Mbowe: Wabunge wamejiongezea Mishahara Kutoka Tsh milioni 13 za awali na sasa wanalipwa Tsh milioni 18 kwa mwezi mbali na posho

Mbowe: Wabunge wamejiongezea Mishahara Kutoka Tsh milioni 13 za awali na sasa wanalipwa Tsh milioni 18 kwa mwezi mbali na posho

Mwenyekiti wa Chadema mh Freeman Mbowe amesema Wabunge wa Bunge la JMT wamejiongezea Mishahara kutoka TSH 13 million walizokuwa wanalipwa awali hadi TSH 18 million

Mbowe amesema mshahara huo ni mbali na Posho mbalimbali wanazolipwa kila Siku

Jumaa Mubarak 😀🔥

----
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Freeman Mbowe amedai kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamejiongezea mishahara yao kutoka milioni 13 waliyokuwa wanapata hapo awali hadi kufikia milioni 18 kwa mwezi, hiyo ikiwa ni nje ya posho ya vikao anayopatiwa Mbunge kila anapohudhuria kikao kimoja cha Bunge

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Machi 21.2024 Babati mjini, mkoani Manyara Mbowe amesema kuwa mara nyingi viongozi wa serikali wamekuwa wakijitokeza hadharani na kueleza kuwa uchumi umekua hapa nchini, jambo ambalo anakubaliananalo kwa kutumia kipimo cha pato la Taifa (GDP) lakini ameeleza kuwa uchumi huo umekua kwa watu wachache walioko serikalini na sio kwa mtu mmoja mmoja au jamii kwa ujumla wake

Amesema viongozi walioko serikalini wamekuwa wakiendekeza maisha ya anasa ambayo kwa kiasi kikubwa hayaangalii maslahi ya nchi na wananchi wake ndio maana inawawia vigumu kukubali kufanya marekebisho ya msingi ya sheria za nchi kutokana na msingi wa uwepo wa Katiba mpya

Ametolea mfano kupitishwa kwa sheria ya mafao ya wenza wa viongozi kama sehemu ya anasa hizo kwa kuwa sasa mwenza wa Rais mstaafu analazimika kupokea asilimia 60 ya mshahara wa Rais aliyeko madarakani, wakati Rais mstaafu akipokea asilimia 80 ya mshahara huo, hiyo ikienda sambamba na kupatiwa magari yanayobadilishwa kila baada ya muda, walinzi, nyumba na watumishi wengine binafsi.

Chanzo: Jambo Tv
Sisi hatuna wabunge bali tuna wachumiatumbo wakubwa. Kama ingewezekana nchi hii irudi kwenye utawala wa kichifu au mkoloni arudi kutawala tungekuwa mbali sana kiuchumi. Sijawahi kuona nchi ya kipumbavu kama hii nchi ya kusadikika.
 
Ulikuwa hujui?

Ncho ya wajinga. Watu wanagawana 18m plus kwa mwezi, akina Mwashambwa wanabweka kila siku kusifia kwa malipo shilingi 10,000 kwa siku, yaani laki 3 kwa mwezi! Halafu anajiona amefanikiwa sana!!
Mimi silipwi na mtu yeyote yule kwa ajili ya kuandika hapa jukwaani.kama unao huo ushahidi basi naomba uweke hapa jukwaani, kuliko kufanya kazi ya kunichafua na kunidhalilisha bila sababu ya msingi.
 
Back
Top Bottom