Mbowe: Nitaunda tume ya ukweli na upatanishi nikishinda Uenyekiti

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema iwapo atachaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho, ataunda tume ya ukweli na upatanishi.

Amesema katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho kuanzia ngazi za chini hadi wa taifa, utakaohitimishwa Jumanne ya Januari 21, 2025, kumetokea mnyukano mwingi unaohitaji kupata mapatano.

Mbowe amesema hayo leo Ijumaa, Januari 17, 2025, katika mahojiano maalumu na wahariri na waandishi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Tabata, jijini Dar es Salaam.

"Tukimaliza uchaguzi, tutafuata utaratibu unaofanyika duniani kote kutengeneza mapatano na kutibu majeraha ya uchaguzi.

"Kutengeneza tume ya ukweli na upatanishi kwa sababu watu wamekanyagana sana. Watu wameumizana sana. Nikichaguliwa, tutaitana na kuzungumza kwani tunahitajiana wote," amesema Mbowe.
Pia, Soma:
Utakuwa na tofauti na na four ARAS au ndio yale yale hadi leo wapo waliotelekezwa njia panda?
 
Tume ya upatanishi ya nn we Mzee? Acha kutufanya mafala, umeshindwa kupambana tupate tume huru ya uchaguzi unatuambia tume ya upatanishi! Itusaidie nn sisi wananchi wa chini? Tooooka
 
Nakutoka kwenywe ni kwa ushirika na wamachukua chako mapema
 
"Kutengeneza tume ya ukweli na upatanishi kwa sababu watu wamekanyagana sana. Watu wameumizana sana. Nikichaguliwa, tutaitana na kuzungumza kwani tunahitajiana wote," amesema Mbowe.
Na asipochaguliwa je?
 
Sijasoma yote lakini mambo ya kuunda tume ni ya kijinga sana maana binafsi sijawahi ona faida ya hayo matume labda ile ya kina Harrison Mwakyembe kipindi kile cha Richmond.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema iwapo atachaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho, ataunda tume ya ukweli na upatanishi.

Amesema katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho kuanzia ngazi za chini hadi wa taifa, utakaohitimishwa Jumanne ya Januari 21, 2025, kumetokea mnyukano mwingi unaohitaji kupata mapatano.

Mbowe amesema hayo leo Ijumaa, Januari 17, 2025, katika mahojiano maalumu na wahariri na waandishi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Tabata, jijini Dar es Salaam.

"Tukimaliza uchaguzi, tutafuata utaratibu unaofanyika duniani kote kutengeneza mapatano na kutibu majeraha ya uchaguzi.

"Kutengeneza tume ya ukweli na upatanishi kwa sababu watu wamekanyagana sana. Watu wameumizana sana. Nikichaguliwa, tutaitana na kuzungumza kwani tunahitajiana wote," amesema Mbowe.
Pia, Soma:
 
Huyu janja janja nyingi hapo anatafuta sympathy votes..miaka21 kipi hujafanya hadi uongezwe 5 mingine?
 
Back
Top Bottom