Mbowe yuko huru, Sabaya nae aachiwe

Ili aje kuendelea kukata watu masikio na kubaka binti zetu kwa kutumia cheo chake. Acha kwanza abakwe na nyapara wakimalizana naye ndo aje huku
 
Kwanini hata ccm wenzie mmemwacha azame peke ?
 
Unamhusisha vipi Mbowe na Sabaya? Mbowe hajahukumiwa na Sabaya kahukumiwa. Tumia vizuri "grey matter" yako fuvuni.
 
Wewe ni punguani wa taifa kwa kulinganisha tuhuma za hawa watu wawili (Sabaya na Mbowe)!
 
muwe na akili hata kidogo unawezaje kufananisha jambawazi na mtu huru asiye hata na kosa la kuiba penseli darasani? muwe na akili nasisitiza hilo Period.
 
Kwani Mbowe kasamehewa?
Huyo Sabaya kapatikana na hatia kwa makosa yake ambayo alipotakiwa atoe utetezi mahakamani alisema eti aliyatenda hayo akitekeleza maagizo ya mamlaka yake ya uteuzi! Na wala hajaomba msamaha licha ya kutiwa hatiani. Nasikia amekata rufaa, asubiri uamuzi wa rufaa yake.

Msitake kufananisha jambazi aliyetiwa hatiani kwa ushahidi wa dhahiri (Sabaya) na raia mwema aliyebambikiwa kesi isiyo na ushahidi (Mbowe)
 
Kabla ya Mbowe kuachiwa, mahakama ilisema anakesi gani ya kujibu?
 
Sabaya ni jambaz amechukua hela za watu,
Akiachiwa nani atarejesha hizo hela?
Na kabaka, nani atahukumiwa badala yake ktk ubakaji?
 
Huyo alishahukumiwa... Mbowe hakufika hatua hiyo...
 
Taifa lina safari ndefu sana kuelimisha watu wake, watu hawaelewi tofauti ya kukutwa na hatia na kusemwa una kesi ya kujibu. Unaweza kukuta watu wa hivi wana digirii kabisa lkn vichwani hakuna maarifa
Hilo tatizo nimeliona. Halafu hata hawataki kuhangaisha vichwa vyao kufahamu tofauti kati ya kukutwa na KESI ya kujibu na kukutwa na HATIA. Ukikutwa na KESI ya kujibu katika utetezi wako unaweza USIKUTWE na HATIA na ukaachiwa HURU.

Kwa kesi ya Mbowe Jamhuri iliona kabisa Mbowe HAWEZI kutiwa HATIANI kwa ushahidi wa kijinga waliokuwa nao. In fact kama jaji angetumia haki alitakiwa amwachie huru siku ile yaani Hakukuwa na kesi ya kujibu pale.
 
Kitengo mpo kazini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…