Mbowe warudishe Halima na wenzake kundini kwanza

Mbowe warudishe Halima na wenzake kundini kwanza

Umeandika vema kabisa. Lakini sasa huyu utamwamini kumpa nafasi kwenye kundi lako? Umemkuta amelala na mwanamume kitandani kwako, unafanyaje? (inaweza mfano huu umekwenda juu sana).

Akina Lowasa ni malaya wa kisiasa na kama Chadema at that time ingeliingia madarakani, wasingerudi CCM, Am I wrong?
Kitanda sheikh hakizai haramu. Ungekuwa upuuzi kama nafasi zile zingejazwa na maccm. Bora ya hivi
 
Mgogoro wa CHADEMA na akina Halima ulipangwa kama mkakati wa kujiua chama cha chadema.

Chadema msikubali kunaswa na mtego huo. Warudisheni kundini makamanda wetu akina Halima na wenzake.

Hii itaifanya CCM itetemeke na CHADEMA iheshimiwe kimataifa. Kama CCM imewarudisha kundini Lowasa, Sumaye na wengine kwanini ishindwe kutafuta muafaka na wasichana wao makamanda.

Nijuavyo mimi akina Halima walitumbukia kwenye mtego wa kimasilahi tu na vitisho baaasi.
Weka namba yako ya kadi ya uanachama wa Chadema.
 
Chadema rudini nyuma mmeze ego zenu na mrudishe wale kina mama walahi
Mchango wao ulikuwa ni mkubwa sana na kwa kweli pengo waliloliacha ni kubwa sana!
Waliitwa kwenye vikao wakagoma kwenda,wangeeleza kilichotokea na kuomba msamaha hilo lingewezekana. Mtu anayesamehewa ni yule anayekiri kosa kisha kuomba msamaha sasa hawa wameamua kutunishiana misuli na chama kwa kwenda Mahakamani huku wakipata backing ya CCM.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Mgogoro wa CHADEMA na akina Halima ulipangwa kama mkakati wa kujiua chama cha chadema.

Chadema msikubali kunaswa na mtego huo. Warudisheni kundini makamanda wetu akina Halima na wenzake.

Hii itaifanya CCM itetemeke na CHADEMA iheshimiwe kimataifa. Kama CCM imewarudisha kundini Lowasa, Sumaye na wengine kwanini ishindwe kutafuta muafaka na wasichana wao makamanda.

Nijuavyo mimi akina Halima walitumbukia kwenye mtego wa kimasilahi tu na vitisho baaasi.
Once a traitor always a traitor.. Tulishatoka huko.. Kama wakati una rivasi basi tunawarudisha
 
kama wakirudishwa kundini hata ruzuku ya chama uliyozuiliwa utarudishwa kundini pia, wee veepe!!
Kazi unayo Kavulata. Ruzuku imezuiluwa au wao wameigomea hawataki kula haramu? Jitahidi kujya vitu vigodovigodo kiufasaha kama hivi ili mada zako ziwe na nguvu. Vinginevyo ukizoeleka kwa mada puuzi mwishowe hutapata wachangiaji

Sent from my SM-G977B using JamiiForums mobile app
 
Mgogoro wa CHADEMA na akina Halima ulipangwa kama mkakati wa kujiua chama cha chadema.

Chadema msikubali kunaswa na mtego huo. Warudisheni kundini makamanda wetu akina Halima na wenzake.

Hii itaifanya CCM itetemeke na CHADEMA iheshimiwe kimataifa. Kama CCM imewarudisha kundini Lowasa, Sumaye na wengine kwanini ishindwe kutafuta muafaka na wasichana wao makamanda.

Nijuavyo mimi akina Halima walitumbukia kwenye mtego wa kimasilahi tu na vitisho baaasi.
ukweli uko wazi ndugu akina halima waliidhunidhwa na mbowe
 
Wadau nawasabahi

Naomba moja kwa moja niingie kwenye Maada naamini ni MUHIMU kwa CHADEMA sio kwa CCM.
Viongozi wa CHADEMA hebu kwanza Jiulizeni Swali hili.

Kwanini Mzee LOWASSA SUMAYE MAKAMBA NYALANDU KINANA na Wengine pamoja na kufanya MAKOSA MAKUBWA ndani ya Chama ikiwa na kujiunga na CHADEMA (Lowassa Nyalandu na Sumaye) lakini CCM iliamua KUWASAMEHE na kuwarudisha KUNDINI?

Je, mmewahi kujiuliza Walichokifanya Mzee Makamba na Kinana lakini CCM imewarudisha KAMBINI?
Je, mmewahi kujiuliza kwanini HALIMA MDEE na Wenzake 18 walikubali kuteuliwa na TUME ya Uchaguzi na Kuapishwa nje ya Bunge na mwingine kutolewa Gerezani Usiku je mnajua VITISHO walivyopewa na Aliyeagiza hayo yote yafanyike na je mnajua kwanini alifanya hivyo kwa CHADEMA na Sio kwa VYAMA vingine vya Upinzani?

Je kina HALIMA MDEE na Wenzake pamoja na Chadema kuwafukuza je Wamejiunga na CCM au Chama kingine? Kati ya MAKOSA Makubwa ndani ya Chama chochote cha Siasa ni Mwanachama KUKISALITI Chama chake na kujiunga na Chama Pinzani Mzee Lowassa na Sumaye Walifanya hivyo LAKINI CCM imewasamehe na Kuwarudisha kwani Walikuwa wanaipa nguvu CHADEMA na CCM ili kupunguza nguvu za Chadema ilifanya MAAMUZI MAGUMU ya kuwarudisha na kweli kuondoka kwa LOWASSA na SUMAYE kuliitikisa Chadema na kuiimarisha Ccm kwani Wafuasi wa Lowassa nao waliiacha Chadema.

