Pre GE2025 Mbowe: Uchaguzi kila baada ya miaka mitano ndiyo uomo wa madaraka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kwa mujibu wa katiba ya chama hicho uchaguzi kila baada ya miaka mitano ndio ukomo wa madaraka.

Mbowe aliyeiongoza Chadema kwa miaka 20 tangu 2004, ameyasema hayo jana Desemba 3, 2025 katika mahojiano na Crown Media jijini Dar es Salaam.

“Katika demokrasia una haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Sasa inawezekana wewe humtaki Mbowe, au mko 10 msiomtaka Mbowe, lakini wako 100 wanamtaka Mbowe, sasa hao 100 haki yao mnaipeleka wapi?

“Ndio sababu kwenye mfumo wa demokrasia kuna uchaguzi unafanyika kila baada ya miaka mitano, ule ni ukomo wa madaraka,” amesema.

Amesema kila chama kina mfumo wake, “Sisi katika chama chetu cha Chadema, hakuna ukomo wa madaraka, ACT wana ‘term limit’ usitulazimishe tuwe kama ACT ndio useme demokrasia, au usitulazimishe kuwa kama CCM.”

Amesisitiza kuwa katiba ya chama hicho imeeleza namna ya kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya kwenye ya katiba lakini hakuna mwanachama au kiongozi yeyote aliyewasilisha mapendekezo kuhusu suala hilo.

PIA SOMA
- Mbowe: Mimi sijachoka, ukomo wa madaraka ni watu wanaokutaka au kukukataa
 
Huyu ameshakuwa kichaa sasa, kwa maana hiyo hata Rais aliyeko madarakani ukomo wake ni miaka mitano baada ya hapo anaweza kuendelea hata baada ya mihula miwili?

Mbowe katudhalilisha sana tuliomuamini na kuiamini CHADEMA kama chama mbadala, ameifuta legacy yake mwenyewe.
 
A good dancer must know when to leave the stage, Mbowe amekuwa Statesman Na Mentor Mkubwa sana for past 20 yrs ila sasa hii kungangania Top position ya Chama inaenda Kuruin Legacy yake
Kukaa Pembeni ni Busara Sana Sana
 
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kwa mujibu wa katiba ya chama hicho uchaguzi kila baada ya miaka mitano ndio ukomo wa madaraka.

Mbowe aliyeiongoza Chadema kwa miaka 20 tangu 2004, ameyasema hayo jana Desemba 3, 2025 katika mahojiano na Crown Media jijini Dar es Salaam.

“Katika demokrasia una haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Sasa inawezekana wewe humtaki Mbowe, au mko 10 msiomtaka Mbowe, lakini wako 100 wanamtaka Mbowe, sasa hao 100 haki yao mnaipeleka wapi?

“Ndio sababu kwenye mfumo wa demokrasia kuna uchaguzi unafanyika kila baada ya miaka mitano, ule ni ukomo wa madaraka,” amesema.

Amesema kila chama kina mfumo wake, “Sisi katika chama chetu cha Chadema, hakuna ukomo wa madaraka, ACT wana ‘term limit’ usitulazimishe tuwe kama ACT ndio useme demokrasia, au usitulazimishe kuwa kama CCM.”

Amesisitiza kuwa katiba ya chama hicho imeeleza namna ya kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya kwenye ya katiba lakini hakuna mwanachama au kiongozi yeyote aliyewasilisha mapendekezo kuhusu suala hilo.

PIA SOMA
- Mbowe: Mimi sijachoka, ukomo wa madaraka ni watu wanaokutaka au kukukataa

GgZdpxUWMAAT6EU.jpeg

Aka, Mheshimiwa Mungu asema Yeriko.
 
Huyu ameshakuwa kichaa sasa, kwa maana hiyo hata Rais aliyeko madarakani ukomo wake ni miaka mitano baada ya hapo anaweza kuendelea hata baada ya mihula miwili?

Mbowe katudhalilisha sana tuliomuamini na kuiamini CHADEMA kama chama mbadala, ameifuta legacy yake mwenyewe.
Umbeya na siasa wapi wapi?Alichozungumzia Mbowe ni ukomo kwenye Katiba ya Chadema.Kwamba unakuwa kiongozi kwa muda wa miaka 5.Baada ya hapo unakuwa na haki ya kikatiba kugombea tena.
Hakuzungumzia ukomo wa vipindi viwili ambayo ndio hoja yako unayoilinganisha na Urais wa Nchi.
Kujidai unaiamini Chadema haitoshi soma na katiba ya Chadema uielewe.
Kichaa hapa sio Mbowe.
 
Huyu jamaa ameshaingia tayari kwenye kundi la akina Lipumba, Mrema, Cheyo, nk. Kiufupi hana tofauti nao hata kidogo.
 
Back
Top Bottom