Naona mbowe anadema yeye ndio anapigania mabadiliko na demokrasia nchini. Mbowe anataka mabadiliko ya kimfumo, ccm waondoke madarakani wamekaa muda mrefu, demokrasia, katiba mpya inayotoa ukomo wa madaraka lakini yeye ndani ya Chadema hivyo vitu hakuna.
Chadema ilikua na ukomo wa madaraka kwenye katiba yeye akaondoa, anasema ccm imekaa muda mrefu madarakani inabidi itoke ila yeye hataki kutoka chadema, yeye ni mwenyekiti wa maisha.
Anasema atailinda chadema kwa gharama zote ila ukweli unabaki kwamba chadema ni saccos yake, lazima ailinde na hawezi kuruhusu saccos yake ichukuliwe na watu wengine.
View: https://x.com/CrownMediaTZ/status/1875240469359153653?s=19