HALIMA MDEE na Wenzake hawakuutafuta UBUNGE wa VITI MAALUM bali Walitafutiwa kwa nguvu na kwa VITISHO na Wenye MAMLAKA na ndio maana Mchakato wa kuwapa Ubunge Chadema hawakushirikishwa na pamoja na Chadema kufuata taratibu zote za KUWAFUKUZA UANACHAMA ili Wafukuzwe BUNGENI bado ZIMESHINDIKANA licha ya KATIBA kusema WAZI kuwa Huwezi kuwa Mbunge bila kuwa Mwanachama wa Chama cha Siasa LAKINI HALIMA MDEE na Wenzake 18 Sio Wanachama lakini bado WAPO Bungeni na kufanya juhudi za Chadema kutaka WAONDOLEWE Bungeni zimegonga MWAMBA. Hivi CHADEMA Mmewahi kujiuliza kwa NINI na nani Anawalinda Hao kina HALIMA MDEE na Wenzake 18?

Aliyewapa Ubunge HALIMA MDEE na Wenzake 18 alikuwa na NIA ya kuidhihofisha Chadema na Nia hiyo bado inaendelea mpaka 2025 na Chadema Kesi yenu na HALIMA MDEE na Wenzake 18 LAZIMA MTASHINDWA TU ili HALIMA MDEE na Wenzake 18 Wamalize Miaka 5 BUNGENI kama CCM ilivyopanga.

CHADEMA kitendo cha KUWAFUKUZA HALIMA na Wenzake 18 Mliingia na Kunaswa na Mtego wa CCM .Ili KUJINASUA lazima mkubali kuwa HALIMA MDEE na Wenzake 18 Walilazimishwa na kutishwa na mwingine kutolewa Gerezani Usiku. CHADEMA kubalini kuwa HALIMA MDEE na Wenzake 18 SIO WASALITI hivyo basi WASAMEHENI na KUWARUDISHA KUNDINI ili KUJITOA ktk MTEGO wa CCM wa Kukidhoofisha Chama chetu.HALIMA Mdee na Wenzake 18 SIO Wasaliti na Wangekuwa WASALITI wangekwisha JIUNGA na CCM au Chama kingine.
Jiulizeni.

KWANINI CCM Imewarudisha Wanachama wake kina LOWASSA SUMAYE NYALANDU KUNDINI kwanini HAIKUWAACHA waendelee kuwa CHADEMA?

CHADEMA msione AIBU Hebu WARUDUSHENI KUNDINI WANACHAMA wenu HALIMA MDEE na Wenzake 18
Mtakuwa MMEIBWAGA CCM kwenye huu MTEGO.

JamiiForums-1998729802.jpg
1744462805.jpg
1652427482224.jpg
 
Nimemuona babu Balozi Dr Slaa baada ya kutumiwa na CCM kisha mke kumkimbia wakiwa CANADA anaanza kuhudhuria mikutano ya hadhara ya CHADEMA
 
Kunduni tena😂😂😂😂warudishwe kwenye kundu la nani ambalo ni kubwa kiasi cha kutosha watu 19😂😂😂😂
Screenshot_20230302_075504.jpg
 
Wayamalize nje ya mahakama na warudishwe kwa vile siasa na hali ya kisiasa imebadilika,Samia/Tulia awafukuze kwanza Bungeni . CDM wafanye political cost/benefit analysis kuona faida na hasara za kisiasa na political opportunity,wakati mwingine maamuzi ya kisiasa hayapaswi yawe rigid hivyo muhimu ni kuangalia fursa,warudishwe hao walisumbuliwa na njaa na madeni ya mabenki tu, na siyo dhamira ya kukisaliti chama haswa, hawa bado ni asset iwapo wataokoka a' la pentecoste na kutumiwa vizuri kimkakati.
 
How? Nipe facts tafadhali
Kwani chadema inapokea ruzuku Yao?
ukweli uko wazi ndugu akina halima waliidhunidhwa na mbowe
hata mm ningefanya hivyohivyo, hakuna siasa bila uchumi. Kuachia nafasi za ubunge wa viti maalum zipotelee CCM ungekuwa ujuha +++. Mpango wa akina halima kwenda bungeni haukuwa wa Job ndugai peke yake bila kuhusika kwa watu wengi sana muhimu. Ulikuwa ni mpango wa kuinusuru nchi dhidi ya vikwazo vya mabeberu. Akina halima unawaonea bure kuwalaumu. Kwanye mpango huo lazima hata baadhi ya officials wa chadema walikuwemo.
 
weee!!! hao ni wapambanaji kumshinda hata Mnyika.
Sellouts hao, hakuna mpambanaji ambaye angekubali kuwa chawa wa Jiwe na lile subwoofer lake Ndugai. Walishapiteza trust labda waombe upya uanachama na kila mmoja kivyake wachunguzwe na wakiri hadharani usaliti wao.
 
Kwani chadema inapokea ruzuku Yao?

hata mm ningefanya hivyohivyo, hakuna siasa bila uchumi. Kuachia nafasi za ubunge wa viti maalum zipotelee CCM ungekuwa ujuha +++. Mpango wa akina halima kwenda bungeni haukuwa wa Job ndugai peke yake bila kuhusika kwa watu wengi sana muhimu. Ulikuwa ni mpango wa kuinusuru nchi dhidi ya vikwazo vya mabeberu. Akina halima unawaonea bure kuwalaumu. Kwanye mpango huo lazima hata baadhi ya officials wa chadema walikuwemo.
Asante kwa kunielewa ni wenye AKILI KUBWA ndio wataelewa kwanini Tunataka Wasamehewe na Kurudishwa KUNDINI
 
Back
Top Bottom