Mbowe ni master wa siasa Tanzania tumpe pongezi

Wanaukumbi.

View attachment 2219314

Freeman Mbowe atabaki kuwa na nafasi ya Pekee sana kwenye Siasa za Upinzani hapa nchini, jina lake litaishi hata asipokuwepo. Huwa hakurupuki na haongozwi na hisia bali anapeleka mambo yake kwa akili na Mipango. Viongozi Vijana wa Upinzani wana mengi ya Kujifunza toka kwa Mbowe.
Kweli Mbowe anaweza kuongoza watu tumlinde na tumuunge mkono.
 
Mfano ni huu, Mbowe anaitwa IKULU mara ya pili - anaongea na Rais wa nchi ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, lakini kwa namna ANAVYOAMINIKA hakuna mwana CDM yeyete ambaye amedhani kwamba Mbowe alikwenda IKULU kufanya dili.

Mtaji wa mwanasiasa ni uaminifu kwa wafuasi wake na kwenye level hii Mbowe kashaipita.
Wanaogopa kuhoji ukihoji unafukuzwa chama
 
hapana, CDM ni chama chenye uwazi na ukweli daima - kwa mfano hao COVID-19 walidanganywa na mwendazake wakadanganyika - mshahara wa dhambi ni ....
 
Unaonekana ulianza mataputapu ktk umri mdogo sana kiasi kwamba akili zako zimedumaa!
Ni vyema ukajitafakari kwani unakoeleleka ni kuwa mwendawazimu!
Mlishakuwa misukule wa makengeza Mbowe mnajiona mmeshakuwa na akili kubwa kinoma.

Mmekuwa vijibwana vya ajabu ajabu sana
 
Huyu Mbowe pia ni sahihi Sasa akiachia uenyekiti wa cdm, kwani kuna sababu zote za msingi kwa yeye kupumzika sasa.
Hili umelishikilia kwa muda mrefu sana, nakumbuka.
Sina sababu tena za kutofautiana na wewe juu ya hili. Kama ndani ya CHADEMA hakuna viongozi wengine wanaoweza kukipeleka chama mbele, bali kumtegemea mtu mmoja tu, Mbowe, basi hicho siyo chama.

Ila, pengine tutatofautiana njia tu za kumpumzisha Mbowe wakati huu. Ni jukumu la wanachama kufanya uamzi huo kwa uhuru wao wenyewe, bila ya kushinikizwa na yeyote. Yaani, pawepo na uchaguzi ulio huru kufanya maamuzi hayo.
 
Wanaukumbi.

View attachment 2219314

Freeman Mbowe atabaki kuwa na nafasi ya Pekee sana kwenye Siasa za Upinzani hapa nchini, jina lake litaishi hata asipokuwepo. Huwa hakurupuki na haongozwi na hisia bali anapeleka mambo yake kwa akili na Mipango. Viongozi Vijana wa Upinzani wana mengi ya Kujifunza toka kwa Mbowe.
Kwahiyo viongozi wasio wa upinzani hawana cha kuiga?
HEBU KOLEZA WINO KWENYE KICHWA CHA POST YAKO.
 
Hili umelishikilia kwa muda mrefu sana, nakumbuka.
Sina sababu tena za kutofautiana na wewe juu ya hili. Kama ndani ya CHADEMA hakuna viongozi wengine wanaoweza kukipeleka chama mbele, bali kumtegemea mtu mmoja tu, Mbowe, basi hicho siyo chama.

Ila, pengine tutatofautiana njia tu za kumpumzisha Mbowe wakati huu. Ni jukumu la wanachama kufanya uamzi huo kwa uhuru wao wenyewe, bila ya kushinikizwa na yeyote. Yaani, pawepo na uchaguzi ulio huru kufanya maamuzi hayo.

Nilisema kitu ninachokifahamu na mifano nimekuwa nikitoa. Kiongozi yoyote yule wa kuchaguliwa mwisho wa ubora wake ni miaka kumi kwenye nafasi moja. Hapo niliwataja kina Nyerere, Moi, Mugabe, Gaddaf, Elbashir, Mubarack nk. Wote hao waangalie walifanya vyema ndani ya miaka 10, baada ya hapo walianza kulazimisha mitazamo yao. Finaly waliishia kuharibu hata mazuri yao waliyofanya.

Mifano ya hao watu ndio naiona wazi kwa Mbowe, kama kweli Mbowe alitaka mazuri yake yabaki ni iwapo angejiuzulu baada ya ile blunder ya kumleta Lowassa. Au kama bado aliona anastahili, basi siku Lowassa anarejea ccm, naye angestep down. Tuchukulie bado hakuona tatizo yeye kuendelea baada ya Lowassa kurejea ccm. Basi uchaguzi uliopita hakupaswa tena kugombea. Kwa sasa naona wazi Mbowe akipigiwa na serikali jinsi ya kufanya siasa za kushindana na ccm. Kwasababu hiyo ndio maana unaona anaenda kwenye vikao ikulu mwenyewe kupewa maagizo, kisha anakuja kuagiza watu namna ya kufanya siasa kwa mtazamo wa dola/ccm. Aina Hii ya sasa ya siasa za Mbowe ndio tumekuwa tukizikataa toka kwa kina Mrema, Cheyo, Lipumba nk. Na Mbowe sasa naye anaelekea huko kwani umri wa mapambano umetoka, na bado analazimisha kuongoza mapambano.
 
