Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA, amesema alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa chama hicho akiwa na umri wa miaka 30. Akizungumza kupitia Clouds FM, amesema;
"Mimi nilikuwa miongoni kwa waanzilishi wa CHADEMA. Kipindi hicho nilikuwa mdogo sana kati ya watu 10 tulioanzisha Chama hiki. Nilikuwa na umri wa miaka 30.
"Nilikuwa nafanya biashara na familia yetu ilikuwa ya Wafanyabiashara na Mzee wangu baada ya vuguvugu la Uhuru alikuwa kwenye siasa aligombea ubunge 1965 alikuwa rafiki wa karibu na Mwl Julius Nyerere. Sisi familia yetu ilikuwa ikifanya biashara kabla ya uhuru wa nchi yetu.
"Niliingia kwenye siasa nikawa nafanya vyote, siasa na Biashara" - Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA
Soma, Pia:
• Mbowe arudisha fomu ya kugombea Uenyekiti CHADEMA
• Ezekia Wenje: Msimshangae Mbowe, mbona Nyerere alikaa Madarakani muda mrefu zaidi
• Lissu ataka Ukomo wa Madaraka kwenye nafasi za uongozi CHADEMA. Asema itapunguza 'Uchawa'
So what? Achia ngazi tu mzee mbowe, umeshachokwa