Mbowe: Waliokimbia CHADEMA watarudi, tutawasamehe dhambi zao

Mbowe: Waliokimbia CHADEMA watarudi, tutawasamehe dhambi zao

Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa, Freeman Mbowe amesema Chama hicho kikisema kinajenga uadui wa kudumu na watu waliohama, watakuwa haitakii mema Nchi...
... huyu jamaa ni mwamba wa siasa sio siri!
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Ndiyo hapo mnapokosea!!! Ndiyo maana mtaendelea kufanyiwa hivyo hivyo na namna hii dola mtaisikia tu!!! Muwe na misimamo. Mkishajua huyu mamluki mumkimbie kama ukoma, sasa nyie mnakumbatia spies!!! halafu mnawaingiza hadi kamati kuu!!!! Hapa ndiyo huwa nawashangaa sana CDM! Yaani wale wapuuzi akina silinde and comapany 2025 mtawakaribisha tena!!!!! Siasa bwana. Heri tusio wanasiasa!!!!
... siasa haziko hivyo wewe!
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Kisheria huruhusiwi kumkataa yeyote atayetaka kujiunga na chama chochote akitakacho, mkikosea kwenye hilo chama kinaweza kufutiwa usajili.
Mkuu huoni aibu kuandika hili uliloandika? Hiyo kauli ya Mbowe ina ukakasi sana, ila wafia Mbowe hamtaacha kumtetea hata afanye nini.
 
Sawa warudi ni haki yao kiatiba, lakini wasipewe ridhaa ya kugombea nafasi yoyote kwenye chama kwasababu walishaonesha wanaweka maslahi yao binafsi mbele zaidi ya chama, hawaaminiki tena, na huo msamaha ni vyema uwe public.
Wanataka lowasa na nyalandu warudi chama hakina hela

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Nadhani kabla hatujajipa majibu juu ya kauli ya Mbowe ni vyema tukasubiri ili tuone ndo tutoe hisia maana tunaweza kua na majibu yetu juu ya kauli yake kumbe uwanjani mambo ni tofauti
 
Yaani na mie nilivyooona tu heading ya hii thread waz namba moja nikakumbuka maneno ya Pascal Mayalla kuwa uongozi wa Chadema unawahadaa wanachama wao na wanajua kila kitu kuhusu Covid 19 na WATAWASAMEHE KWA 100%, tayari dalili ndio hizi zimeanza ngoja tuone
Sio kweli, tuache kupiga ramli
 
Mbowe bado anatakiwa kuulizwa kwanini zile rufaa walizokata wale 19 bado hazisikilizwi mpaka leo, shida iko wapi? akiendelea kukaa kimya wanaanza kuonekana matapeli.
Hii alishaijibu kwamba Baraza Kuu linakusanya watu wengi manake sio Kikao cha watu wachache kwenye Katiba vikao vya kamati kuu nadhani vinaitishwa mara mbili kwa mwaka habari za Rufaa sio dharula so watulie watasikilizwa
 
Maelezo mazuri, na moja ya consequence ya wale Covid ni kuvuliwa nafasi za uongozi walizokuwa nazo, na kutopewa nafasi ya kuongoza chama mbele ya safari.
Kuwa mwanachama sio tatizo
 
Dunia hii kuna watu hawana msimamo
 
Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa, Freeman Mbowe amesema Chama hicho kikisema kinajenga uadui wa kudumu na watu waliohama, watakuwa haitakii mema Nchi.

Amesema, "Tunatakiwa tuwapokee wote, waliokimbia watarudi tutawasamehe dhambi zao. Tutajenga CHADEMA kuwa Chama Kiongozi. Tusivae utakatifu, sisi sote ni binadamu, tuna mapungufu yetu."

Amefafanua, Chama hicho kinapigania Haki za Watanzania wa Vyama vyote hata CCM akisisitiza lengo ni kuwa na Taifa lenye mshikamano.
Amesema, "Tunatakiwa tuwapokee wote, waliokimbia watarudi tutawasamehe dhambi zao. Tutajenga CHADEMA kuwa Chama Kiongozi. Tusivae utakatifu, sisi sote ni binadamu, tuna mapungufu yetu."[emoji736][emoji736][emoji817]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom