Wadau nawasabahi
Naomba moja kwa moja niingie kwenye Maada naamini ni MUHIMU kwa CHADEMA sio kwa CCM.
Viongozi wa CHADEMA hebu kwanza Jiulizeni Swali hili.
Kwanini Mzee LOWASSA SUMAYE MAKAMBA NYALANDU KINANA na Wengine pamoja na kufanya MAKOSA MAKUBWA ndani ya Chama ikiwa na kujiunga na CHADEMA (Lowassa Nyalandu na Sumaye) lakini CCM iliamua KUWASAMEHE na kuwarudisha KUNDINI?
Je, mmewahi kujiuliza Walichokifanya Mzee Makamba na Kinana lakini CCM imewarudisha KAMBINI?
Je, mmewahi kujiuliza kwanini HALIMA MDEE na Wenzake 18 walikubali kuteuliwa na TUME ya Uchaguzi na Kuapishwa nje ya Bunge na mwingine kutolewa Gerezani Usiku je mnajua VITISHO walivyopewa na Aliyeagiza hayo yote yafanyike na je mnajua kwanini alifanya hivyo kwa CHADEMA na Sio kwa VYAMA vingine vya Upinzani?
Je kina HALIMA MDEE na Wenzake pamoja na Chadema kuwafukuza je Wamejiunga na CCM au Chama kingine? Kati ya MAKOSA Makubwa ndani ya Chama chochote cha Siasa ni Mwanachama KUKISALITI Chama chake na kujiunga na Chama Pinzani Mzee Lowassa na Sumaye Walifanya hivyo LAKINI CCM imewasamehe na Kuwarudisha kwani Walikuwa wanaipa nguvu CHADEMA na CCM ili kupunguza nguvu za Chadema ilifanya MAAMUZI MAGUMU ya kuwarudisha na kweli kuondoka kwa LOWASSA na SUMAYE kuliitikisa Chadema na kuiimarisha Ccm kwani Wafuasi wa Lowassa nao waliiacha Chadema.
HALIMA MDEE na Wenzake hawakuutafuta UBUNGE wa VITI MAALUM bali Walitafutiwa kwa nguvu na kwa VITISHO na Wenye MAMLAKA na ndio maana Mchakato wa kuwapa Ubunge Chadema hawakushirikishwa na pamoja na Chadema kufuata taratibu zote za KUWAFUKUZA UANACHAMA ili Wafukuzwe BUNGENI bado ZIMESHINDIKANA licha ya KATIBA kusema WAZI kuwa Huwezi kuwa Mbunge bila kuwa Mwanachama wa Chama cha Siasa LAKINI HALIMA MDEE na Wenzake 18 Sio Wanachama lakini bado WAPO Bungeni na kufanya juhudi za Chadema kutaka WAONDOLEWE Bungeni zimegonga MWAMBA. Hivi CHADEMA Mmewahi kujiuliza kwa NINI na nani Anawalinda Hao kina HALIMA MDEE na Wenzake 18?
Aliyewapa Ubunge HALIMA MDEE na Wenzake 18 alikuwa na NIA ya kuidhihofisha Chadema na Nia hiyo bado inaendelea mpaka 2025 na Chadema Kesi yenu na HALIMA MDEE na Wenzake 18 LAZIMA MTASHINDWA TU ili HALIMA MDEE na Wenzake 18 Wamalize Miaka 5 BUNGENI kama CCM ilivyopanga.
CHADEMA kitendo cha KUWAFUKUZA HALIMA na Wenzake 18 Mliingia na Kunaswa na Mtego wa CCM .Ili KUJINASUA lazima mkubali kuwa HALIMA MDEE na Wenzake 18 Walilazimishwa na kutishwa na mwingine kutolewa Gerezani Usiku. CHADEMA kubalini kuwa HALIMA MDEE na Wenzake 18 SIO WASALITI hivyo basi WASAMEHENI na KUWARUDISHA KUNDINI ili KUJITOA ktk MTEGO wa CCM wa Kukidhoofisha Chama chetu.HALIMA Mdee na Wenzake 18 SIO Wasaliti na Wangekuwa WASALITI wangekwisha JIUNGA na CCM au Chama kingine.
Jiulizeni.
KWANINI CCM Imewarudisha Wanachama wake kina LOWASSA SUMAYE NYALANDU KUNDINI kwanini HAIKUWAACHA waendelee kuwa CHADEMA?
CHADEMA msione AIBU Hebu WARUDUSHENI KUNDINI WANACHAMA wenu HALIMA MDEE na Wenzake 18
Mtakuwa MMEIBWAGA CCM kwenye huu MTEGO.