Mbowe ndiye mwanzilishi wa 'No Reforms No Election' 2024, kwanini hakuunganishwa kwenye kesi ya uhaini ya Lissu.

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,848
Reaction score
63,306
Moja ya mashitaka kwenye kesi ya uhaini ya Lissu ni kutumia kauli ya No Reforms No Election, kauli ambayo mwasisi wake ni Mbowe aliyekuwa Mkiti wa Chadema 2024.

Kwanini mahakama isimuite Mbowe aje afafanue alikuwa na maana gani badala ya kumbana Lissu peke yake atoe ufafanuzi, au kwanini hakuwa mmoja wa mashahidi wa upande wa utetezi.
 
Ngoja tusubiri tuone hukumu ya majaji wa ccm.
 
sidhani kama ni muhimu hiyo porojo gentleman 🐒
 
Nami nilifikiria hivyo, ila alichofanya Heche jana , nadhani ndicho hicho hicho ambacho hata Mbowe angefanya...Heche alielezea kwa MAPANA, Movement ya NO REFORMS NO ELECTION,nadhani amekuwa shahidi muhimu kwa Mahakama katika kufikia hukumu ya HAKI!
 

Kisheria ukikutwa na Kisu na kumetokea Mauaji ya kisu eneo usika wewe ndio muuaji✍️
 
Dalali la kisiasa hilo....
 
Nadhani kwa Mbowe kutokuwa shahidi upande wa utetezi, hilo aulizwe Lissu kwanini hakumuita. Au labda Lissu aliogopa Mzee Mbowe angemu "overshadow" mahakamani! Ahahahahaha!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…