Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema iwapo atachaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho, ataunda tume ya ukweli na upatanishi.
Amesema katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho kuanzia ngazi za chini hadi wa taifa, utakaohitimishwa Jumanne ya Januari 21, 2025, kumetokea mnyukano mwingi unaohitaji kupata mapatano.
Mbowe amesema hayo leo Ijumaa, Januari 17, 2025, katika mahojiano maalumu na wahariri na waandishi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Tabata, jijini Dar es Salaam.
"Tukimaliza uchaguzi, tutafuata utaratibu unaofanyika duniani kote kutengeneza mapatano na kutibu majeraha ya uchaguzi.
"Kutengeneza tume ya ukweli na upatanishi kwa sababu watu wamekanyagana sana. Watu wameumizana sana. Nikichaguliwa, tutaitana na kuzungumza kwani tunahitajiana wote," amesema Mbowe.
Pia, Soma: