Pre GE2025 Mbowe: Nimeanzisha CHADEMA nikiwa kijana mdogo wa miaka 30

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA, amesema alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa chama hicho akiwa na umri wa miaka 30. Akizungumza kupitia Clouds FM, amesema;

"Mimi nilikuwa miongoni kwa waanzilishi wa CHADEMA. Kipindi hicho nilikuwa mdogo sana kati ya watu 10 tulioanzisha Chama hiki. Nilikuwa na umri wa miaka 30.

"Nilikuwa nafanya biashara na familia yetu ilikuwa ya Wafanyabiashara na Mzee wangu baada ya vuguvugu la Uhuru alikuwa kwenye siasa aligombea ubunge 1965 alikuwa rafiki wa karibu na Mwl Julius Nyerere. Sisi familia yetu ilikuwa ikifanya biashara kabla ya uhuru wa nchi yetu.


"Niliingia kwenye siasa nikawa nafanya vyote, siasa na Biashara" - Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA

Your browser is not able to display this video.

FREEMAN MBOWE: ACHA INYESHE TUJUE PANAPOVUJA
Akizungumza katika mahojiano na Clouds FM, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kuelekea Uchaguzi wa Chama hicho amesema β€œWatoto wa Mjini wanasema acha inyeshe tujue panapovuja”

Soma, Pia:
β€’ Mbowe arudisha fomu ya kugombea Uenyekiti CHADEMA
β€’ Ezekia Wenje: Msimshangae Mbowe, mbona Nyerere alikaa Madarakani muda mrefu zaidi
β€’ Lissu ataka Ukomo wa Madaraka kwenye nafasi za uongozi CHADEMA. Asema itapunguza 'Uchawa'
 
miaka 30 ni kijana mdogo? hivi kwa nini watanzagiza wanapenda sana kujiita vijana hata kama ni watu wazima? kijana mwisho miaka 19 hapo ndiyo u teeneger unaisha na kuanzia hapo ni mtu mzima ambaye anakuwa held responsible for his actions …
 
Ni sahihi kabisa lakini mwamba huu ni wakati wa kupumzika na kuwapisha wengine
 
Mwanzilishi wa Chadema anagombea cheo chake.
Team Lissu Γ nzisheni Chadema yenu.
 
Miaka 30 tena wa enzi zile ni mdogo? Is he serious?
 
1. Kwa biyo kama nimuasisisi alianzisha chama cha familia?
2. Je chadema sio taasisi?
3. Hajataja aina ya biashara?

Na sisi tunajivunia Mugabe wetu.
 
Miaka 30 ni kijana mdogo aisee..OK sawa waachie wengine waongoze kuanzisha chama cha siasa haimaanishi kuwa ni mali yako..
 
Kwahiyo anataka kumaanisha kwamba ni chama chake binafsi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…