LGE2024 Mbowe yuko sahihi Mgombea Kujaza Fomu siyo Mtihani ni kuweka tu Kumbukumbu zake kimaandishi kwenye Mfumo wa Pamoja!

LGE2024 Mbowe yuko sahihi Mgombea Kujaza Fomu siyo Mtihani ni kuweka tu Kumbukumbu zake kimaandishi kwenye Mfumo wa Pamoja!

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
CCM wa aina yako huwa hatuwapi nafasi za juu za uongozi. Tunataka CCM kama akina Mwashambwa lakini wawe na akili angaa kidogo. Huyu Lucas amechezewa chezewa sana ni aibu kumpa vyeo. Wapinzani watatucheka.
Wamemfanya kama pombe ya ngomani watu wanajichotea tu.
 
Nimecheka sana hii heading

Ujue kweli kuna vitu vingine hata huku makazini unakuta unakaziwa hadi nukta, hati na ujinga mwingine mdogo dogo mpaka unajiuliza hivi nimeleta barua ya kufuatilia haki zangu au nipo kwenye interview!?
 
Hili linafikirisha sana, kwamba wagombea wa ccm wote hakuna asiyejua kujaza form. Lakin wale wa upinzan hawajui kujaza.
Wapi, tuna mwenyekiti wetu ukifika ofisini anakupa form ujaze mwenyewe, hapo mtamalizia ile ya uchaguzi alijazaje. Labda huwa wanajaziwa
 
ni muhimu sana kua makini na serious kwenye mambo muhimu ya msingi,hasa ya kisheria na kikatiba..

unaweza kua sahihi kusema, lakini ukakosea vibaya sana kutenda.

haikubaliki kunajisi sheria na katiba ya nchi kwa kukosea au kukiuka kwako miiko, vigezo na masharti mahususi yaliyowekwa kama utaratibu wa kuwashindanisha wenye mawazo na fikra tofauti.

kuzingatia sheria ni suala mtambuka jumuishi. Asie zingatia hilo ni muhuni tu 🐒
Unadhani wapinzani wote wammekosea na CCM wote wamepatia inakuja akilini? Wakati mwingine muongee mambo yenye tija kwa nchi siyo tija ya matumbo yenu.
 
Gentleman,
hayo ya huko x na spaces, kutwa kucha kaupotoshaji hako hako tu mnatembea nako,

wakati huyo si miongoni mwa wagombea uongozi popote nchini, ila mmeokota picha ya hata asiehusika mkajaza fomu mjuavyo ili kuvutia huruma ya wananchi..

hiyo ni useless,
kampeni zinaanza rasmi kesho na uchaguzi ni tar 27 Nov 2024🐒
Dogo,
Hakuna upotoshaji wowote hapo.
Kwenye hiyo fomu jina la mhusika lipo, namba ya simu ipo na location ni Arusha. Wacha kulialia, mpigie ujiridhishe
 
Dogo,
Hakuna upotoshaji wowote hapo.
Kwenye hiyo fomu jina la mhusika lipo, namba ya simu ipo na location ni Arusha. Wacha kulialia, mpigie ujiridhishe
kwahiyo gentleman,
tuahirishe uchaguzi nchi nzima tukajiridhishe sio?🤣
 
Unadhani wapinzani wote wammekosea na CCM wote wamepatia inakuja akilini? Wakati mwingine muongee mambo yenye tija kwa nchi siyo tija ya matumbo yenu.
Gentleman,
wapinzani wengi hawajajiandikisha kwenye daftari la wakazi wa eneo husika na kwahiyo hawatambuliki lakini, lakini ETI wamepotoshana wao kwa wao, wameenda kuchukua fomu ati nao wagombee🤣


wanachama wa CCM wote nchi nzima zaidi ya milioni 35 wamejiandikisha na kwahiyo hiyo inathibitisha kua ni wakazi wa eneo husika wanatambulika na kwahiyo wengi wao wamejaza fomu hapo hapo ofisini na kuirudisha...

sasa wapinzani mpaka waipeleke fomu kwa mganga kwajili ya ushirikina, watashinda kweli uchaguzi 🤣
 
Back
Top Bottom