Mbowe: Rais, wanaopinga ushiriki wa Taifa kwenye vita ya Corona wanawaza uchaguzi na huruma yako ktk uteuzi. Ukweli lawama zote zitakuangukia wewe

Mbowe: Rais, wanaopinga ushiriki wa Taifa kwenye vita ya Corona wanawaza uchaguzi na huruma yako ktk uteuzi. Ukweli lawama zote zitakuangukia wewe

Narudia mara kwa mara, tunapenda kusikia takwimu za maambukizi na vifo kutokana na COVID-19 kutoka Serikalini, lakini humu JF, kama wewe, husemi idadi ya walioambukizwa au vifo nyumbani kwako, jirani, mtaani, rafiki au ndugu zako? Hayo maambukizi na vifo viko wapi?
ninawafahamu madaktari 5 walioambukizwa corona kutokana na vifaa duni wanavyotumia wanapowahudumia wagonjwa wa corona , wawili wako kwenye oxygen hivi ninavyoandika hapa
 
Hivi Mbowe hana washauri wamshauri kwamba hili la corona raia wamesimama na rais Magu?

Au nyie chadema mambo yenu mnafanyia utafiti wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Inawezekana sisi chadema hatujui,pia inawezekana wawemba(wazambia)hawajui,pia inawezekana,wajaluo na wakamba(wakenya)pia inawezekana,wa turuki wanaohamisha raia zao hawajui,pia inawezekana hata balozi ya marekani iliyowaasa raia wake waliopo tz wajichunge haijui,pia hata wataalamu wa WHO nao hawajui,si hao tu pia hata wataalamu wetu wa maabara na msd waliosimamishwa hawajui,si hao tu ha aliyekuwa naibu waziri wa afya aliyepinga kujifukiza kitaalamu hajui (wakati mtoto wa rais kapona)bali wapambe wachache wa lumumba ndio wanajua,,ok wanaojua na wasiojua wote tu wahanga wa hili janga,muda unaosema utaendelea kusema

Sent from my ALE-L21 using JamiiForums mobile app
 
Watu wengi wanaomponda Rais na Serikali humu ni wale waliokua wakiwaibia wananchi na sasa wameminywa, Mbowe ni muhuni fulani na wala siwezi kumuita muheshimiwa hata siku moja. haihitaji elimu kumuelewa Rais wetu kua na kichwa chenye mawazo pevu sana,iwapo Africa tungekua na maRais kama JPM wasiopungua 40 hivi, Makaburu yangenyoosha mikono juu

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
Mkuu umerudi lini kutoka Geita ?
 
anzia kwenye ukoo wako kupata hizo takwimu au na ukoo wako mnafichana ? vipi kwenye ukoo wenu mna takwimu rasmi ya idadi ya waliopona, waliofariki na rate ya maambukizi imepungua au imeongezeka kwa kiasi gani.?
hebu zimwage hapa hizo hazihitaji serikali tupe wewe
Kwa hiyo kila mtu atoe takwimu za ukoo wake sio?!
Sasa nini maana ya kuwa na Serikali
 
Kwa kweli wametuacha dilemma, halafu wafanya mambo kimya kimya sasa hivi nasikia wanataka kufungua mashule.

Hapo ndio unashindwa hata kuelewa.
Wanatuambia wagonjwa wamepungua ila takwimu wamezikalia. Wanachoficha ni nini hasa?!
 
Hivi Mbowe hana washauri wamshauri kwamba hili la corona raia wamesimama na rais Magu?

Au nyie chadema mambo yenu mnafanyia utafiti wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio wananchi Sena wewe na wenzio, ila kanifutahisha katoa data kwenye koti za wagonjwa! Wanapungua japo upimaji hamna! Hahaha sasa hapo sijui tuseme wanapungua au?
 

HOTUBA YA MBUNGE FREEMAN MBOWE KWA UFUPI

Nimezungumza na Rais kwenye simu nimemuambia tafadhali shirikisha Jamii pana ya Watanzania ili jambo tulibebe wote, huu ni msiba na msiba haachiwi Mtu mmoja, kwa nia njema kabisa, tushirikiane kwa pamoja kwenye mapambano haya dhidi ya virusi vya corona.

Mhe. Rais unafiki haujawahi kuliacha taifa lolote salama, usikae wakati wote ukafikiri sisi ambao tunajaribu kukushauri, kuikosoa Serikali yako na kuilekeza, eti tuna nia mbaya au nongwa na wewe, hapana! , tunafanya hivi kwa nia njema na mapenzi sana kwa nchi yetu."

Mhe. Rais lawama zote za janga la Corona zitakuangukia wewe, huu ni ukweli wa Mungu na mimi kama Mbowe, mtu mdogo sana katika nchi yetu, nikwambie Rais wangu, wanaopinga ushirika wa taifa katika vita hii wanawaza uchaguzi na kuomba huruma yako katika uteuzi.

