Mbowe: Ununuzi wa ndege siyo kipaumbele sahihi kwa nchi yetu zaidi ya Elimu, Afya na Miundombinu!

Mbowe: Ununuzi wa ndege siyo kipaumbele sahihi kwa nchi yetu zaidi ya Elimu, Afya na Miundombinu!

Naona Mbowe sasa akili imerudi anaongelea maendeleo ya vitu

njia ya mwongo fupi.Sasa kampeni za uchaguzi 2020 kwa nini walipinga maendeleo ya vitu?
Ndege anayemuongelea mbowe ni kiumbe hai,,sera ya chadema ni maendeleo ya watu na ndege ni mtu pia
 
Ununuzi wa midege toka nchi za mabeberu ni zigo la hasara kwa walipakodi wa Tanzania.

Ukiacha Ethiopia, hakuna shirika la ndege la nchi za Afrika linaloendeshwa kwa faida.

Na Ethiopia wameweza kwasababu walianzisha shirika lao zamani kabla biashara ya usafiri wa anga haijawa biashara kichaa.

JPM alisema Kagame ndio mshauri wake ktk ununuzi wa midege, lakini Kagame ameingia hasara kubwa na amelazimika kuomba ubia na Qatar Airways.

Ethiopian wana zaidi ya ndege 100 lakini sio kwa cash. Nyingi ni za kukodi (lease) na mkopo (lease purchase). Malipo yamepangwa kwa taratibu na mikataba ya kibiashara. Zinaweza kurejeshwa kwa mkopeshaji/muuzaji biashara isipoenda vizuri. Unaweza kukuta gharama ya kuwa na nusu ya ndege hizo haifikii tuliyotumia kununua zetu 12.

Hata hivyo wanakiri kuwa biashara hiyo ni ngumu sana na faida wanayopata ni kiduchu kulinganisha na nyingine kama za usafiri wa meli (ESLSE) na telecoms. Lakini Ethiopian Airlines ndiyo nembo ya taifa na wao ndio wanaongoza Afrika kwa uwezo wa biashara hiyo. Hivyo inabidi wakomae nayo tu.
 
Baba akinunua lori la mchanga tunapandaje nyumba nzima na hakuna siti za kutosha?

Watoto watakula faida inayotokana na lori na sio lazima wote wapande
Mtanzania anayeishi chini ya Dola 1 ya Tsh 2300 kwa siku ambao ni wengi anawezaje kumudu ticket ya ndege ya 230k hadi 300k ?
 
Ethiopian wana zaidi ya ndege 100 lakini sio kwa cash. Nyingi ni za kukodi (lease) na mkopo (lease purchase). Malipo yamepangwa kwa taratibu na mikataba ya kibiashara. Zinaweza kurejeshwa kwa mkopeshaji/muuzaji biashara isipoenda vizuri. Unaweza kukuta gharama ya kuwa na nusu ya ndege hizo haifikii tuliyotumia kununua zetu 12.

Hata hivyo wanakiri kuwa biashara hiyo ni ngumu sana na faida wanayopata ni kiduchu kulinganisha na nyingine kama za usafiri wa meli (ESLSE) na telecoms. Lakini Ethiopian Airlines ndiyo nembo ya taifa na wao ndio wanaongoza Afrika kwa uwezo wa biashara hiyo. Hivyo inabidi wakomae nayo tu.
Kwa mawazo yako haya watu wangekuwa wanapanga maishani mwao kuliko kujenga nyumba
 
Mbowe si ni yule mwenyekiti wa chama kisichokuwa na angalau kiwanja cha kujenga makao makuu licha ya kupata ruzuku za mamilioni kila mwezi? Sasa huyo ndo aje atupangie vipaumbele vya kitaifa?! Ama kweli nyani haoni 'nyuma yake'!
Haihusiani na hoja iliyopo mezani.Muwe mnatikisa hivyo vibebeo vya nywele kabla ya maoni yenu.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema kununua ndege siyo kipaumbele sahihi kwa maendeleo ya nchi yetu ukilinganisha na Elimu, Afya na Miundombinu.

Mbowe amesema uwekezaji kwenye ATCL unahitaji mtaji mkubwa, utaalamu uliotukuka kwa watu wetu na mbinu za kisasa kuhimili ushindani wa soko.

Hata hivyo msemaji wa serikali Dr Abbas amesema serikali kuwekeza katika ndege haimaanishi kuwa imeacha kuwekeza katika maeneo mengine.

Source BBC Dira ya Dunia

My take: Naona Mbowe ana hoja na Dr Abbas ameipangua kiufasaha.

Maendeleo hayana vyama!

Mbowe akili imeanza kumrudia polepole.
Hapo zamani alisema miundombinu ni vitu havina maana sasa anaaanza kurudi taratibu.
Elimu na afya ni vitu endelevu, kwani watu wanaongezeka na mahitaji yanongezeka, hakuna siku utaacha kuifanya hiyo kazi hivy ni upuuzi kusema ufanya kazi ya afya na elimu kisha vingine ukaviacha eti mpaka ukamilishe afya.
Mbowe anajua, alinunua gari la bei kubwa wakati sehemu ya kutunzia afya yake makao makuu ya chama nyumba mbovu.
Kwa hiyo yeye hakyona umuhimu wa nyumba kwanza ila gari?
Unasomesha wati bila miundombinu ya kufanyia kazi sasa unatafuta vita ndani ya nchi kwa hao wasomi?

Kwani mpaka sasa wataalamu wa ndege na hiyo biashara hawapo hapa tanzania au kuna vhuo cha kuwasomesha ili wajue utaalamu wa biashara na nchi yetu hao watu hawapo?

Najua tuaelewana nae tu ngona aendelee kuonyeshwa makali ya ujenzi wa nchi.
 
Hivi Mbowe ana hata 1% ya shida ulizonazo wewe?? Yeye hizo ndege anazipanda sana, sasahivi yuko Dubai anakula maisha huko, wewe uko wapi sasahivi?? Umeshapanda hizo ndege mara ngapi?
Yap..yuko Dubai anakula maisha na kupumzisha akili baada ya misukule yake kushindwa kumpa bata ubunge
 
Mtanzania anayeishi chini ya Dola 1 ya Tsh 2300 kwa siku ambao ni wengi anawezaje kumudu ticket ya ndege ya 230k hadi 300k ?
Nchi gani kila mtu anapanda ndege? Ungejua hata mabasi kuna watu hawana uwezo wa kupanda usingeandika utumbo wako hapa. Acha wenye uwezo watumie usafiri wanaoweza. Wewe tumia unaoweza
 
Halafu jiwe ana tabia ya kujibu kabla hajasikia,je kwenye mithali haijaandikwa yeye ajibuye kabla hajasikia ni mpumbavu
 
Back
Top Bottom