifu wa sheria anaousimamia tena akiwa kama kiongozi wa chombo cha kutunga sheria? hizi ni dharau kwa watanzania.
Kwani "STOP ORDER" huko kwenye Sheria maana yake nini?
 
Wanasiasa (kasoro Nyerere na Magufuli) wapo pale kwa masilahi yao binafsi, siyo ya wananchi.
Magufuli anahusika vipi hapa?? Kama hana maslahi binafsi kwa nini aibe uchaguzi?
Mfateni kaburini aliko.
 
Back
Top Bottom