Nasikitika kwa niaba ya CHADEMA kwa namna ushauri wetu wa kuwataka Wabunge wajiweke karantini ulivyopokelewa vibaya na kuonekana tunashindana, Spika ametumia majukwaa mbalimbali kunishambulia na kuninidhalilisha mimina Viongozi wenzangu bila kuiona nia yetu njema.

Spika kila akitaka kuahirisha Bunge lazima apande na Mbowe, tumekutana Bungeni na Spika miaka 20 iliyopita sijawahi kumvunjia heshima hadharani wala sirini, nimesoma Kibaha na Spika amesoma pale ni mwanafunzi mwenzangu wa shule moja, namuheshimu,naliomba Taifa kumuombea.

Tuligoma lockdown tukashindwa hata kufanya partial lockdown na tukaruhusu ugonjwa kuenea na kuua wapendwa wetu, tulidhani tunalinda uchumi wetu na kusahau uhai wa watu wetu, sasa Corona inaendelea kutula wote, inakula uchumi wetu tupende tusipende.

Namshukuru Mungu kwa sasa Mwanangu ambaye alikuwa mgonjwa wa corona hatimaye amepona baada ya kukaa karantini kwa siku 57 nina uhakika amejifunza mengi, Familia nayo imejifunza mengi, nawashukuru Madaktari na wahudumu wengine

Kufuatia kikao hiki, Kamati Kuu imejadili kwa kina, miongoni mwa agenda mbalimbali, Janga la Corona na athari zake kwa taifa letu, mataifa ya jirani na dunia nzima katika ujumla wake.

Kamati Kuu,ilijiridhisha kuwa janga hili halihitaji masihara, mzaha wala usiri katika kulikabili.Ilitambua kwa mara nyingine umuhimu wa kuweka tofaui zetu pembeni na kutoruhusu chuki za kisiasa, hodhi za kisiasa, kiburi cha madaraka na mamlaka katika kupambana na vita hii.

Mwisho
Screenshot_2020-05-17-23-00-42.jpeg
 
Ndugu yangu mimi nimesoma ud nimemaliza 2006 lecture theatre hua tunajaa kuliko darsa la form one. Nakumbuka wakati mwengine ukichelewa ht kuingia huez.

Pili katika hostel zero distancing is equal to zero. Jamani tuwe na utu na tufikirie wengine pia
 
Nimejaribu kujizuia nimeshindwa.

Tanzania inaenda kuangamia kwa kukosa maarifa.

nilikuwa nasubiri nipewe ripoti ya mashine za kupimia ambapo kila takwimu zilizokuwa zinatoka ugonjwa ulikuwa unaongezeka maradufu.

tujiulize km wagonjwa wamepungua je tulipima wangapi na kwa mashine zipi?

Tunaomba viongozi watuambie sisi wananchi je ripoti ya ukaguzi ya mashine imetoka?

na wakaanza kupima tena lini?

najiuliza sipati majib pale mashabiki watakapojazana viwanjani, wanafunzi maskulini na wageni kuingia bila karantini hii ni jambo la kustia mno.


salaam.
Wiki kesho tunaweza kufungua vyuo na shule, wewe unatuleta corona tena wakati INAISHIA! Kila mmoja ataguswa kwa wakati wake
nyie mtaongea sana aisee ..

Sent using Jamii Forums mobile app
hawaruhusu kama unavyofikiria wewe kuna utaratibu maalum utakao zingatiwa wa kitaalam utakaofatwa.
corona haishi leo wala kesho ni lazima maisha yaendelee huku kukiwa na tahadhari kubwa.

magufuli anaanzisha ila hamini nakwambia kuna nchi nyingi tu zita fuata,


Sent using Jamii Forums mobile app
Toka mwezi uliopitia huo ndiyo wimbo kwa hiyo hata hii ndoto yako ni sawa na ya alinacha.Endelea kuota bado giza.
Pole kwa kukutana na hawa watu wasiojali uhai wa watu. Corona imeonesha jinsi watanzania wengi walivyo na fikra za kienyeji kuanzia mkuu hadi hawa wafia-jiwe. Tunapaswa kuweka uhai mbele na sio ushabiki wa kisiasa.
 
Wiki kesho tunaweza kufungua vyuo na shule, wewe unatuleta corona tena wakati INAISHIA! Kila mmoja ataguswa kwa wakati wake
Dada kule chato kanigwa na kaugonjwa.
 
Pole kwa kukutana na hawa watu wasiojali uhai wa watu. Corona imeonesha jinsi watanzania wengi walivyo na fikra za kienyeji kuanzia mkuu hadi hawa wafia-jiwe. Tunapaswa kuweka uhai mbele na sio ushabiki wa kisiasa.
Kaugonjwa kamembeba dada huko chato.
 
Back
Top Bottom