Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kwa mujibu wa katiba ya chama hicho uchaguzi kila baada ya miaka mitano ndio ukomo wa madaraka.
Mbowe aliyeiongoza Chadema kwa miaka 20 tangu 2004, ameyasema hayo jana Desemba 3, 2025 katika mahojiano na Crown Media jijini Dar es Salaam.
“Katika demokrasia una haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Sasa inawezekana wewe humtaki Mbowe, au mko 10 msiomtaka Mbowe, lakini wako 100 wanamtaka Mbowe, sasa hao 100 haki yao mnaipeleka wapi?
“Ndio sababu kwenye mfumo wa demokrasia kuna uchaguzi unafanyika kila baada ya miaka mitano, ule ni ukomo wa madaraka,” amesema.
Amesema kila chama kina mfumo wake, “Sisi katika chama chetu cha Chadema, hakuna ukomo wa madaraka, ACT wana ‘term limit’ usitulazimishe tuwe kama ACT ndio useme demokrasia, au usitulazimishe kuwa kama CCM.”
Amesisitiza kuwa katiba ya chama hicho imeeleza namna ya kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya kwenye ya katiba lakini hakuna mwanachama au kiongozi yeyote aliyewasilisha mapendekezo kuhusu suala hilo.
PIA SOMA
- Mbowe: Mimi sijachoka, ukomo wa madaraka ni watu wanaokutaka au kukukataa