Mbowe umesamehewa na Rais, nawe wasamehe Mdee na wenzake 18

Mahakama imeingiliwa? Afu unasema dpp alipokea maelekezo (can you prove it?) ,Usiishi kwa hear sayings ,huo ni utoto.
 
Wewe lazima ni ccm mnaohangaika kuwaweka KIKULACHO wenu ndani ya Chadema ili mkisambaratishe chama!! Kama mnawapenda sana wachukueni muwe nao.
 
Mbaada ya kupitia ushahidi wote DPP kasema Mbowe alikuwa na kesi ya kujibu, ni nani kamfanya apige U turn? Wacheni uzuzu, nchi zetu za Afrika hizi hata jaji mkuu na DPP wote ni wateule wa Rais.
Hivyo bas hatuna mahakama huru, Rais ndie anaamua chochote atakacho? Wanaodai katiba mpya wapo sahihi ✔️
 
Wewe lazima ni ccm mnaohangaika kuwaweka KIKULACHO wenu ndani ya Chadema ili mkisambaratishe chama!! Kama mnawapenda sana wachukueni muwe nao.
Hiyo sio kweli, mchango wa Halima na Esther kwa chadema sio wa kutiliwa mashaka koboya kama hivyo unavyosema wewe. Lazima tukubali kuwa awamu ya tano haikuwa nzuri kwa demokrasia nchini, ukurasa ule lazima tuufunge sote kama taifa, Rais Samia ameanza kuufunga na sisi lazima tufanye hivyohivyo ndani mioyo yetu na vyama vyetu pia, tuuone kama upepo mbaya uliolipitia taifa letu. Hata Mama Samia upepo ule ulimpitia pia wa kuitwa majina mbalimbali hadharani. Ile sio tu kuwa ni historia kwa taifa letu lakini imetukumbusha sote kuhusu umakini katika kuchagua watendaji kwenye nafasi mbalimbali na kuwa na Katiba imara isiyotegemea utashi wa kiongozi wa siku hiyo ameamkaje.

Kuwaondoa akina Halima na Ester inaweza isiwe shida sana kwenye chama lakini shida inayoweza kukipasua chama vipandevipande ni sura za wale watakaokwenda kujaza nafasi zitakazoachwa na akina Mdee. Hapa namaanisha makabila na kanda watakazotoka, uhusiano wao na waasisi na viongozi wa chadema na mchango na uzoefu wao ndani ya chadema. Ni afadhali nafasi zao zikaachwa wazi ziende vyama vingine kuliko viongozi wa chadema kuingia kwenye mtego wa kupeleka "watu wao" bungeni kumalizia hiyo miaka 3 iliyosalia.

Kwetu tumezaliwa wasichana 5 na wavulana 3, baba yetu aliniambia mwanaume halisi hapigani na mwanamke, ikimaanisha kuwa sisi wanaume tusamehe zaidi dada zetu kuliko dada zetu wanavyowasamehe kaka zao.
 
Usijitoe ufaham, alisema Mbowe alienda kumshukuru
Hakuna ubishi Lisu na Mbowe walikwenda kwa mama kuomba na kushukuru. Mama ni mstaarabu lazima tuseme ukweli hata kama kufanya hivyo tunaona kutatudhoofisha. Tuna watanzania wenzetu waliogeuka wakimbizi, mama huyu hawezi kufika huko.
 
Mahakama imeingiliwa? Afu unasema dpp alipokea maelekezo (can you prove it?) ,Usiishi kwa hear sayings ,huo ni utoto.
dpp huyu ndiye yuleyule aliyekuwepo awamu ya tano na ndiye yuleyule aliemfutia Lisu na Mbowe makosa yao. Keep everything (IGP, PM, CDF, Jaji Mkuu, Gavana, etc) constant, then find the factor influencing the DPP to act differently in the two regimes (5 and 6).
 
Hapa Mh. Mbowe kabisa hajautendea haki msamaha wa Rais; yeye naye alitakiwa awasamehe pia wabunge hawa. After all, ni wabunge wa JMT na si wa CHADEMA
 
Hapa Mh. Mbowe kabisa hajautendea haki msamaha wa Rais; yeye naye alitakiwa awasamehe pia wabunge hawa. After all, ni wabunge wa JMT na si wa CHADEMA
kila mtu akibaki na sumu kwenye moyo wake nchi haitakalika. Nakubali kwamba chadema iwaite hawa wabunge wote kwenye chama ili wayajenge na the way forward kuelekea 2025, 2030. Chadema iwape agenda zake hawa wabunge akina Mdee maana wao ndio wanaofahamu kile kinachoendelea huko bungeni maana walikuwepo na wapo huko.
 
 
Anawafukuza wanawake madhubuti sana ambayo walikubali kupigwa na hata kuvunjwa miguu na mikono na vyombo vya dola kwaajili ya chadema, hawa ni wanawake ambao walikataa mamilioni ya fedha ili kwenda kuunga juhudi, wanawake wa aina hii ya Mdee na Ester hawazaliwi wengi duniani, wallah nakwambia chadema itafanya kosa ambalo litabaki kwenye kumbukumbu zao kwa miaka yote.
 
Hapa Mh. Mbowe kabisa hajautendea haki msamaha wa Rais; yeye naye alitakiwa awasamehe pia wabunge hawa. After all, ni wabunge wa JMT na si wa CHADEMA

Kama ni wa JMT basi waende huko kwenye serikali ndio iwape ubunge!! Kwanini mnalilia warudishwe CHADEMA? Mnataka kukihujumu chama sasa mnatafuta pa kuingilia!!
 
Tatizo lililopo Hawa wabunge Hawana faida yoyote Kwa chama
 
Waliamua kujufukuza wenyewe; mbowe hana cha kufanya.

Unapokiuka misingi ya taasisi unapofqnyia kazi hufujuzwi wala kusamehewa na boss, bali unafukuzwa nabtaasis husika, ina ku reject.
 
Bila shaka mmoja wa hao Covid 19 ni ndugu yako au hawara. Wasaliti unawapigiaje debe?
 
Bila shaka mmoja wa hao Covid 19 ni ndugu yako au hawara. Wasaliti unawapigiaje debe?
Kwahiyo unataka na wewe umpeleke hawara yako, tit for tat? Ukabila unakutafuna TU wewe, hivi Tanzania Kuna wanawake shupavu kama Halima na Esther? Wanaokubali kuswekwa lupango. Nakumbuka Halima alikuwa anakojolea kwenye kopo hadharani ndani ya chumba Cha kuhesabia kulinda kura za chadema zisiibiwe. Wacheni ujinga wenu wa uroho wa pesa. Walah kama Mbowe na Sugu wangetangazwa kushinda ubunge kwenye majimbo Yao kusingekuwa na kususia ubunge. Hela mbaya sana, tabia ya tume mbona ndiyo hiyohiyo kwenye chaguzi zote? Na malalamiko ya wapinzani mbona ndiyo hayohayo kwa chaguzi zote za vyama vingi. What is so special with this 2020 election results? The only different is all men not announced winners,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…