Mbowe: Tozo ya Matangazo kwenye Facebook itawapunguzia Vijana Kipato na Fursa za Kujiajiri

Nchi nyingi zenye Serikali zinazoongozwa na wanaojitambua, hawatozi kodi yoyote kwa biashara ndogo. Lengo ni kuwapa nafasi wafanyabiashara hao wakue, na wakishakua watatozwa kodi.

Lakini hapa kwetu, kabla hajainuka anadidimizwa kwa kodi, na kufia hapo hapo. Ndiyo maana ongezeko la mitaji kwa nchi hizi zinazoongozwa na watu wasio na upeo wa kouchumi, ukuaji wa mitaji kwa wajasiriamali ni duni sana au haupo kabisa. Wachache wanaotoboa, ni wale wanaoamua kuweka maadili ya biashara pembeni, na hivyo kujitahidi kukwepa kpdi kwa mbinu zote.

Hakuna mjasiriamali wa Tanzania anayelipa kodi zote kama zilivyoorodheshwa, na tozo zote, halafu akafanikiwa kuikuza biashara na mtaji wake.

Mbaya zaidi, hiyo kodi ambayo anakabwa mtu mwenye kipato duni, kiasi kikubwa inaenda kwenye matumizi ya anasa ya watawala.
 
Nchi nyingi zenye Serikali zinazoongozwa na wanaojitambua, hawatozi kodi yoyote kwa biashara ndogo. Lengo ni kuwapa nafasi wafanyabiashara hao wakue, na wakishakua watatozwa kodi.

Lakini hapa kwetu, kabla hajainuka anadidimizwa kwa kodi, na kufia hapo hapo. Ndiyo maana ongezeko la mitaji kwa nchi hizi zinazoongozwa na watu wasio na upeo wa kouchumi, ukuaji wa mitaji kwa wajasiriamali ni duni sana au haupo kabisa. Wachache wanaotoboa, ni wale wanaoamua kuweka maadili ya biashara pembeni, na hivyo kujitahidi kukwepa kpdi kwa mbinu zote.

Hakuna mjasiriamali wa Tanzania anayelipa kodi zote kama zilivyoorodheshwa, na tozo zote, halafu akafanikiwa kuikuza biashara na mtaji wake.
 
Kutoza kodi hiyo mitandao ni jambo zuri. Hata hivyo 2% ni kodi fair sana.
 
Pesa unayotumia kuboost ads facebook inaenda moja kwa moja kwa mmiliki sasa sijui wao serikali hii kodi wataikusanyaje
Mfano watanzania wote waache kutangaza #Facebook wao watafanyaje sasa
 
Huyu mzee ni mjinga sana asisee,uliona wapi bishara isiyotozwa kodi?
 
Bado hatujasema na tutasema yaan mpaka tuseme 😂😂😂
 
Kinachoudhi hizi kodi zinenda kuchezewa na kufadhili kampeni za ccm
 
Binafsi ninamuunga mkono 100%. Serikali iwezeshe kwanza hii biashara ikue ndo ianze kukusanya kodi. Mwigulu na wenzako mjitathmini. Mbowe kaandika hivi:

Kwa mtu aliyejielimisha kuhusu mabadiliko ya nne ya viwanda duniani, ataelewa kuwa Tanzania mabadiliko haya yanaanza na biashara ndogo zinazoanza mitandaoni na hukomaa na kuingia kwenye mifumo rasmi baadae. Inahusisha pia wasio kwenye mtandao. Muuza mitumba anayetafuta elfu mbili au tatu anatarajia kufungua maduka siku moja, anatumia mitandao kutangaza na kutafuta wateja; dalali wa nyumba na viwanja, wauza simu na electronics mfano ac , frigid, makochi yaliyotumika nk, wauza nguo na vitambaa, wauza chakula, siwezi kuwataja wote hapa ila itoshe kuwa mtandao ni Ulimwengu halali uliopo na biashara inashamiri. Hii ni hatua ya kwanza kuelekea urasimishaji wa biashara.

Serikali inayotoa 'grace period ' ya kodi kwa makampuni yenye mitaji ya mabilioni ndiyo serikali hiyo hiyo imegoma kuwapatia wananchi wake ahueni kwaajili ya ujinga tu. Vijana wengi ambao wamejiajiri kupitia mitandao ya kijamii, kuwatoza Kodi kwa matangazo madogo wanavyofanya kutafuta wateja ni kung'oa mizizi ya biashara ambazo ndio kwanza zinachipukia.

Serikali hii inaendelea kujaza kodi kila sehemu huku ikishindwa kwa kiwango cha kutisha kuibiwa na kufanya anasa nyingi kwa kodi ambazo Watanzania wamelipa kwa jasho na damu na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali amethibitisha kwa miaka mingi. Kila upenyo unaoweza kuwa na manufaa kwa mwananchi wa kawaida kwao ni chanzo cha tozo na kodi, ndio maana ni ngumu kwa kijana kutoboa kwa jitihada zenu binafsi.

Mungu atutangulie.

Freeman Aikael Mbowe
Hai, Kilimanjaro, Tanzania
 
Mbowe ana uelewa mpana wa Dunia ya Kisasa inavyokwenda wakati Wote

Kwa kifupi Freeman hana " Ushamba" kama walivyo Wanasiasa wengi
 
Kuna voice note ya Mbowe na Wema inasambaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…