Mifano ya hao watu ndio naiona wazi kwa Mbowe, kama kweli Mbowe alitaka mazuri yake yabaki ni iwapo angejiuzulu baada ya ile blunder ya kumleta Lowassa. Au kama bado aliona anastahili, basi siku Lowassa anarejea ccm, naye angestep down
Wakati huu CHADEMA ungekuwa unaisoma kwenye historia.

Sikubaliani nawe kamwe kwenye dhana yako hiyo 'arbitrary' ya miaka kumi, kwani haina msingi wowote wa uthibitisho, na wala haitilii maanani mazingira yanayokuwepo katika muda wa uongozi.
 
Sikulazimishi popote ukubaliane na Hii dhana yangu maana hiyo ndio afya ya mjadala, ila sina shaka na Hii dhana yangu, na mifano nimekutajia ya viongozi waliokaa madarakani muda mrefu, na hatima ya tawala zao. Kama kukaa madarakani chini ya miaka 10, kwa mwenyekiti ingekuwa sababu ya kufa cdm, basi wenyeviti wengine walitangulia ambao hawakukaa zaidi ya miaka 10, Mbowe asingeikuta cdm.
 
Nilipojibu, nilitazama mifano hiyo hiyo na kuona kuwa dhana yako haina uhalali juu ya wote, ndiyo maana nikakuwekea na umuhimu wa mazingira, kama huo ambao uliihusu CHADEMA na uwepo wa Mbowe. Naona hili hukulipata.
 
Labda nimguse Nyerere maana ww ni muumini wake, alifanya vizuri kuanzia 1965-1978 kabla ya vita vya Ihanda, kufika 1980 alikuwa ana zaidi ya miaka 15 madarakani, nadhani unafahamu wananchi walifikia mahali wakawa wanavaa viraka. Mugabe alifanya vizuri ndani ya miaka 10 ya mwanzo ya utawala wake, baada ya hapo Wazimbabwe waligeuka wakawa masikini wa kujitakia.
 
Hapo ndipo unapokosea na dhana yako hiyo. "Watu kuvaa viraka" alisababisha Nyerere? Kwani kabla ya hapo watu walikuwa hawavai viraka, au hata baada ya yeye viraka havivaliwi?
Na wala mazingira kwako hayana maana yoyote? Unaelewa uchumi wa dunia ulikuwa vipi? Katani/mkonge zao lililotegemewa, hujui dhoruba iliyolikumba? Tanganyika packers kutouza nyama ulaya, yalikuwa makosa ya Nyerere? Mafuta duniani kuwa ya shida ilikuwa ni matatizo aliyosababisha Nyerere?
 
Viraka viliisha baada ya Salim Ahmed Salim kuruhusu mitumba. Dhoruba lilitupatapa kutokana na siasa za ujamaa za Nyerere na hasa misimamo yake. Mbona Kenya hapo waliendelea sawa hadi kuwa wanatuuzia na bidhaa nyingi za viwandani?
 
Kenya ni koloni. Uchumi wao uliendelea kuendeshwa na wakoloni hadi leo. Lakini pamoja na kuwa hivyo, hata wao dhoruba ya mtikisiko wa uchumi iliwaathiri.
 
Mbowe ana sifa zote za kuwa Kiongozi wa Upinzani

Mbowe ni muumini wa Siasa za kistaarbu
Ukiwauliza CCM Ile kesi yao ya Ugaidi hewa dhidi ya Mbowe imekuwaje wamebaki kukenua meno tuu.
Mbowe ni muhimili kamili wa nne wa upinzani hapa nchini upende usipende.Mbowe ni mwanadamu anayo mapungufu yake lakini kwa namna alivyo ongoza upinzani nchini chini ya dhalimu aliyeko kuzimu kila mwenye Akili timamu atampa pongezi.
 
Kenya ni koloni. Uchumi wao uliendelea kuendeshwa na wakoloni hadi leo. Lakini pamoja na kuwa hivyo, hata wao dhoruba ya mtikisiko wa uchumi iliwaathiri.

Bora wao ni koloni kuliko sisi wenye uhuru wa bendera. Na wao mtikisiko uliwaathiri wakawa wanapiga mswaki na chumvi, kufulia na majani ya papai, huku wakisimama misururu mirefu kwa mabalozi kununua matumizi ya nyumbani kama sukari, sabuni mafuta ya kula nk?
 
Back
Top Bottom