Kwanza nianze kumshukuru Jemedari Mama Samia kwa kuniwezesha kukomenti!Habari za Mchana wanajamvi
Kwanza nianze kumshukuru Dr Samiah Suluhu Hassan kwa kuniwezesha kuanzisha thread,yeye ndiyo karuhusu JF iwepo angeamua isingekuwepo.
Mbili jamani Mwanadamu ni Selfish by Nature hivi inakuwaje Mbunge unajilipa Mil 18 na Maposhoposho juu huku Mwalimu analipwa Laki nne?Huku ndiyo kuongoza kwa Mfano?
Nashauri kama ambavyo Katiba Mpya inahitaji Bunge Maalumu huru lisilo na Mgongano wa Maslahi hili la Mishahara na Posho pia linahitaji Bodi Maalum huru isiyo na Mgongano wa Maslahi.
Suala la Mishahara ni usalama wa nchi msije mkasema sikuwaambia.
Nimekaa paleee.
PorojoHili Jukwaa hakulianzisha Raisi Samia. Muwe wakweli.
Itoshe, hakuna anayeweza kufunga Internet. Hilo haliwezekani
Hivyo basi, ile nadharia kwamba Internet ilifungwa au Jamiiforums Ilifungwa, haina mashiko-ni Upotoshaji.
CHADEMA wanapokea ruzuku kwa Uchaguzi walioukataa, kwa Serikali waliyokataa na kuitambua. Huo ni unafiki kuendelea kupokea hela za Walipa kodi.
Turudi kwa msharhara wa 18 millioni, hizo nazo ni fedha za Walipa kodi, Je, CHADEMA wapo tayari kukataa Mshahara huo.Je, ni Kwanini wasianze na Mbunge wao, kama mfano?
Ina maana huko Kenya hakuna vijana wanaoshabikia michezo? Hao vijana wa Kenya walioingia barabarani ni asilimia ngapi ya vijana wote wa Kenya?Vijana kenya wanaingia barabarani.....Tz kazi kushabikia simba na yanga