benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amewataka wananchi kutanguliza uzalendo kwa taifa lao na kuweka mbele zaidi mshikamano kitaifa Badala ya kukumbatia vyarna vya siasa vinavyowagawa na kuwafanya waendelee kuwa maskini huku viongozi wachache wakinufaika na mapato ya rasilimali za nchi.
Alitoa kauli hiyo juzi, wakati akihutubia Wananchi mjini Mugumu wilayani Serengeti, mkoani Mara kuwa wakati umefika kuwataka wananchi kuwa kitu kimoja bila kujali itikadi za vyama vyao.
Aidha, suala la kudai Katiba mpya itakayojali haki, uhuru, usawa na demokrasia kwa watu wote litafanikiwa endapo wananchi watapaza sauti zao bila kujali itikadi za vyama vyao ili kupata itakayoharakisha maendeleo kwa wote.
Alisema ameshaongea na Rais Samia Suluhu na kumweleza kuwa nchi inakokwenda siko na kwamba ukombozi pekee wa Watanzania ni Katiba mpya.
Alibainisha kuwa Katiba iliyopo itaendelea kuwalinda wakubwa waendelee kutenda wanayotaka wao, lakini haimsaidii mwananchi mwingine kustawi ki-jamil, kisiasa na kiuchumi.
"Katika hili tuungane paroja tuache itikadi za kisiasa turekebishe Katiba kwa ushirikiano mkubwa ili tuokoe Jamil yetu," alisema.