The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Baadhi ya walimu na Wajumbe wa Chama cha Walimu (CWT), wilayani Mbozi, mkoani Songwe, wameomba viongozi waliochaguliwa kuwaongoza kwa awamu nyingine kuhakikisha wanatetea maslahi yao ikiwa ni pamoja na kuishauri serikali kuondoa makato ya asilimi mbili ambayo hukatwa kwenye mishahara yao .
Walimu na wajumbe hao wameyasema hayo mara baada ya kumaliza zoezi la kuwachagua viongozi wao ngazi ya Wilaya, ambapo wameongeza kuwa licha ya serikali kuendelea kuboresha sekta ya elimu hasa upande wa miundombinu ya kusomea ipo haja ya kuboreshewa maslahi yao ikiwemo kuondoa hizo asilimia mbili za makato.